Ingekuwa wewe ndo kikwete...ungetoa tamko gani??

sijui nini

JF-Expert Member
Sep 29, 2010
2,553
1,285
Najaribu kujiuliza tu, kulingana na mwenendo mzima wa kiasa ulivyo sasa hivi na upepo unavyovuma..mpaka sasa raisi wetu yuko kimya kabisa hasa katika jambo hili muhimu sana la msukumo wa kujiuzulu kwa viongozi muhimu sana wa nchi...hivi kwa mtazamo wako (bila kujali itikadi za ki chama) ungetoa tamko gani au ungechukua uamuzi gani!?

Nawasilisha!
 
Ningeuda serikali ya Mseto ili kila upande uchangie kutatua matatizo yaliyopo. Wewe Je?
 
Akifukuza wote atatoa wapi wengine - au ateue kutoka nchi za nje huko anakolala na kushinda kila siku?

Wapo wengi sana capable to be Minister, wengi, with all credibility, ability, loyal to Tzs na wachapa kazi...
 
Ningejiuzuru mara moja, maana yote haya ni dalili ya wazi kwamba serikali yangu imeshindwa kuongoza.
 
its funny nikikumbuka huyu aliwahi kuitwa
'Rais kijana'....wakati ki maamuzi huyu ndo 'Rais mzee' kuliko wote
katika historia ya nchi yetu
 
Wapo wengi sana capable to be Minister, wengi, with all credibility, ability, loyal to Tzs na wachapa kazi...

Unawaona wewe kwa sababu umetulia nchini kwako, mtalii atawaona lini? akirudi ikuru anaanza kuangalia movie za kanumba na bongo flavour music,
Usishangae akimteua AY an Lady JD kuwa mawaziri.
 
Unawaona wewe kwa sababu umetulia nchini kwako, mtalii atawaona lini? akirudi ikuru anaanza kuangalia movie za kanumba na bongo flavour music,
Usishangae akimteua AY an Lady JD kuwa mawaziri.
au aunde kamati....lol!!
 
Nawafukuza kazi waziri mkuu maana hawajibiki ipasavyo, mawaziri wote waliotajwa kuwa vinara wa kufuja mali ya Watanzania, makatibu wakuu wao na watendaji wakuu wote kwenye wizara hizo na kutengua uteuzi wao kuanzia leo maana wengine hawajadhitishwa tangu wateuliwe, naunda tume maalumu ya kujiridhisha kwa wafanyakazi wote wa wizara husika na kwa kila mfanyakazi alivyohusika anachukuliwa hatua ya kusimamishwa kazi ili apishe uchunguzi na ikidhibitika tu ni kwenga lupango na kufirisiwa mali yake yote na kutopata ajira serikalini kamwe yeye binafsi na vizazi vyao vyote ili liwe fundisho kwa watu wenye tabia na ujinga kama huo.
 
Ningewafukuza kazi mawaziri wote waliohusishwa na wizi, kufuatilia kwa kina nani wameiba hizo pesa na anaishi wapi, timua kazi na kisha kuwawajibisha kwanza kwa kuwafilisi, pili kuwafunga kama wahujumu uchumi. Period. Baaaye ningeteua mawazi hata 4 kutoka vyama pinzani ili wanisaidie kumalizia muda wangu.
 
embu vuta picha saiz kwa jinsi unamvyomfaham JK kwa sasa anaweza kuwa kwenye hali gani...anawaza nini...au anafanya nini hivi!!?...vuta picha tu!

Yuko kawaida - si ubongo wa zamani? Vuta picha watu wa kale wanawaza nini wakati cc tunapokuwa tuna-access information kwa internet. UMENIPATA
 
Kupitia kikao cha wazee wa Dodoma ningetamka yafuatayo:

NDUGU WANANCHI,

NIMEAMINI SASA HASIRA ZA MUNGU ZIMEZIDI KUWA KALI JUU YANGU.

NASEMA HIVI KWAKUWA MUELEKEO WA SERIKALI YANGU NI WA KUSUA SUA, NINYI WENYEWE NI MASHAHIDI.

KILA KITU, KILA SEKTA INARUDI NYUMA BADALA YA KUSONGA MBELE. MIKIKI MIKIKI YA KUTISHA. HII INANIFANYA

NIAMINI KILE KITENDO CHA KUIIBA KURA NA KUBADILI MATOKEO YA URAIS KIMEMCHUKIZA MWENYEZI MUNGU.

HAWA MAWAZIRI HAWANA KOSA HATA KIDOGO, BALI NI HASIRA YA MWENYEZI MUNGU TU; NAJUA KABISA ITAKUWA YENYEWE.

HIVYO BASI NIMEAMUA KUJIUZULU NA KUPISHA CHAGUZI NYIGINE KWA MANUFAA YA TAIFA LETU.

AHSANTENI.
 
Ningewataka wachukue uamuzi wenyewe kabla hata sijafika Dar...ndipo sasa tujadili cha kuwafanyia wale wote waliochukua mipesa hii ikiwa ni pamoja na kuwafilisi
 
Back
Top Bottom