Mtaka Haki
JF-Expert Member
- Oct 1, 2010
- 492
- 149
Mh. Makamba ( Katibu Mkuu wa CCM) naomba unijibu hata kupitia kwa January Makamba ambaye huwa humu JF kwa jina jingine.
Ulisema CHADEMA hawakutii amri halali.
1. Je ukiwa na barua ya kukuruhusu kuandamana, kisha pakatokeo taarifa kwa mdomo kuwa umezuiwa kuandamana bila maandishi. Utatii amri ipi?
2. Kama polisi walikuwa na taarifa za kiitelijensia kuwa kuna shida itatokea na ndio maana wakawa wengi mno hata kutoka mikoa mingine kuzuia maandamano. Kwa nini wingi huo usitumike kuzuia yaliyokusudiwa katika taarifa hizo za kiitelijensia?
3. Unadhani kama kweli kuna taarifa za kweli zilizoonyesha kusudio lolote baya, je kwa nguvu iliyotumika na maisha yaliyoondolewa na waliojeruhiwa ( waliokuwamo na wasiokuwamo) imesaidia kugeuza ubaya wa yeyote aliyekusudia mabaya au mmewaongezea mashabaki hao waliokusudia mabaya?( kama kweli wapo waliokusudia mabaya)
4. Ni kwa nini vurugu haikutokea kabla ya polisi kuanza kuzuia maandamano?
5. Hata kama umezuiliwa kuandamana lakini ukapewa kibali cha mkutano wa hadhara. Je watu waende kwenye huo mkutano kwa Helkopta ili wasikamatwe kwa kuandamana? Je unaweza kuwawekea watu muda maalum wa kwenda kwenye mkutano mtu moja mmoja ili wasiende kwa pamoja au kwa makundi?
6. Kama kinacholindwa ni UMEYA na siyo wananchi wanaohudumiwa na meya huyo, ukishawaua utawasimamiaje?
7. Je CCM inaiheshimu mamlaka iliyo kuu (katiba) ambayo ndiyo mamlaka kuu kuliko zote?
TAFADHALI NIJIBU.