WomanOfSubstance
JF-Expert Member
- May 30, 2008
- 5,457
- 956
Kumekuwepo na majadiliano ya kutosha sana humu jamvini kuhusu matatizo ya wanawake na waume au wapenzi wao - Kutelekezwa, kuletewa nyumba ndogo,kuachiwa mzigo wa kulea familia, kutumiwa n.k.Pia tumejadili kuhusu kwanini wanaume hawapendi ushirika kwenye mapenzi.
Tunajua kabisa kuwa tamaduni, mila, desturi, dini vyote vinaamrisha wanandoa kuheshimu ndoa zao.Pamoja na hayo ukweli unabakia kuwa wanandoa hutetereka katika kuheshimu viapo vyao.Msisitizo zaidi uko katika kuwataka wanawake wajiheshimu na inashangaza kuwa msisitizo hauko zaidi katika kuwabana wanaume.Kutokana na hili, wanaume nao wamekuwa wakilega zaidi katika kuheshimu ndoa au mahusiano yao.
Matokeo yake ni kuwa watu wamekuwa wakifumbia macho suala zima la kutoka nje ya ndoa.Hakuna mwanamke anakubali kuwa wanawake nao wanatetereka , na hata wanaume nao wanajidanganya kuwa wapenzi wao au hata wake zao hawatoki nje ya ndoa.Ila hapohapo tunasikia ati vipimo vya DNA vimethibisha kuwa idadi kubwa ya watoto waliozaliwa na wazazi waliokuwa na mabishano kuhusu nani baba wa mtoto - wameonekana siyo wa akina baba hao walengwa.
Je, Mwanaume anayetoka nje ya ndoa na mke wa mtu au mpenzi wa mtu mwingine anajisikia vipi pale mkewe akichukuliwa na mwanaume mwingine?

Last edited: