Elections 2010 Inawezekana mali za CCM kurudi Serikalini?

mudushi

Senior Member
Oct 19, 2010
151
84
Wana JF mi huwa najiuliza CCM ina mali nyingi ambazo wazazi wetu na sote tulizichangia km vile viwanjavya mipira (Jamhuri, kirumba nk) ofc nyingi tu. Je kuna uwezekano zikarudi serikalini maana ni mali zetu sote?

Nisaidieni p'se.
 
Itawezekana wakati ambao CCM watakuwa wameshindwa kwenye uchaguzi. Serikali itakayokuwa madarakani, ambayo si ya CCM, ndo itatirudisha mali hizo serikalini.
Wana JF mi huwa najiuliza CCM ina mali nyingi ambazo wazazi wetu na sote tulizichangia km vile viwanjavya mipira (Jamhuri, kirumba nk) ofc nyingi tu. Je kuna uwezekano zikarudi serikalini maana ni mali zetu sote?

Nisaidieni p'se.
 
Hizi ni mali za wananchi, sio za CCM. Ilibidi/inabidi zirudi kwa wananchi (serikalini). Amini au usiamini "hakuna marefu yasiokuwa na ncha".
 
Wana JF mi huwa najiuliza CCM ina mali nyingi ambazo wazazi wetu na sote tulizichangia km vile viwanjavya mipira (Jamhuri, kirumba nk) ofc nyingi tu. Je kuna uwezekano zikarudi serikalini maana ni mali zetu sote?

Nisaidieni p'se.
Hiki kitu hata mimi huwa kina niumiza kichwa sana kuna majengo yalijengwa na wazazi wetu leo tuna ambiwa ni mali ya ccm mifano ni hapo juu...iko siku tutarudisha mali za wananchi na siyo kumilikiwa na mafisadi kijanja janja tu
 
Itawezekana kama watanzania watafumbua macho na kujua baya ni lipi na zuri ni lipi,pia Demokrasia itakapo kuwa imechukua mkondo wake ili Maamuzi ya waliyo wengi yeweze kuchukua nafasi ya maamuzi.
 
Zitarudi tu ni suala la muda na watalipa faida yote waliyokula kutokana na mali hizo tangu 1992
 
Sasa hivi wakati ccm bado wako madarakani sahau. Kama unabisha, jaribu kumpa paka kipande cha nyama, halafu akianza kula msogelee ukitaka kukichukua kipande kile ili umgawie paka mwingine ambaye ndio kwanza katokea kutoka porini, utasikia music. Hata mbwa wana hulka hiyo. Music utakaousikia ndio sawasawa na ule ccm watakaoutoa kwako kama unataka kurudisha mali za wananchi kwa wananchi ambao kusema kweli ndio walioikabidhi ccm wakati wa chama kimoja. Ili kukipata kipande hicho bila bughudha, mwondoe paka huyo kwa style yoyote halafu kichukue kipande na kukifanya utakavyo.

Damu iliyokuwa inaimbiwa kumwagika wakati wa kampeni, nyingi ilimwagwa na mashabiki wa ccm, lakini kwa kuwa wapinzani hawana visemeo vya uhakika kujitetea wakageuziwa kibao na wao sasa wakaonekana wanamwaga damu. CCM atakapokuwa KANU au ZANU ndipo wataweza kuelewa unachosema. Hata ukiwapeleka mahakamani kwa sasa watatetewa tu. Humsikii Chenge anamponda SITTA kwa sababu ati aliachia mafisadi waanikwe hadharani na sasa anadhani yeye atamudu kudhibiti Bunge lisiongelee mambo hayo akiwa speaker? Mungu ibariki Tanzania, Mungu ibariki Afrika.
 
Inawezekana, ila lazima iwe chama nyingine ndani na siyo ccm..

Kenya walikuwa na kenyatta conference center(kcc) pnu ya kibaki walipochukua nchi wakalirudisha serekalini.
 
So rahisi na si kweli mal za CCM ni za Watanzania na wana CCm ni watanzania. Wao ndio walioanza mali ni zao na nyie CHADEMA mkiwa madarakani fanyeni vyovyote mwezavyo hatutawadai.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom