Mshiiri
JF-Expert Member
- Jun 16, 2008
- 2,012
- 507
Nimejaribu kutafuta sana maana nzima ya insurance na siipati kabisa. Sijawahi ona au kusikia jamii fulani hapa Tanzania au mtu fulani kapata kanufaika na bima hizi za mali. Labda tuwaulize ndugu zetu wanaounguliwa na ma-godown pengine wanajua means! Au pengine ni mimi sina elimu ya kutosha ya bima za mali na vyombo kama magari. Bima za afya na mifuko ya jamii kama NSSF ana PPF wao wako clear sana na utendaji wao na hii nawapa pongezi katika kukwamua Tanzania na lindi la umaskini. Kwa mdau anayejua kuhusu hizi insuarence za magari na mali anifahamishe au anijuze tafadhali. Kwa sababu mimi sioni why pay for insurance ambayo kulipana mpaka upigwe danadana na uishie kukata tamaa wakati polisi wanakubonyeza ulipe na kama umelipa katika ajali hawafanyi lolote na kama hujalipa moto utauona. Huu si wizi kweli? Watu wanapata ajali katika basi lakini huishia kusikojulikana wala hawa mabwana bima hawaonekani hata wakisema katika eneo la tukio. Hivi si wizi huu kweli?