inawezekana kuwa na mpenzi unayemzidi upeo?

habari za asubuhi wana mmu, ni mwaka umepita tangu nikutane na huyu kaka. naweza kusema ni wa kawaida sana, yan kimaisha,elimu na muonekano pia. nilikutana naye tukiwa tunasoma koz flan.alionesha nia ya kunitaka kimapenzi ila nilimkatalia kwa sababu binafsi. baada ya kumaliza kozi hakukata tamaa, aliendelea kuwa karibu na sasa tunaelekea kuwa wapenzi. ukaribu wetu umenifanya nigundue kuwa hatuendani kwa kiasi kikubwa, hana upeo wa vitu vingi, hatuendani hata kidogo. je nawezaje kuwa nae ktk hali kama hii?
Kwa ufupi sema A/C yake haisomeki, upeo siyasa QI ndogo kote shosti unazunguka,asikuchoshe sana wala usimchoshe
mwambie huna nnachokitaka kwa mwanamme ili ajipange.....
 
hahaa! umenichekesha billie. nasema hivyo kwa maana kwamba kuna vitu ambavyo huwa anaongea ni local sana hana exposure kabisa! ama ni mshamba flani labda niseme hivyo. pia kuna baadhi ya mambo hajui yaani namuelekeza mambo mengi hadi ananikera. ukimbana na maswali kidogo anashindwa kujieleza mpaka ananibore.

yaani hapo nimekuelewa kabisa...ni vizuri kua na mtu ambae mnaweza ku conversate...ukiwa na mtu ambae kila anapofungua mdomo unakereka au huelewi anaongea nini au mtazamo wake kimaisha ni tofauti na wewe ujue hapo hamtakaa kwa mda mrefu..kama mnapenda muridhishane tu kila mtu aende kivyake..na watu kama hao hawabadiliki
 
duh, mabwaku! wakat wengne tunapinga mfumo dume wengne wanaulilia. haki ya kwel tupo tofaut sna. . .
 
...Kwa maoni yangu mahusiano yakiwa katika viwango hivi kati ya wahusika basi huwa hayana maisha marefu, ila wako njemba/wadada wengine wanaweza kuvumilia. Amua kunyoa ama kusuka haraka sana lakini wakati huo huo ujue kupata mchuchu mwingine inaweza kuchukua muda au kama tayari ulikuwa naye mwingine :):) ambaye inabidi apewe promotion ya nguvu.

hahaa! umenichekesha billie. nasema hivyo kwa maana kwamba kuna vitu ambavyo huwa anaongea ni local sana hana exposure kabisa! ama ni mshamba flani labda niseme hivyo. pia kuna baadhi ya mambo hajui yaani namuelekeza mambo mengi hadi ananikera. ukimbana na maswali kidogo anashindwa kujieleza mpaka ananibore.
 
Last edited by a moderator:
daah dada umenishangaza sana! Upeo umepima na kitu gangi? IQ TEST?,unataka mwanaume wa show? Mapenzi hayapo hivyo nikwamba ww humpendi, unatakakuniambia hata ukiolewa na mwanaume ikatokea ukawa na pesa au kupandishwa cheo,au ukajiendeleza kuliko yeye utaachana nae na kutafuta mwingine?? Unaeendana nae? Dada wanawake wadisign ya ww huwa hawaolewi ukiolewa utaachika tu kwani hawanatabia ya kujishusha na kunyenyekea.katika ndoa huwahatuangalii tofautihizo kwa binadam hatufanani au me au ke.mfano halisi.mama yangu alikuwa draja la 3A na baba alikuwa na 1st degree,wakaanza hadi sasa mama ana Phd na baba masters,alichotamka baba ni kwamba mama sikuwezi ww endelea. Ukweli bimkubwa anauwezo na upeo wajuu sana amba dad hukili wazi.nawanaishimaisha ya amania na upendo.uwezo wa akili,pesa,maumbile si tija dada utachina.
 
inatosha My Dear,ujumbe Wa Busara Umefika!
 
haelewi mambo mengi, mfano issue za ujasiriamali, nini kanaendelea duniani, siasa. in short hayupo updated kabisa. ni mshamba mshamba tu

Well say mrembo? naomba nikuulize swali na mie hivi wewe ulipoanza shule ulikuwa unajua kusoma? mie nafikiri unaweza kuwa mwalimu kwake ukamfundisha mpaka akaelewa. ni kwa nini unasema ana upeo mdogo haelewi ili khali wewe upo ina maana huwezi kumfundisha, hapo kwenye bold hakuna anaezaliwa anajua kila kitu na hata mbuyu ulianza kama mchicha. kama unampenda mfundishe kumbe walimu wana kazi ngumu sana na wana moyo wa pekee.
 
yaaani mai lavu ndo umeamua kuja kunichana huku..dah kweli umenichoka.
 
soma post yangu ya kwanza. nimesema tunaelekea kuwa wapenzi

Yaani wewe mpaka kuleta shauri hapa maana yake limekushinda, kakuchanganya akili.

Kwa hiyo huwezi kuwa umemzidi upeo kiasi hicho.

Ungemzidi upeo kiasi hicho ungefanya uamuzi mmoja tu na kulimaliza.
 
*******you don't love him at all, if you love somebody then you will have no time to judge**********
 
Nyakwatory, mie naweza jaribu elezea nachokiona hapa kwa mtindo huu.

Kuna kitu kichokuvuta kwa huyu kaka, ndiyo maana unaanza kuelekea kutaka kuwa na mapenzi naye.
Kitu hicho chaweza kuwa chochote labda kujali kwake, pesa zake, chemistry kwake.

Lakini kutokana na maisha ya 'mwanamme wa kiafrika-Rejea uzi wa Babu Dark City', baadhi ya wanawake wanapenda wanamme wawe viongozi wa familia hasa katika maamuzi. Hii imewafanya baadhi ya wanawake aidha kupenda au kuheshimu mwanamme anayemzidi 'uelewa wa mambo' ili katika maamuzi mengi ya kifamilia au kimahusiano mwanamme aweze kuchukua nafasi yake.

Ikitokea wakati katika mahusiano, mwanamke anakuwa 'smart' kuliko mwanamme maana yake ni kuwa, mambo mengi ya ushauri wa kifamilia au kimahusiano utatoka kwa mwanamke. Kwa watu ambao hawako biased na mfumo dume wala hawashangai na wala hawaoneni tofauti sababu kama mahusiano ni yenu wote na mnafurahia wote.

Kwa baadhi ya wanawake waliokubaliana na mfumo dume, hupenda wanamme watoe maamuzi ili uanamme wake uonekane.

Sasa wewe kikubwa ni kujichunguza, unakubaliana na mfumo dume bila labda hata kutambua??
Kama unakubaliana na mfumo dume, tafuta mwanamme atakayeweza kuwa mwanamme wa kiafrika kwako.

Kwa kifupi, huyu kaka ameshindwa ku-meet expectations zako za mwanamme anatakiwa aweje.
Pamoja sana, hata mie napenda mwanamme ataye-take charge kwenye maamuzi, mie naweza kutoa aidiaz tu
Lakini kufanya maamuzi ya familia afanye mwanamme, na ili uweze ridhika na maamuzi yake lazima awe na upeo aidha wa kulingana na wewe au akuzidi.

Kuna saa unakaa na mtu unajisemea tu moyoni " Dear God, bless his heart"
 
mambo kama haya ndo yanafanya wasichana wa siku hizi wakose wanaume wa maana, matokeo yake wanaishia kuolewa na wanaume na kubaki kunyanyaswa ndani ya nyumba

basi achana naye utafute aliye up-todate
 
Mara nyingi sana umekuwa ukilalamikia kuhusu mapenzi kwenye post zako.......ikawa inaonekana kama kuna mtu anakuchanganya ndiye huyo?
 
Make Sure That In Search Of A Perfect Person
You Don't Loose A True One,
Because
Perfection Is Fantasy
&
Truth Is Reality
 
Huyu mtu kwa kifupi humpendi hata kidogo ni bora usimpotezee muda mwambie ukweli.

Haya ni matokeo ya kuingia kwenye mahusiano wakati unategemea mambo makubwa.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom