Inawezekana kufutwa Azimio la Arusha kulianza Nyerere akiwa bado mwenyekiti CCM

SubiriJibu

JF-Expert Member
Jun 26, 2009
1,803
1,863
Najua JF ni kisima cha kumbukumbu,

Natafuta tarehe ambayo Juliu Nyerere aliachia ngazi unyekekiti wa CCM. Pia na tarehe ambayo NEC-CCM ilikaa huko Zanzibar na kulifuta Azimio la Arusha.

Nataka kujua kama walitumia miaka michache tangu Nyerere aache uenyekiti, basi nitaamini mikakati ya kulifuta Azimio hilo huenda ilianza kwa siri angali Mwenyekiti.

Nasubiri jibu.
 
Ulikuwa unaishi Tanganyika? Au ulikuwa Mtoto chini ya Miaka 5? Azimio la Zanzibar ndilo lililovonja Azimio la Arusha
'
Wakati huo Rais wa Nchi alikuwa na Ali Hassan Mwinyi; Makamu wa Rais John Samwel Malecela

Nyerere hakuwa Madaraka hata kwenye Chama alishang'atuka 1987 Azimio la Zanzibar lilikuwa Miaka ya 1992

Kwanini unaweka Topic bila Ufafanuzi na Bila Ufahamu? Unaifana Jamii Forum kuwa hatuelewi Mengi tusemayo?

* Kama haujui Soma; ELIMU NI UFUNGUO WA MAISHA
 
Najua JF ni kisima cha kumbukumbu,

Natafuta tarehe ambayo Juliu Nyerere aliachia ngazi unyekekiti wa CCM. Pia na tarehe ambayo NEC-CCM ilikaa huko Zanzibar na kulifuta Azimio la Arusha.

Nataka kujua kama walitumia miaka michache tangu Nyerere aache uenyekiti, basi nitaamini mikakati ya kulifuta Azimio hilo huenda ilianza kwa siri angali Mwenyekiti.

Nasubiri jibu.
Mkuu umepata majibu sahihi lete basi hoja yako.
 
Mkuu umepata majibu sahihi lete basi hoja yako.

Mkuu,

Bado nasubiri jibu kwa sababu hawa watoa majibu wanaropoka kwamba Mwalimu Nyerere aling'atuka mwaka 1987 wakati that is terrible mistake kwani aling'atuka rasmi August 17, 1990.
 
Back
Top Bottom