Ingekuwaje wangekuwa Wachagga?

Status
Not open for further replies.
...bachoji bah mhilya duhu angoh?! .....amboh bamanile tulenah-'masekeni (segeni), maalmasi, madhahabu, mang'ombe, mhulu (mhuru genge), sungwi, masondwa, mabele, ngubo, mahama, ng'ong'osela, maliboto, manumbu, bubele, lunyenya, madoke, nembe, mashe, sato, nguryati, linyanza, maliwa, maguha, makubi (nzubo, lunani, matembele, mashiri, manyang'wanga, ndulu, lugaka), noni (jiiji, hungwe, dodorima, jolowe, topunda, n'helegani...), etc, etc..... maaayne - just luv it!!! :) :) :D

SteveD,
Hiki ni Kisukuma? Mbona nimetoka nje kwa asilimia kubwa? Au ndiyo Kinyantunzu (Bariadi) maana hicho hata Wasukuma (Mwanza) hulalamika kuwa hawaoni kitu. Ila mbona mnaandika na matusi? Duhu si ni Uchi ..:)
Du, hiso kwenye RED sijala siku nyingi sana Agrrrrrr!!!!!
Ila kwenye ndege, nimemkumbuka mdogo wangu ambaye marehemu dada yangu ilibidi aanze kumwita TITI. Bwana mdogo alivyoletwa Dar kutoka shamba akawa siku nzima anaimba "titiii wa Mpotyapotya, kwikala mkalambo lufindo ftetete mtweeee pono..." Hiki kindege hupiga makelele sana titiiii!!!
NB: What is Maliwa? Nguryati? Au una maana ya matikiti?
 
Sidhani kama ni sahihi kusema kuwa Wanyamwezi/wasukuma hawakusoma mapema.
Kumbuka kuwa kashkashi za za kumpindua Nyerere miaka hizoo, zilianzia na Wanyamwezi. Hawa walianza kumletea sana shida na akawarudi si kawaida. Akina Kasanga Tumbo, Mtemi Lugusha, Mtemi Fundikira. Fundikira aliishia mitini Kenya na hawa wakapata house arest. Mtemi Lugusha nakumbuka alikuwa hawezi kwenda sehemu yoyote penye watu wengi bila ya kutoa taarifa kituo cha Polisi cha sikonge.

Kuna jamaa mmoja kaandika huko nyuma kuwa Nyerere alikutana na Wachaga UN wakidai ardhi yao. Ninavyofahamu ni kuwa walikuwa Wahaya na Nyerere akawaambia kuwa yeye kaja kudai Tanzania nzima.
 
Nadhani imefika wakati, tuachane na fikra finyu za kikabila na udini. Haitusaidii chochote kila kukicha tunalalamikia, kwa mfano kama huu, wasukuma wengi, wachagga wachache au wakristo wengi, waislamu wachache na wanawake wengi, wanaume wachache au wazee wengi, vijana wachache.

Midhali mtu ni mtanzania na uwezo wa kufanikisha kazi aliyopewa anao, basi asinyimwe wadhifa kwa sababu ya umri wake, jinsia yake, kabila lake au dini yake. Yeyote mwenye uwezo atuongoze, atuondolee kero na kutuletea maendeleo tunayoyahitaji kwa wakati huu tulionao na kwa faida ya vizazi vijavyo.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom