Inawezekanaje Kambi ya Jeshi ya Chita jirani na Kihansi haina umeme?

Jadi

JF-Expert Member
Aug 2, 2011
1,494
860
Jamani wanajamii forum,na wale wahusika wa Nishati na Madini,naomba nichochee wakazi wa Chita wagomee sherehe za miaka 50 ya uhuru kwa ukatili wanaofanyiwa na TANESCO kunyimwa umeme,wanaishia kuona nguzo tu zinazopeleka umeme Kidatu. Shame on you TANESCO na yeyote ambaye alitakiwa afatilie suala hili na amekaa kimya.

Jeshi letu lazima liheshimiwe,wanafanya kazi nzuri ya kutulinda na wanastahili huduma za kijamii kama umeme. Ukipita kambini utaona nyaya za jenereta ambayo huwaka masaa machache na si kwa watu wote. Inasikitisha sana
 
ulitaka wapata ili iweje kama tatizo ni la kitaifa? waache na wao waonje uchungu wa kukosa umeme. huo ndio uzalendo sio kama wabunge wanajiongezea posho wakati nyongeza ya maslahi ni tatizo la la kitaifa.
 
usikurupuke tafuta sababu ya kukosekana umeme eneo hilo hata kama umeme unapita hapo. Ni wananchi wangapi nchi hii nikiwemo mimi umeme umepita kwangu lakini sina kwa sababu natakiwa kulipa service chaji sh. 460,000/- na nguzo moja sh. 1,100,000/=
 
unaweza kukuta jeshi halijalipa connection charge na vivyo hivyo wananchi wa hapo? kwani hujasikia siku hizi jeshi kukatiwa umeme na Tanesco? hata kama ni jeshi wanatakiwa kufuata taratibu sio amri za jeshi kupewa umeme eboooooooooooo
 
Jamani wanajamii forum,na wale wahusika wa Nishati na Madini,naomba nichochee wakazi wa Chita wagomee sherehe za miaka 50 ya uhuru kwa ukatili wanaofanyiwa na TANESCO kunyimwa umeme,wanaishia kuona nguzo tu zinazopeleka umeme Kidatu. Shame on you TANESCO na yeyote ambaye alitakiwa afatilie suala hili na amekaa kimya.

Jeshi letu lazima liheshimiwe,wanafanya kazi nzuri ya kutulinda na wanastahili huduma za kijamii kama umeme. Ukipita kambini utaona nyaya za jenereta ambayo huwaka masaa machache na si kwa watu wote. Inasikitisha sana

Mkuu unataka kuchochea jeshi wasipige kwata? Tumuulize Kamanda Regia kwa nini hawana umeme manake najua anatoka maeneo hayo
 
Back
Top Bottom