Inawezekana

kande kavu

JF-Expert Member
Sep 17, 2011
234
86
Kumbe inawezekana Waungwana.

Mpaka miaka miwili iliyopita nilikuwa Fataki hasa. Namaanisha niliwabinua kweli kweli wa kila sampuli. Ilikuwa ni kama laana fulani kwani kila nilipomuona wa kike akili yangu ilirukia kwenye kumbinua.Hata kabinti kamoja kazini kalikaribia kabisa kuvunja ndoa yangu.Na hapo ndo nilipojua wamama wanaweza kuua kwa mapenzi, maana wife ghafla akawa si yeye tena.Hata hivyo niliendelea "kutengeneza CV" kwenye fani.

Ikaja wakati nikaanza kutafakari hasa ninachokipata kwenye hilo game.Nimetafuta mpaka kwenye uvungu lakini sikupata nilichopata kwa kuwekeza kwenye ngono. NIKAAMUA HIVI HIVI kuacha.Na NIMEACHA.Hivi naandika niko lunch time na kuna kabinti kako hapa kazuri kwa viwango vya nje.Naamini nimeishinda hiyo dhambi, kwani ingekuwa enzi zangu mpaka nywele za kwapa zingenisimama kwa mikakati ya kumbinua huyo mdada.Kwa hivi sasa wala, kwani hata meza nimebadili na nimemepa mgongo asinitege.

Sijaacha uzinzi kwa sababu za kiafya wala kiuchumi na nashukuru MUNGU nimetoka na afya yangu safi kwenye hilo balaa. Hayo maeneo niko poa.Je wewe unayesoma hapa,je unafanya uzinzi? kwa sababu gani hasa? Je ni kwa sababu umeambiwa ni kawaida ya mwanaume? Je ni kwa vile unaona haiwezekani kuacha? Hebu fikiri hizo gharama za "uwezeshaji wa uzinzi" zingefaa vipi maeneo mengine bora kwenye maisha yako!

INAWEZEKANA KUACHA UZINZI.ACHANA NA ILE SAUTI YA PILI KCHWANI MWAKO.

Nimetimiza wajibu.
 
awesome jaman.... well done mkuu.
ni vema kuvishinda vishawishi.
mmh hongera tena mkuu.
 
Mke alikuwa anajidai ana mume mzuri! Dah! Nway, hongera kwa kuacha uzinzi.
 
Hongera sana, sasa wewe kaa pembeni wachia mafataki wengine wakusaidie.
 
Kumbe inawezekana Waungwana.

Mpaka miaka miwili iliyopita nilikuwa Fataki hasa. Namaanisha niliwabinua kweli kweli wa kila sampuli. Ilikuwa ni kama laana fulani kwani kila nilipomuona wa kike akili yangu ilirukia kwenye kumbinua.Hata kabinti kamoja kazini kalikaribia kabisa kuvunja ndoa yangu.Na hapo ndo nilipojua wamama wanaweza kuua kwa mapenzi, maana wife ghafla akawa si yeye tena.Hata hivyo niliendelea "kutengeneza CV" kwenye fani.

Ikaja wakati nikaanza kutafakari hasa ninachokipata kwenye hilo game.Nimetafuta mpaka kwenye uvungu lakini sikupata nilichopata kwa kuwekeza kwenye ngono. NIKAAMUA HIVI HIVI kuacha.Na NIMEACHA.Hivi naandika niko lunch time na kuna kabinti kako hapa kazuri kwa viwango vya nje.Naamini nimeishinda hiyo dhambi, kwani ingekuwa enzi zangu mpaka nywele za kwapa zingenisimama kwa mikakati ya kumbinua huyo mdada.Kwa hivi sasa wala, kwani hata meza nimebadili na nimemepa mgongo asinitege.

Sijaacha uzinzi kwa sababu za kiafya wala kiuchumi na nashukuru MUNGU nimetoka na afya yangu safi kwenye hilo balaa. Hayo maeneo niko poa.Je wewe unayesoma hapa,je unafanya uzinzi? kwa sababu gani hasa? Je ni kwa sababu umeambiwa ni kawaida ya mwanaume? Je ni kwa vile unaona haiwezekani kuacha? Hebu fikiri hizo gharama za "uwezeshaji wa uzinzi" zingefaa vipi maeneo mengine bora kwenye maisha yako!

INAWEZEKANA KUACHA UZINZI.ACHANA NA ILE SAUTI YA PILI KCHWANI MWAKO.

Nimetimiza wajibu.

1. Sirajarii kuacha hivi karibuni mpk nimpe mkeo nafasi ya kukulipizia kisasi kwa yale uliyomfanyia
2. Nikuombe unyoe nywele za kwapa
3. Nikupongeze kwa uamuzi wa busara wa kutoa nafasi kwa wengine, Ubarikiwe sana Mtumishi
 
Beware
Any addiction kuna relapse
But namtakia mafanikio
1. Sirajarii kuacha hivi karibuni mpk nimpe mkeo nafasi ya kukulipizia kisasi kwa yale uliyomfanyia
2. Nikuombe unyoe nywele za kwapa
3. Nikupongeze kwa uamuzi wa busara wa kutoa nafasi kwa wengine, Ubarikiwe sana Mtumishi
 
Jasiri haachi asili.
Wewe upo likizo unakusanya nguvu kurudi kazini kwa kishindo.
Maoumziko mema mkuu
OTIS
 
congrats! Ni maamuzi ya busara hayo. Endelea kuomba mungu akuepushe na vishawishi. Halafu zidisha mapenzi kwa wife.
 
Mshukuru Mungu kwa kukuepushia hilo roho ya uzinzi!!!
Na usitende tena hiyo dhambi ya uzinzi, u
we mwalimu na kioo safi katika jamiii!
 
Mke alikuwa anajidai ana mume mzuri! Dah! Nway, hongera kwa kuacha uzinzi.

Ndio maana aliposhtukia alitaka kuua mtu. Na uAsha ngedere alioufanya pale shambani kwangu haukuwa wa kitoto lakini mzee niliendelea kupiga game.Any way, that is gone, but from her eyes, she does not trust me anymore.And that is for me to live with.
 
Inawezekana, lakini kulingana na maelezo yako kwamba umekapa mgogo ili kasikutege, hapo nina wasiwasi, Hujaacha ila unapumzika. maana ungekuwa umeacha usingekuwa na wasi wasi wa kutegwa ungekaona kama mwanaume mwenzio.
 
1. Sirajarii kuacha hivi karibuni mpk nimpe mkeo nafasi ya kukulipizia kisasi kwa yale uliyomfanyia
2. Nikuombe unyoe nywele za kwapa
3. Nikupongeze kwa uamuzi wa busara wa kutoa nafasi kwa wengine, Ubarikiwe sana Mtumishi

1.Kila kitu kina matokeo yake, nimepoteza kuaminiwa naye hata kama napendwa.Lakini pia uzinzi sio kisasi ni tabia.Kama hana mpango wa kunisaliti, hutompata kamwe.
2.Jifunze lugha na mnyumbuliko wake.
3.Bila shaka umetumia mtumishi ukimaanisha labda mi ni mlokole.Umenoa. Mimi sio mlokole na kuacha kwangu habari hiyo hakuhusiani kabisa na ile amri maarufu, amri ya sita. Sio mpaka watu wakufuate na vitabu vya ibada ndo ufikirie kwa makini. Huenda ukapotea.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom