Inawezekana matatizo ya nchi ni makubwa kuliko tunavyodhani: Immanuel Didas, apasuliwa kichwa badala ya mguu MOI

On the question of Muhimbili Orthopaedic Institute (MOI), I personally know a lot more than I should say here. I know the INSIDE story. Anyone wants details, send me PM.

What I can say is the following:

a) What happened is a consequence of mismanagement of MOI by the current administration. Emphasis on the word 'current'. A lot of hanky-panky stuff is going on there, but neither the Ministry or the President's Office has the guts to do anything about it.

b) MOI was 'taken' from the Swiss founders of the Institute before the previously agreed-to date. As a result, there was no management mechanism in place when this unofficial handing over took place.

c) What happened is tantamount to 'criminal negligence', but we Tanzanians have a culture of silence. We always 'leave things to God' even when we know we should demand compensation. Do the families of the victims of this criminal negligence and medical malpractice have the will to pursue legal action against the doctors, who negligently operated their beloved ones?

I rest my case!


Thank you MwanaHaki

As always, it's Political Decisions that mess things up....
 
Siku moja nilienda muhimbili kuangalia mgonjwa, nilichokiona ilinifanya nirudi siku ya pili safari hii sio kuangalia mgonjwa ila kuthibitisha nilicho kiona.

Kwa nilichokiona hilo lililotokea linawezekana na litatokea lingine.

Wodi ilikuwa imejaa wagonjwa pomoni, acha waliolala vitandani, waliowekewa magodoro uvunguni wa vitanda bila kusahau waliolala kwenye njia huku ndugu zao wakishikia dripu kwa sababu viwekea dripu hamna. Hii haikuwa ajali ila ni wodi ya watu kulazwa kwa kuandikiwa na daktari.

Wakati wagonjwa wakiwa wamelala hivi, bado kulikuwa na nesi anahudumia mgojwa kwenye kona walipopata walau kanafasi cha kumpa mgonjwa dawa.

Nina rafiki yangu daktari nilikuwa namlaumu sana kwa nini hatukutani bar, lakini kwa nilichokiona siku ile na siku niliyofuata nilichokabaki nacho nikuwaonea huruma madaktari na manesi kwa kazi waliyokuwa nayo, nakumshukuru Mungu kwa afya niliyokuwa nayo kila asubuhi.

Ndugu zangu pamoja na maneno yenu makali dhidi ya madaktari hao. Mimi kwa mtazamo wangu nilichokiona siku ile naamini watu wenye mapenzi mema na wanadamu hawajui au wanafichwa au wamefumba macho. Matatizo yetu ni mengi lakini watatuaji wa matatizo haya sio shetani wala serikali, bali ni mtu mmoja na yeye ni wewe na mimi.

Nilitamani nipige picha hali iliyokuwepo pale wodini lakini sikufanya hivyo, kwa sababu mtu yeyeto angekataa kuwa pale ni wodini, wengi wetu mngesema ni sokoni tena kariakoo shimoni na wala sio wodini.

Hakuna raha ya kwenda kuangalia wagonjwa halafu wote wanakuangalia kwa macho ya kukata tamaa kwamba umeshindwa kuwasaidia na wewe ndio chanzo cha mazila hayo yote. Wanasubiri lini wataondoka hapa duniani.

Nasikitika mgonjwa niliyekwenda kumuaangalia siku ya tatu yake akafariki lakini sikushangaa maana wagonjwa wote uliokuwa unawaangalia usoni walikuwa wamekata tamaa na mazingira yalikuwa hata kama sugu kiasi gani lazima utakata tamaa.

Uko Ulaya mliko hamna wagonjwa nyomi wodini, ndugu zenu huku tunawekewa godoro chini ya uvungu wa mgonjwa mwenzio, uliyelala kwenye vinjia vinavyotebganisha vitanda nduguyo anakushikia dripu yako. Kulala kwetu ni shida hapa Muhimbili hapatoshi na bado tunaletwa wengine toka Mkotokuyana, Namapwia, Mferejini, Narung'ombe, Kwedikwazu, Muheza, na hata Litembo tuje kuonana na madaktari bingwa hapa Muhimbili wakati tumewaacha waganga wetu wa jadi huko tulikotoka. Hamjui kama Muhimbili kumejaa? Na bila hiyana ukiletwa unalazwa wodini unatafutiwa sehemu ambayo wagonjwa watasogezwasogezwa na wewe ulale ukisubiri majaliwa ya Mungu.

Wana JF wote mlioko Dar nendeni mkatembelee wagonjwa pale MUhimbili uone kama hautapasuliwa kichwa badala ya mguu na mguu badala ya kichwa.

Walioko ulaya ukiumwa usijaribu kutiwa huku. Ukumbuki waziri wetu tulikuwa tunampelekea bacteria mpaka anafika South Africa vindinda vishaoza.

Kwa herini naenda kuangalia wagonjwa Muhimbili. Machozi ninayo lakini hata nikilia itasaidia nini?
 
Jamani kwa wenzetu ulaya au marekani hilo ni dili kubwa sana.. mtu anatakiwa alipwe hadi afe kwani kama huyo aliyefanyiwa operation ya kichwa ni kwamba amepewa kilema cha maisha kichwani mwake... JF hakuna mwanasheria? hilo mtu akipanda nalo mahakamani atakuwa ameokoa maisha ya watu wengi sana na pia watakoma
 
Mzee Mwanakijiji kiambatanisho ulichokiweka hapo ni really healpful lakini tatizo kubwa tulilonalo ni luck of patient involvement kwenye process nzima ya matibabu, especially kwenye hospitali za serikali.Kuna rumours nimewahi kuzisikia kwamba kuna madaktari ukiingia kuwaona wala hawakuulizi unachoumwa, wanakuangalia tu na kukuandikia dawa, na wale wenye tabia ya kuongea na wagonjwa wengi watakuuliza swali moja tu- nikusaidie nini?, au una tatizo gani? etc. baada ya majibu ya swali hilo- of course utaambiwa unachoumwa (sometimes huambiwi!!) lakini its very rare kwa mgonjwa kuambiwa namna atakavyotibiwa ugonjwa wake. In most cases communication kati ya daktari na mgonjwa kwenye mahospitali mengi ya serekali ni one way traffic, mgonjwa anajibu maswali tu, hapewi nafasi ya kutoa maoni yake au kufanya choice kama kuna more than one alternative. Kwa maana hii basi haka kapengere ka "MAKE SURE THER IS AN AGREEMENT BTN YOU AND YOUR HEALTH CARE TEAM ABOUT THE EXACT TYPE OF PROCEDURE YOU WILL BE UNDERGOING" hakapo huko kwenye mahospitali yetu wachovu, its purely on the basis of -what you see is what you get- take it or leave!
Sidhani kama identification bracelets zimeanza kutumika kwenye hospitali zetu za serekali, kama zingekwepo chance ya matatizo kama haya kutokea ingepungua.Naamini this is just a mix up- mtu ameingizwa theatre na wrong file, mind you hakuna picha ya mgonjwa kwenye hilo file so hata kama wangekua watu mia kwenye hiyo operating team wasingeweza kushtukia kosa.Kuna kapengere kenngine hapo kanasema "MAKE SURE SOMEBODY ASK YOU YOUR NAME...."- Sidhani kama wagonjwa wanapewa nafasi ya kupanga yale wanayoyaona yanafaa kwa maslahi yao, ukiingia theatre kazi ni moja tu.
Mimi nina personal experience ambayo labda nikiizungumzia hapa itasaidia kama wahusika wananisoma. Mwaka huu mwezi wa nne niling'olewa my 2 wisdom teeth under general anaethetic, lakini prior to siku yenyewe ya operation nilienda hospital kama mara mbili kwanza for tests and consultations only, hadi siku yenyewe imefika wahusika walikua wananitambua kwa jina na sura.
 
Source: http://www.freemedia.co.tz/daima/2007/11/8/habari2.php

Madaktari wasimamishwa kazi
Aliyepasuliwa kichwa MOI bado hajaamka

na Lucy Ngowi
HALI ya mgonjwa aliyefanyiwa upasuaji wa kichwa kwa makosa katika Taasisi ya Mifupa Muhimbili (MOI), bado hajapata fahamu, Tanzania Daima imefahamishwa.
Habari za uhakika kutoka MOI zinaeleza kwamba, hali ya mgonjwa huyo ambaye kimsingi alikuwa akipaswa kufanyiwa upasuaji wa goti, bado inaendelea kubakia kuwa ni ya shaka, leo ikiwa ni siku ya nane tangu afikwe na balaa hilo.

Mgonjwa huyo, Emmanuel Didas, alifanyiwa upasuaji huo wa kichwa Novemba mosi, wakati akijiandaa kupasuliwa mguu ambao ndiyo ulikuwa ukimsumbua.

Badala yake wakati Didas akifanyiwa upasuaji huo, mgonjwa mwingine Emmanuel Mgaya ambaye ndiye aliyekuwa na matatizo ya kichwa hata kutakiwa kufanyiwa upasuaji huo, aliishia kupasuliwa mguu.

Hali hiyo imesababisha baadhi ya wagonjwa wanaosubiri huduma ya upasuaji katika taasisi hiyo kuingiwa hofu kubwa kuhusu umakini wa baadhi ya madaktari katika hospitali hiyo.

Tukio hilo la kwanza la aina yake, limesababisha Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Profesa David Mwakyusa ambaye kitaaluma ni daktari, alazimike kutangaza kusimamishwa kazi kwa madaktari wanaohusishwa na matukio hayo mawili.

Wakati taifa likisubiri matokeo ya tume iliyoundwa kuchunguza matukio hayo, Wizara ya Afya mwanzoni mwa wiki hii iliitaka kukamilisha kazi hiyo haraka ili serikali na wananchi waweze kujua, pamoja na kuchukua hatua zinazostahili iwapo itabainika kuwa kulikuwa na uzembe.

Mganga Mkuu wa Serikali, ambaye pia ni Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Dk. Deo Mtasiwa, aliliambia gazeti hili mwanzoni mwa wiki hii kuwa, tume hiyo iliyoundwa na MOI ilikuwa imeshaanza kazi ili kubaini kiini cha tatizo lililojitokeza, na mara baada ya uchunguzi huo kukamilika, wizara itayaweka matokeo hayo bayana.

Ingawa Dk. Mtasiwa alisema tatizo lililojitokeza ni ajali kama ajali nyingine zinazotokea, alieleza pia kuwa, katika mazingira kama hayo, ni bora kujua tatizo hilo limesababishwa na nini, ili wizara iweze kuchukua hatua.

"Hii ni accident (ajali) ambayo si ya kawaida. Bodi na Utawala wa MOI inachunguza, na baada ya hapo kuna Baraza la Madaktari, ndipo tutaona na sisi tunafanyaje. Tunataka kujua kama ni system (mfumo) ilikorofisha au ni uzembe ulifanyika," alisema Dk. Mtasiwa.

Pia aliwataka wananchi kutumia taasisi hiyo bila woga wala wasiwasi kwa kuwa suala hilo linachunguzwa kwa undani. Aliongeza kuwa, uongozi wa MOI umeihakikishia wizara hiyo kuwa 'system' zote za kufanyia upasuaji zimechunguzwa na hazina tatizo.

Hata hivyo, Tanzania Daima kupitia vyanzo vyake mbalimbali vya habari hospitalini hapo, ilibaini kuwa, upasuaji huo ulifanywa na madaktari wawili (majina tunayahifadhi), mmoja mwanamke na mwingine mwanaume.

Chanzo kimojawapo kilidai kuwa, daktari mwanaume ambaye alisoma nchini Japan, ni mgeni katika fani hiyo, pia hakusomea mambo hayo na pia hana uzoefu, hivyo alitakiwa ajifunze chini ya wenzake wenye uzoefu.

"Kwa daktari aliyesomea, alitakiwa ajue kitu anachokifanya, kama ubongo umeathirika au la. Kitu kinachoshangaza daktari huyo alikata kinyama kidogo kichwani ili akifanyie uchunguzi, lakini kwa aliyesomea alitakiwa ajue kuwa ubongo ule haujaathirika kwa ugonjwa," kilisema chanzo hicho.

Kwa maelezo ya chanzo hicho, baada ya mgonjwa huyo kufanyiwa upasuaji wa kichwa wakati akiwa mzima, hali yake sasa imebadilika na amelazwa katika wodi ya wagonjwa mahututi (ICU).

Chanzo kilieleza kuwa, daktari mwingine aliyemfanyia upasuaji mgonjwa mwenye matatizo ya kichwa, kwenye mguu alikuwa ni mwanamke, aliyesomea udaktari wake hapa nchini, ambaye alisomea mifupa.

"Daktari huyo alifungua mguu kwa mtu aliye na tatizo la ubongo. Baada ya kufungua mguu huo, aligundua kuwa ni mzima, akaandika ni normal. Hakufuata taratibu," kilisema chanzo hicho.

Kwa maelezo ya chanzo hicho, kuna hatua za kufuata kwa daktari kabla ya kufanya upasuaji kwa mtu yeyote.

Kilisema kuwa kiutaratibu, daktari anatakiwa kumjua mgonjwa wake siku moja au mbili kabla ya kumfanyia upasuaji. Pia wale wauguzi wanatakiwa waweke faili la mgonjwa na utambulisho wake katika kitanda chake.

Kiliongeza chanzo hicho kuwa, hata kule katika chumba cha upasuaji, yule anayehusika na kutoa nusu kaputi, inatakiwa ajue kiasi cha dawa anayotakiwa kuchanganya kulingana na mgonjwa mwenyewe pamoja na yule anayefanya upasuaji inatakiwa ajue kama ndiye mgonjwa aliyemwona kabla.

"Inashangaza hizi hatua zote hawakujua kuna tatizo, inaonyesha umakini umekosekana. Madaktari wa sasa hawatakiwi kuwa hivyo, wanatakiwa umakini," kilisisitiza chanzo chetu.
 
Mimi nafikiri matatizo ya nchi yetu ni makubwa kuliko tunavyofikiria. Yapo kila kona, si tu katika siasa. Kama daktari anaweza akamfanyia mtu upasuaji wa kichwa badala ya mguu, hivi jamani utasema hapo ni siasa tena? Very confusing! Hii dhana ya uwajiikaji itafika siku tutaielewa kweli katika nchi yetu?.

...hivi hao wagonjwa wenyewe wakati wanatayarishwa kwa Operation nao walikuwa, "NDIO , NDIO, NDIO!" tu? Sometime mgonjwa nae anachangia kum mislead daktari, Kama mguu ndio unauma, kwanini hakushangaa "KUTAYARISHWA" kichwa kwa upasuaji (i.e kunyolewa, etc)?. yule anayehusika na kutoa nusu kaputi, inatakiwa ajue kiasi cha dawa anayotakiwa kuchanganya kulingana na mgonjwa mwenyewe pamoja na yule anayefanya upasuaji inatakiwa ajue kama ndiye mgonjwa aliyemwona kabla. Daktari anatakiwa kumjua mgonjwa wake siku moja au mbili kabla ya kumfanyia upasuaji

Mzee Yebo yebo ingawa sikupingi lakini haya mambo hayataondoka kwa Maombi na Sala.Tutafute suluhisho la kudumu kama jamii.

You are very right. Tumeomba sana, na huenda tumeshapewa hicho tunachoomba lakini hatutaki kukitumia!

...akili za kung'amua zuri na baya, hasa kusema NDIO au HAPANA, sio kila lisemalo daktari mgonjwa anasema ndio! mfano; 'jino linalouma la juu unasema "ndio" ling'olewe la chini!', Upuuzi mtupu!

Sasa kuna kisa kingine nimepewa tu muda mfupi uliopita kwamba katika hospitali hiyohiyo kubwa ya kwetu kuna mwanaume mmoja juzi amepima mkoja-majibu yalipokuja akaambiwa UPT+ yaani ana mimba!!! Yeye of course alikuwa hajui UPT+ nini, alishangaa daktari akawa anamuuliza haya ni majibu yako, naye akawa anamshangaa daktari kumuuliza swali hilo wakati anamjua fika!
!

...na ilikuwaje huko maabara wakaamua kumfanyia huyo MWANAUME (UPT) Urine for Pregnancy Test? kama sio kutafutana mchawi?

"Pia wale wauguzi wanatakiwa waweke faili la mgonjwa na utambulisho wake katika kitanda chake.

... tatizo la msingi lipo hapo ^^^ (Wauguzi)!!!!!!
 
Hii issue ni complicated sana na inasikitisha.Lakini technically ni kwamba kwa mtu anayeitwa daktari na alikula kiapo siku ya kutunukiwa hiyo shahada haiwezekana mambo yakawa rahisi kama hiyo article juu inavyoeleza.Ambacho pia hakikukaa sawa ni kutaja sehemu hawa madaktari waliposomea, japo majina yao yamehifadhiwa.Hii inaleta picha nyingine kwamba labda hawakupata training muafaka walikosomea (incompetent).Nadhani article ya gazeti la mwananchi la leo inaelezea kwa undani zaidi hali ilivyokuwa.Sijaflash back nione kama na hayo maelezo yapo kwenye hii thread au la.Ila ukiangalia haraka ni kwamba wagonjwa wanafanana majina na operation zimekuwa opposite katika muda unaofanana(wa mguu ikawa kichwa na kichwa ikawa mguu on the same day).Hivyo suala la competence hatuwezi kulizungumzia ikiwamo daktari kuchukua sample fulani kutoka kwa mgojwa.Nadhani zaidi ni uzembe uliotokea wagonjwa wakachanganywa.Natumaini tujadili mada katika mwelekeo huo_Otherwise tukisema fulani amefanya kosa sababu alikuwa trained sehemu fulani tutakuwa hatuzitendei haki nchi husika ikiwamo Tanzania.Labda kwa wale ambao hawajaiona hiyo current article ni kwamba daktari yaliyomkuta ndio alikuwa bingwa na tegemeo katika idara husika na kwamba baada ya kusimamishwa na kazi imeanza kusuasua hapo idarani
 
Mkasa wa Muhimbili, upasuaji waanza kulegalega MOI
* Hakuna Daktari wa kupasua kichwa
* Aliyekuwapo amesimamishwa kazi

* Chanzo cha mkanganyiko chaelezwa

*Daktari aliyepangwa hakutokea


Na Jackson Odoyo


SIKU chache baada ya daktari aliyefanya upasuaji tata wa kichwa kwa mgonjwa aliyetakiwa kupasuliwa mguu, huduma za upasuaji wa kichwa katika Taasisi ya Mifupa (MOI) zimelezwa kuanza kulegalega.


Kwa mujibu wa taarifa kutoka ndani ya taasisi hiyo zilizothibitishwa na baadhi ya maafisa wake ambao hawakutaka kutajwa majina yao, daktari aliyempasua kichwa mgonjwa aliyekuwa na matatizo ya mguu ndiye aliyekuwa bingwa na mkongwe katika upasuaji wa aina hiyo kwenye taasisi hiyo.


Taarifa hizo zimedai kwamba daktari huyo tangu aliposimamishwa kumekuwa na msongamano wa wagonjwa wanaosubiri huduma ya upasuaji wa kichwa kwa sababu yeye ndiye aliyekuwa msimamizi wa madaktari wengine wakati wa upasuaji.


"Tangu daktari huyo aliposimamishwa kuna msongamano wa wagonjwa wanaosubiri upasuaji wa kichwa kwa sababu yeye ndiye aliyekuwa msimamizi mkuu wa huduma ya upasuaji wa kichwa kwa wagonjwa maalum," alisema mtoa taarifa hiyo.


Hata hivyo watoa taarifa hizo walisema kwamba siku ya tukio daktari huyo hakuwa zamu, ila alifika hospitalini hapo kwa lengo la kumsimamia daktari aliyetakiwa kumfanyia Emmanuel Mgaya upasuaji wa kichwa, lakini baada ya kufika akakuta daktari aliyetakiwa kumpasua mgonjwa huyo ana udhuru ndipo alipoamua kuingia na kumfanyia upasuaji wa kichwa Emmanuel Didas badala ya Mgaya.


Taarifa hizo zinadai zaidi kuwa kwamba daktari huyo hakuwahi kumuona mgonjwa kabla ya kumfanyia upasuaji na kwamba alipoingia kwenye chumba alikuta tayari mgonjwa ameshachomwa sindano ya usingizi (nusu kaputi).


Inadaiwa kwamba kabla ya kumpasua aliuliza mbona hajanyolewa kichwa ndipo wauguzi waliokuwa zamu wakamnyoa bila ya kutoa maelezo kama mgonjwa huyo ndiye aliyetakiwa kufanyiwa upasuaji wa kichwa.


Baada ya daktari huyo kumaliza upasuaji alimkabidhi mgonjwa kwa wauguzi ili wamrudishe katika wodi ya wagonjwa ambao walimrudisha wodini na kumkabidhi mjomba wake.


Lakini baada ya mjomba wake huyo kumtazama mgonjwa, aligundua kwamba hakuwa ndiye kisha akatoa taarifa kuwa huyo siyo ndugu yake.


Maafisa hao wanaendelea kudai kwamba baada ya hapo wauguzi walirudi kumueleza daktari aliyehusika katika kumpasua mgonjwa huyo kwamba siye mgonjwa aliyetakiwa kufanyiwa upasuaji huo na kwa kuwa siku hiyo mgonjwa aliyefanyiwa upasuaji wa kichwa alikuwa ni mmoja tu ndipo waliamua kuwatafuta wagonjwa wote waliofanyiwa upasuaji siku hiyo.


Akizungumzia suala hilo Afisa Uhusiano Msaidizi wa taasisi hiyo , Mary Ochieng alisema ingawa msongamano upo, lakini si kwa kiasi kikubwa kama inavyoelezewa kuathiri wagonjwa.


Hata hivyo ndugu wa mgonjwa, kijana Emanuel Didas aliyefanyiwa upasuaji wa kichwa badala ya mguu wameanza mikakati ya kufanya vikao vya familia na ukoo ili kujadili mambo mbalimbali hususan suala la afya ya mgonjwa wao.


Kati ya mambo ambayo wanajadili ni namna ya kumpeleka ndugu yao nje ya nchi ili akafanyiwe uchunguzi wa kina kuhusu afya yake .


Akizungumza na Mwandishi wa habari hizi jana ofisini kwake, kaka wa mgonjwa huyo alisema kwamba japo yeye si msemaji wa familia na hapendi kujatajwa gazetini, lakini ukweli ni kwamba wameshaanza vikao vya kujadili namna ya kumsaidia ndugu yao.


Alisema taarifa waliopewa na uongozi wa hospitali hiyo iliwashutua na ikaonyesha ni kwa kiasi gani wanalengo la kupindisha taarifa ya madaktari kuhusu afya ya mgonjwa baada ya kufanyiwa upasuaji.


Alisema baada ya madaktari hao kumaliza upasuaji waliwaita mjomba wa Emmanuel Mgaya na kumwambia kwamba aende akamchukuwe ndugu yake kwa sababu walishamaliza kazi yao bila kumwambia kwamba hawajaona tatizo lolote .


Alilalamika kwamba hata walipouliza kwamba walipomfanyia upasuaji huo walitoa nini, ama kukuta matatizo gani katika kichwa chake walisema hawakuona kitu.


"Kinachotushangaza ni kwamba madaktari hao hawataki kusema ukweli kama kuna kitu walikitoa katika kichwa cha ndugu yetu, hii ndiyo inayotupa wasiwasi wa kutaka kumpeleka ndugu yetu nje ya nchi kwa vipimo maalum ili kubaini kama mgonjwa wetu amepata madhara makubwa katika mfumo wake wa mawasiliano," alisema.


Wagonjwa hao walifanyiwa upasuaji tata Novemba mosi, mwaka huu katika hospitali ya MOI ambapo Emmanuel Didas alipasualiwa kichwa badala ya mguu na Emmanuel Mgaya alifanyiwa upasuaji wa mguu badala ya kichwa.


Kaka mwingine wa kijana aliyepasuliwa kichwa ambaye ni msemaji wa familia, Sestis Marishay alisema ni kweli kuna mipango hiyo, lakini hawajajua watampeleka nchi gani kwa sababu vikao havijaanza rasmi na anayesubiriwa ni mama yake mzazi aliyepo Moshi, ikiwa ni pamoja na kusubiri majibu ya tume iliyoundwa na serikali.


Kuhusu hali za wagonjwa hao, aliyepasuliwa kichwa hali yake ya kiafya bado ni mbaya, lakini ameanza kufumbua macho na kuchezesha mkono bila kutambua chochote na aliyepasuliwa mguu badala ya kichwa hana mabadiliko na anaendelea kulalamikia maumvivu ya kichwa, ila kidonda cha mguu kimeanza kupona.


Nadhani tuiangilie hii issue kwa kuangalia na mantiki ya hii story.Tuwe na common stand kwamba future ni ipi?
 
Kuna fununu kwamba Dr aliyekuwa assigned kuwafanyia operation wagonjwa hawa alikuwa ameenda kufanya operation katika hospitali binafsi na kazi hiyo akawaachia madaktari wenzake yeye akaenda kutafuta pesa. Tatizo hilo pia imesemekana si mara moja kutokea hapo MNH kwani hata hivyo imekuwa ni bahati hao walipona maana ikiwa wangekuwa wamefariki basi isijulikana nini kimekuwa kikijiri katika hospitali hiyo. Wakati nikizunguka zunguka mitaani kupata japo feedback toka kwa wananchi kuhusiana na sakata hilo wananchi wengi wamelaumu serikali kuwaruhusu madaktari wengi kuwa nje ya sehemu zao za kazi tatizo ambalo wananchi wanasema ni hatari kwa maisha yao kwani mara kwa mara madaktari wanafunzi wamekuwa wakijifunzia kazi zao kwa wagonjwa kama hilo lililotolea.
 
problem ya MNH ni kwamba madaktari wanafunzi wanaachiwa wafanye operation bila ya kuwa na chief surgeon. hapo ndipo mambo yanapokwenda hovyo
 
Maelezo yako BM yametuongezea mwanga zaidi kwamba mhusika mkuu wa operation hakuwepo,na kwamba daktari aliyefanya operation ya kichwa ilikuwa kama emergency case na hakuwa anaifahamu kwa mapana yake. This is a serious problem,huyo mtoro anastahili consequences zote.
 
problem ya MNH ni kwamba madaktari wanafunzi wanaachiwa wafanye operation bila ya kuwa na chief surgeon. hapo ndipo mambo yanapokwenda hovyo

Ukisoma story ya niliyopost hapo juu,wanadai daktari aliyefanya operation ndiyo bingwa na tegemeo katika kufunua vichwa vya wagonjwa.
 
faili linatakiwa liwe kwenye kitanda cha mgonjwa na daktari anayefanya upasuaji amjue mgonjwa wake siku moja kabla.
hapa hii issue watatupiwa lawama ni manesi
tutaona majibu ya uchunguzi wa tume
 
Uliyosema ni kweli tupu.Surgeon anatakiwa amfahamu mgonjwa kabla ili aweze kujiandaa technically.Lakini hii ilifanyika kama emergency baada ya mhusika kutoweka.
 
...hivi hao wagonjwa wenyewe wakati wanatayarishwa kwa Operation nao walikuwa, "NDIO , NDIO, NDIO!" tu? Sometime mgonjwa nae anachangia kum mislead daktari, Kama mguu ndio unauma, kwanini hakushangaa "KUTAYARISHWA" kichwa kwa upasuaji (i.e kunyolewa, etc)?. yule anayehusika na kutoa nusu kaputi, inatakiwa ajue kiasi cha dawa anayotakiwa kuchanganya kulingana na mgonjwa mwenyewe pamoja na yule anayefanya upasuaji inatakiwa ajue kama ndiye mgonjwa aliyemwona kabla. Daktari anatakiwa kumjua mgonjwa wake siku moja au mbili kabla ya kumfanyia upasuaji





...akili za kung'amua zuri na baya, hasa kusema NDIO au HAPANA, sio kila lisemalo daktari mgonjwa anasema ndio! mfano; 'jino linalouma la juu unasema "ndio" ling'olewe la chini!', Upuuzi mtupu!



...na ilikuwaje huko maabara wakaamua kumfanyia huyo MWANAUME (UPT) Urine for Pregnancy Test? kama sio kutafutana mchawi?



... tatizo la msingi lipo hapo ^^^ (Wauguzi)!!!!!!

Tatizo haliko kwa wagonjwa hata mara moja kwani wakati huo walikuwa tayari hawajitambui tatizo la DR aliyehusika kuwapasua wale wagonjwa ni hili kabla hujapewa hata nusu kaputi Dr hufanya usaili kwa mgonjwa akikuuliza yafuatayo:
1. Jina lako nani
2. Umri wako.
3. Unachoumwa ni nini.
4. Wazazi au ndugu zako majina yao.
5. Je unataarifa kwamba utafanyiwa operation n.k n.k.

Procedures hizi waliozitengeneza hawakuwa wajinga kabisa walifanya hivyo kwa ajili kwanza kumuweka mgonjwa katika psychology ya kwamba anatarajia upasuaji, lakini pia ilikuwa ni kumsaidia Dr kuelewa mambo mengi kuhusu mgonjwa wake anakuwa na hali gani katika dakika zile za mwisho kabla ya upasuaji kuanza kufanyika.

IKIWA HILO LINGEFANYIKA

1. Dr aliye mpasua mgonjwa wa goti badala ya kichwa swali lingekuwa hivi.

1. Jina lako nani
Imanuel Mgaya
2. Umri wako
this and that
3. Unaumwa nini
KICHWA

nk nk nk nk nk nk nk nk nk nk nk nk nk nk nk nk nk nk nk nk nk

Kwa usaili huu fika angeweza kugundua mgonjwa huyu anatakiwa kupasuliwa kichwa na si mguu na kamwe hangekosea kama ilivyotokea. Hii hata kama alikuta tayari mgonjwa huyo wa goti alikutwa hajanyolewa nywele.
Vivyo hivyo kwa mgonjwa wa goti hangeweza kupasuliwa kichwa kama ilivyotokea.
 

Hapana, siwalaumu kabisa hawa madaktari wawili kwa hili!!!

...mwisho wa kuonana na mgonjwa huenda ikawa masaa machache kabla ya Operation, baada ya hapo, Surgeon/ daktari mpasuaji akiwa theatre anasubiri mgonjwa ni 'kawaida'/ni kazi ya manesi/wahudumu kumtoa mgonjwa surgical ward kumpeleka theatre.

...mgonjwa anapoletwa theatre, daktari hapo si kazi yake tena kuangalia sura ya mgonjwa, kwani procedures zote zinatakiwa ziwe zishakamilishwa na i.e anaethetist (mtoa nusu kaputi), na Nurse in charge. Kazi ya Daktari hapo ni kuendelea tu na upasuaji!

...ndio maana nawatetea madaktari wote hawa wawili walofanya upasuaji huu, kwani walowajibika kumpeleka mgonjwa wa mguu kufanyiwa Op ya kichwa na mgonjwa wa kichwa kupelekwa theatre ya kufanyiwa Op ya mguu ndio hao walolikoroga!

...Kuhusu kwanini alitoa kipande cha ubongo kwa uchunguzi, hii inatokana na earlier assesment ya infected area, abnomality lazima ifanyiwe tathmini, hata kama ni ndogo kama mdudu chungu. Kma mgonjwa mpaka leo hajaamka inatokana na kuwa kwenye induced coma, ataamka tu, Op ya ubongo sio ya mguu.

fingers crossed!
 
Hii habari imefika mpala BBC. Nimemaliza kuangalia BBC America na wao wameizungumzia. Hata kwenye site yao ipo. Kweli kuna kazi.

Tanzania in surgery name mix-up
By Vicky Ntetema
BBC News, Dar es Salaam



Migraine sufferer Emmanuel Mgaya recovering from knee surgery
A Tanzanian hospital has mixed up two patients who share the same first name, resulting in a surgery blunder.

Emmanuel Didas, who was admitted for a knee operation after a motorbike accident, is now unconscious in intensive care after head surgery.

Meanwhile, chronic migraine sufferer Emmanuel Mgaya is recovering from an unplanned knee operation.

Some angry relatives are demanding a full investigation into the incident at Muhimbili Hospital in Dar es Salaam.

Doctors at Muhimbili National and Referral Hospital are unwilling to comment on the incident which occurred last week, but was not officially reported.

The Ministry of Health and Social Welfare says it has ordered an inquiry into the medical blunder.

Shock

"This is negligence because a doctor must know that a knee is positioned very far from the head," said one of Mr Didas's relatives.

What has happened has not made us lose faith

A relative of Emmanuel Mgaya

The family, who are keeping vigil outside the intensive care ward, has not yet been told the details of his unexpected head surgery.

"The doctors did not even tell us that Emmanuel had had a head operation. It is the responsibility of a doctor to ensure patients get the right treatment," the relative said.

Outside a surgical ward, the relatives of secondary student Emmanuel Mgaya explained how they felt the unfortunate accident had come about.

"We think maybe the nurses mixed the patients' files because they were admitted in the same ward and sharing the same first names," one said.

Mr Mgaya had recently developed acute headaches while studying for his final secondary school exams and was referred to Muhimbili Hospital from a remote district in the Southern Highlands of Tanzania.

"We still have faith in the doctors. What has happened has not made us lose faith," his upbeat family said.

"And we have already spoken to the hospital director who has reassured us that the qualified consultants will operate on our Emmanuel Mgaya. So we are not worried."

But Mr Didas's family remain shocked and dismayed.

"A person has several names. The medical staff should have checked this before the operation," one said.
 

Hapana, siwalaumu kabisa hawa madaktari wawili kwa hili!!!

...mwisho wa kuonana na mgonjwa huenda ikawa masaa machache kabla ya Operation, baada ya hapo, Surgeon/ daktari mpasuaji akiwa theatre anasubiri mgonjwa ni 'kawaida'/ni kazi ya manesi/wahudumu kumtoa mgonjwa surgical ward kumpeleka theatre.

...mgonjwa anapoletwa theatre, daktari hapo si kazi yake tena kuangalia sura ya mgonjwa, kwani procedures zote zinatakiwa ziwe zishakamilishwa na i.e anaethetist (mtoa nusu kaputi), na Nurse in charge. Kazi ya Daktari hapo ni kuendelea tu na upasuaji!

...ndio maana nawatetea madaktari wote hawa wawili walofanya upasuaji huu, kwani walowajibika kumpeleka mgonjwa wa mguu kufanyiwa Op ya kichwa na mgonjwa wa kichwa kupelekwa theatre ya kufanyiwa Op ya mguu ndio hao walolikoroga!

Nakubaliana na wewe.
Pia kuwasimamisha watu wawili tu ni uonevu list nzima ya waliohusika isimamishwe akiwemo theatre in charge!Kuna mtu aliyetakiwa kuhakikisha kuwa mgonjwa aliyetolewa wodini kwenda kupasuliwa kichwa amefikishwa kwenye operation room ya Neurosurgery na sio ya orthopaedics...na vice versa walifanya hivyo???? Nao wasimamishwe. Yule aliyetakiwa kumpokea mgonjwa husika na kuhakikisha amelala kwenye theatre husika na asimamishwe...
Muhimbili mambo yanaendeshwa kienyeji sana mfano nesi anapewa kazi ya kukupeleka ukapige X ray . Yeye nakukuonyesha kwa kidole ingia hapo anawaambia ndugu zako endeleeni kusubiri naye hapo halafu anatoweka . Anawapa na maagizo ya mwisho " Mkimaliza mtamleta eeh! Sawa. Ndugu wanaitikia sawa. Sasa mtasubiri rehema za Mungu mkifanikiwa hewala......
Ukiwa una ufahamu kidogo na kinachoendelea ukahoji...unakuwa victimised...Nurses are good in that na tena wanahakikisha wanamwambia daktari huyu mgonjwa mkorofi sana.Kwa kifupi uswahili unaondelea mitaani ndio umefika hapo.Hakuna usimamizi na vifo vingi vinaendelea kwa sababu ya negligence.
Coming back to MOI issue...
Was this event planned???? Somebody ??? Switched the patients before they were taken to respective theatres. Inawezekana kwani all the patients had the same names??Tusubiri uchunguzi!!!!!Kwa sababu watu waanza kutoa matatizo mengi zaidi....kwamba kuna uongozi mbovu. Je walisubiri hadi tukio hili litokee ndio watoe hizo hoja??Daktari mpasua kichwa alihoji mbona kama ni mgonjwa wa kupasuliwa kichwa hajanyolewa nywele??? And this question did not click that something was wrong???Alitakiwa awe amenyolewa nywele!!!!
Kwa hiyo ina maana kila mtu alishatayarishwa inavyotakiwa na mambo "yalikosewa" wakati wa kuingia vyumba husika??
Most probably madaktari waliwakuta wote tayari wapo kwenye usingizi na mafaili sahihi wakaendelea. Na hawa wote walikuwa makini kwani kila mtu alikuta ni normal
Lingine ni kuhusu waandishi wetu ....acheni ushabiki study the issues in deep. Wengi wa madaktari wetu wanafanya kazi ktk mazingira magumu na kwa kweli ni kama wanajitolea tu. Hizi habari mnazoziandika kishabiki mnakuwa hamwatendei haki....fanyeni deep analysis...Watu wanaamini kwamba hawa madaktari ni wazembe which here it is not the case!!!Be fair to these doctors please.
 
...
Outside a surgical ward, the relatives of secondary student Emmanuel Mgaya explained how they felt the unfortunate accident had come about.

"We think maybe the nurses mixed the patients' files because they were admitted in the same ward and sharing the same first names," one said.

"A person has several names. The medical staff should have checked this before the operation," one said.

...kidogo kidogo ukweli utadhihiri, na uwongo kujitenga japo ndio hivyo tena...

Wengi wa madaktari wetu wanafanya kazi ktk mazingira magumu na kwa kweli ni kama wanajitolea tu. Hizi habari mnazoziandika kishabiki mnakuwa hamwatendei haki....fanyeni deep analysis...Watu wanaamini kwamba hawa madaktari ni wazembe which here it is not the case!!!Be fair to these doctors please.


...anatafutwa 'mtu/watu' wa kutolewa kafara!
 

Hapana, siwalaumu kabisa hawa madaktari wawili kwa hili!!!

...mwisho wa kuonana na mgonjwa huenda ikawa masaa machache kabla ya Operation, baada ya hapo, Surgeon/ daktari mpasuaji akiwa theatre anasubiri mgonjwa ni 'kawaida'/ni kazi ya manesi/wahudumu kumtoa mgonjwa surgical ward kumpeleka theatre.

...mgonjwa anapoletwa theatre, daktari hapo si kazi yake tena kuangalia sura ya mgonjwa, kwani procedures zote zinatakiwa ziwe zishakamilishwa na i.e anaethetist (mtoa nusu kaputi), na Nurse in charge. Kazi ya Daktari hapo ni kuendelea tu na upasuaji!

...ndio maana nawatetea madaktari wote hawa wawili walofanya upasuaji huu, kwani walowajibika kumpeleka mgonjwa wa mguu kufanyiwa Op ya kichwa na mgonjwa wa kichwa kupelekwa theatre ya kufanyiwa Op ya mguu ndio hao walolikoroga!

...Kuhusu kwanini alitoa kipande cha ubongo kwa uchunguzi, hii inatokana na earlier assesment ya infected area, abnomality lazima ifanyiwe tathmini, hata kama ni ndogo kama mdudu chungu. Kma mgonjwa mpaka leo hajaamka inatokana na kuwa kwenye induced coma, ataamka tu, Op ya ubongo sio ya mguu.

fingers crossed!

Are u in the field?
Kwa kweli wewe umeongea.Kilichotokea hapa ni mawasiliano mabovu na wanaopaswa kumuandaa Mgonjwa kuchanganya kila kinachomuhusu mgonjwa na kumfanya daktari kuamini anayemshughulikia ndiyo Ukizingatia tena kwenye operation za vichwa mtu sura inawekwa chini na kichwa juu inategemea ni upande gani wa kichwa unapasuliwa.Alichofanya Dk husika kuchukua Biopsy ni sahihi kwani Baada ya kufunua kichwa hakukuta kilichopo kwenye CT-Scan, HAPA ALIONYESHA UMAKINI KWANI ASINGEKUWA MAKINI ANGEWEZA HATA KUKATA KITU KINGINE KWA KUDHANI NI KILICHOONYESHWA KWENYE SCAN,Lakini kugundua kwamba kilichoonyeshwa kwenye CT hakipo kwa huyo mgonjwa kumesaidia sana kuepuka madhara ya hasa ukizingatia huyo Dr si yeye aliyetakiwa kufanya hiyo kazi .
 
Back
Top Bottom