Ndio sababu viongozi wakuu mara kwa mara wanaomba waombewe kwani kazi iliyo mbele yao ni kubwa na mzito.Tuliangalie hili kwa makini sana. Jana wakati Waziri Mkuu akiwa anatembelea kukagua Kurasini Oil Jet (KOJ) aliambatana na Mkurugenzi Mtendaji wa Wakala wa Vipimo (WMA) pamoja na wakubwa wengine. Swali alilomuuliza huku akitaka maelezo yake yatolewe ni ......KWA NINI ULIAMUA KUWASHA METER JANA BAADA YA KUTUMIWA UJUMBE WA SMS?...... Kwa jicho la weledi ni kwamba katika timu ya watakatifu waliowazunguka Majaliwa na JPM wapo wanaouza taarifa kwa watuhumiwa watarajiwa.
Kiintelejensia hili limekaaje?
Inanipa mashaka hata ulinzi wa viongozi hawa ambapo inawezekana Watanzania wasio wema wakaamua kuwauza ili waondoke mbele ya macho ya Watanzania wenye kuhitaji huduma zao.....