Injinia Stella Manyanya alifunda jiji la Dar kiaina!

KIM KARDASH

JF-Expert Member
Sep 21, 2011
5,139
1,139
[h=3]MKUU WA MKOA WA RUKWA AZINDUA KAMPENI YA USAFI WA MAZINGIRA MJINI SUMBAWANGA LICHA YA MVUA KUBWA KUNYESHA JANA[/h]


Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya (katikati) akifagia kwenye moja ya barabara za Mji wa Sumbawanga Mkoani humo jana katika uzinduzi wa kampeni ya kusafisha Mji huo ijulikanayo kama "SUMBAWANGA NG'ARA 2012". Wanaojumuika naye kwenye usafi huo ni Mkuu wa Wilaya ya Sumbawanga Kanali John Antonyo Mzurikwao na Mkurugenzi wa Manispaa ya Sumbawanga Samwel Simwela. Mkuu huyo wa Mkoa ameanzisha Kampeni hiyo ambayo itakuwa ni ya kudumu baada ya kuona Manispaa hiyo imezorota katika usafi wa mazingira.

Katibu Tawala Mkoa wa Rukwa Alhaj Salum Mohammed Chima akijumuika na Mkuu wa Mkoa huo katika uzinduzi wa Kampeni hiyo.



Huku Mkuu wa Mkoa huo akiendelea na ufagiaji wa barabara za Mji huo wa Sumbawanga Daladala nazo zilikuwa zikiendelea na shughuli zake za kusafirisha abiria kupitia barabara hizo. Nyuma yake ni Mkuu wa Wilaya ya Sumbawanga Kanali John Antonyo Mzurikwao.

Mbunge wa jimbo la Sumbawanga Mjini Mhe. Aeshi Hillal akitoa uchafu kwenye mtaro katika moja ya barabara zilizopo katikati ya Mji wa Sumbawanga wakati wa uzinduzi wa kampeni hiyo jana. Kulia ni Katibu Tawala Mkoa wa Rukwa Salum Mohammed Chima na Mstahiki Meya wa Manispaa hiyo Sabas Katepa.

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mhe. Injinia Stella Manyanya akijumuika na wa wananchi pamoja na viongozi waandamizi wa Serikali katika ufagiaji wa barabara za Manispaa ya Sumbawanga.



Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya akifanya uhamasishaji wa usafi wa mazingira katika Mji wa Sumbawanga kwa abiria wa daladala jana kwenye uzinduzi wa kampeni ya "SUMBAWANGA NG'ARA 2012". Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Sumbawanga Kanali John Antonyo Mzurikwao na Mstahiki Meya wa Manispaa ya Sumbawanga Sabas Katepa.



DSC00990.jpg
Uhamasishaji huo ulifanyika kwa wananchi wote wakiwemo wapita njia.



Mkuu wa Mkoa wa Rukwa akitoa mchanga kwenye mtaro katika moja ya barabara zilizopo katikati ya Manispaa hiyo ya Sumbawanga huku Mvua ikiendelea kunyesha.



Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya (kulia) akifagia kwenye moja ya barabara za Mji wa Sumbawanga Mkoani humo jana katika uzinduzi wa kampeni ya kusafisha Mji huo ijulikanayo kama "SUMBAWANGA NG'ARA 2012". Kushoto ni Naibu Meya Manispaa ya Sumbawanga, Aurelia Kanyengele.


Waandishi wa habari nao walikuwepo kutaka kujua kilichomsukuma Mkuu wa Mkoa huo kuamua kuingia barabarani na kuanza kufagia, ambapo alisema Kiongozi bora ni lazma afanye kazi kwa vitendo na kuwa mfano bora kwa wale anaowaongoza.


Katibu wa Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Frank Maten akijumuika kwenye kampeni hiyo.


 
Hakuna kitu hapo! Usanii tu mbele ya waandishi wa habari, na makamera-man kibao! Hiyo barabara wanayosafisha haina uchafu wowote,sanasana wanaharibu kwa kuondoa layer' ya sub-base na kusababisha mashimo zaidi! Hizi ni politiki, angekuwa makini aende kwenye madampo na mitaani akasafishe.
 
Hakuna kitu hapo! Usanii tu mbele ya waandishi wa habari, na makamera-man kibao! Hiyo barabara wanayosafisha haina uchafu wowote,sanasana wanaharibu kwa kuondoa layer' ya sub-base na kusababisha mashimo zaidi! Hizi ni politiki, angekuwa makini aende kwenye madampo na mitaani akasafishe.

Lakini anaonyesha njia hata kagame alianza hivihivi kigali leo nchi nzima ni safi na kuna siku maalum jmosi nadhani ya usafi kwa nchi nzima...
 
huyu akiongea bungeni ni upupu tu.Hafai hata kuwa mjumbe wa nyumba kumi.
 
Watz huu upinzani wetu wa kisiasa sasa unatupeleka kubaya,yani huyu mama kweli anastahili kejeli kwa hili?sidhani.Mama amefanya jambo zuri,hivi hawa viongozi wetu walio wengi mnawajua mnawasikia,nani anaweza ku taka trouble ya kuingia kwenye mitaro ya maji huku mvua ikinyesha hata kama ni mbele ya camera,hiyo yao maarufu ya kupanda ka mti kamoja lazima watandikiwe mkeka wa kupigia magoti...viongozi wa jiji chafu la dar waichukue hii kama challenge..
 
injia manyanya amethubutu bwana nyie mfumo dume unawasumbua angefanya mnyika,magufuli au maalim seif kusingekua na tabu,mi naona tatizo hapa ni huu uanamke wake!kwani mnavyosikia kwa kaka zenu kwamba sokoine alikua mchapa kazi mnadahni alilima mashamba yote yeye mwenyewe kwa mkono wake tanzania nzima?alikua anaonyesha njia na mfano kama hivi then hii inasambaa mpaka vijijini!
 
Wengine tutatoa credit si kwa manyanya.mnafiki tu na anajipendekeza kwa pinda aliyempigia debe.

Mama ukiongea mimi nakuelewa sana kwa sababu lazima utakuwa unamjua kwa undani tu na kuwa kafikaje fikaje hapo alipo ..
 
Huyu mama amesaidia vipi katika profession yake kwani huyu mama alikuwa kwenye shilika la Megawatt kabla hajaikimbia profession yake, ningempa credit kama angeenda kusaidia mafundi umeme kufanya connection kwenye nyumba zao, kufagia kila mtu anaweza kufanya hivyo na angeweza hata kuajili watu wangefanya kazi hiyo, sasa fuatilia ni kiasi gani cha fedha kimetumika kwenye tukio la huyo Engineer kufagia.
 
Back
Top Bottom