TUJITEGEMEE
JF-Expert Member
- Nov 6, 2010
- 23,914
- 23,077
Kutambua hilo fanya jaribio hili... Hatua:Mkuu kwa hyo penseli ni ant gravity!!?
1.chukua karatasi moja nyeupe ya A4 ibandike kwenye dari, kwa kutumia gundi,ukiwa umesimama sakafuni au umenda ngazi kukitokea sakafuni.
2.Chonga penseli yako vizuri, ijaribu kwenye karatasi kama inaandika vizuri; ukijilizishakuwa inaandika vizuri iweke pembeni. pia chukua kalamu ya wino ijaribu kwenye karatasi uliyojaribia penseli kuona kama inaandika vizuri. Ukiridhika kuwa inaandika sawa sawa iweke pembeni pia.
3. Chukua kalamu zote mbili (penseli na kalamu ya wino) zigeuze kwa sehemu ya kuandikia zitazame juu. Ziache katika hali hiyo kwa muda wa dakika kumi.
4. baada ya dakika kumi, zikiwa bado zimegeuza kama maelezo ya hatua ya nne yalivyo zifunge kwa pamoja kiasi kwamba itakuwa rahisi kuzitumia kuchora mistari kwenye ile karatasi uliyobandika juu darini kwenye hatua ya kwanza. Jiridhishe kuwa umezifunga vizuri na wala hazita hachana wakati wa kuchora mistari.
5. Chukua kalamu hizo (zilizofungwa pamoja) wakati sehemu ya kuandikia ya kalamu hizo ikiwa juu, kuchora mistari nane kutoka ukingo mmoja wa karatasi hiyo kulekea mwingine kwenye karatasi iliyopachikwa darini. Wakati unachora angalia. Ukimaliza, angalia ni kalamu ipi itakuwa imeweza kuchora mistari mingi kuliko nyingine. Jibu utakalopata, litakupa ufahamu wa kujua kuwa penseli ni anti-gravity ama la...!
=====