Mwigamba Mungu hakuwachagulia Israel mfalme bali aliwaacha wafuate mawazo yao ya kuwa na mfalme kama mataifa meingine.Israel hapakuwa na mfalme bali Mungu mwenyewe alikuwa akiwaongoza Israel kupitia watumishi wake kama akina Samuel. Mungu hajipingi mtu wa Mungu atakuwa anaonekana ( mtawatmbua kwa matunda yao).
1Sam9:15-17 Basi Bwana alikuwa amemfunulia Samweli, siku moja kabla Sauli hajamwendea, akisema,
Kesho, wakati kama huu, nitakuletea mtu kutoka nchi ya Benyamini, nawe mtie mafuta ili awe mkuu juu ya watu wangu Israeli, naye atawaokoa watu wangu na mikono ya Wafilisti; maana nimewaangalia watu wangu, kwa sababu kilio chao kimenifikilia.
Hata Samweli alipomwona Sauli, Bwana akamwambia, Huyu ndiye niliyekuambia habari zake; huyu ndiye atakayewamiliki watu wangu.