Ingekuwaje kama ningekuwa mwanamke?

EJM_

JF-Expert Member
Jul 8, 2011
3,836
2,090
Nimekuwa nawaza sana mpaka kuna wakati naogopa, hivi ingekuwaje kama ningekuwa mwanamke?

  • Kila nikipita napigiwa miluzi na ksiiiiiii.............
  • Kila mwezi nakuwa na wasiwasi wa lini itatokea (period)
  • Kila mwezi najua ntaugua (kwa walio wengi tumbo, mgongo au kiuno)
  • Kuogopa mimba ukiwa bado shuleni
  • kujifungua kwa uchungu
  • kupkea kichapo kwa mume
  • huwezi kutembea peke yako usiku bila escort ya mwanaume hata kama ni mdogo kwako
  • na mengine mengi...........

Dah mpaka huwa naogopa, what if i was a woman?
 
Hua unatuthamini wanawake au hizi ni porojo tu? kama wajiuliza yoote hayo ina maana wajua mateso yetu.
 
NInamjua dk anaweza kukubadilisha jinsia. Kama uko tayari sema then utakuja kutupa mauzoefu hapa
 
Ingekuwa kawaida tu km tulivo sisi, Sema kwa vile u mwanaume kwa sasa ndio maana, Otherwise we are happy na tunajivunia kwa namna Mungu alivotuumba!

Am happy to be a woman!!!!
 
Hua unatuthamini wanawake au hizi ni porojo tu? kama wajiuliza yoote hayo ina maana wajua mateso yetu.
Sidhani kama ni mateso being a woman mamy but mi najiuliza tu ni namna gani ningeweza ku kop na hali halisi.......m very carelesss na women need to be extra careful
 
Hapo bado hujazungumzia nanihii....
ila ungezoea tu..
Hivi mashoga wako kundi lipi la kijinsia?
 
Sidhani kama ni mateso being a woman mamy but mi najiuliza tu ni namna gani ningeweza ku kop na hali halisi.......m very carelesss na women need to be extra careful

sijasema mateso kua mwanamke, nimesema kuna mateso tunapata, see the difference?
 
Sana tu..

Mkuu wewe hujawahi kupigwa kibuti kwa sababu ya ukachala?
Muda wote unawaza kumridhisha, ukishindwa tu, unasaidiwa?
Unatafuta pesa kwa jasho na damu ili uweze ung'oe demu mkali?
Unaingia kwenye ushindani yeye ndiye aamue amkubalie yupi?
wanaume tuna changamoto kuliko wanawake Bhana..
 
Hahahahaaa we umeona hapo tu kwenye kumuacha mwanamke aaqmue kama anakutaka wewe ama la eeh!
 
1.Ungetongozwa mpaka uchukie mwenyewe, 2.ungeolewa na kuzaa(kuzaa ni process kumbuka)watoto,
3. Ungekuwa na maringo ujanani mwako.
Mengi tu mkuu ungekuwa nayo,
 
ingekua kawaida tu, na hapo pengine ungejiuliza nngekua m'me ingekuaje kwa kuangalia disadvantages.
Kila kitu kina ubora wake, kutokana na M/mungu mwenyewe alivokijaalia.
 
Back
Top Bottom