Inawezekana hili wengi walikuwa hawalijui

Mtambuzi

Platinum Member
Oct 29, 2008
8,810
15,398
Kwamba wanawake wengi ambao wameolewa wanapoamua kutoka nje, hutoka na waume za watu, na sio wanaume ambao hawajaoa.

Haifahamiki sana ni kwa nini wanawake walioolewa hutoka nje na wanaume waliooa, lakini tafiti nyingi hutaja sababu kadhaa ambazo zinaonekana kukubalika zaidi.

Moja ya sababu inayotajwa ni kwamba wanawake huamini kwamba wanaume waliooa hawatawasumbua kwa sababu na wao wana majukumu kwenye familia zao. Wanaamini pia kwamba wanaume waliooa watakuwa waangalifu sana kwenye uhusiano huo wa wizi kwa sababu ya kuogopa kunaswa.

Ingawa hawajui kwamba , sio lazima, lakini wanawake wengi huamini kwamba wanaume waliooa huwa hawarukiruki sana kutafuta wanawake kila kona. Kwa hali hiyo, wanaaamini hawatakereka, lakini pia hawatapata matatizo ya maradhi ya zinaa au misukosukoya kukimbizana na mahawara wengine wa wanaume hao.
 
Mh ndio maana wanakuwa viraza kishenz. mkuu kwa tafiti hiyo mbona tumekwisha maana mh wako wangu wangu wako kaaz kweli kweli
 
Nakubaliana, na hao ni wale wanawake wanaochanganya akili zao na za mbayuwayu ili kuhakikisha mchakato unafanyika kwa umakini,
angalia hata viongozi wengi wa dini(mapadri n,k) wao huenda kwa wake za watu wakiamini kuwa wako makini na hawawezi kuvujisha siri ,mf hata akimpa mimba haina shida kwan wa kubambikwa kwa bei rahisi yupo tofaut na msichana tu anayekula kwao,
pia walioko kwenye ndoa inaonekana wanaweza vema hilo zoezi ndio maana wanaleseni(hati ya ndoa)
wao huamin kwamba ukitaka samaki nenda kwa mvuvi!!
 
Kama ni kweli tumekwisha, sitajenga karibu na kanisa!
 
Nakubaliana, na hao ni wale wanawake wanaochanganya akili zao na za mbayuwayu ili kuhakikisha mchakato unafanyika kwa umakini,
angalia hata viongozi wengi wa dini(mapadri n,k) wao huenda kwa wake za watu wakiamini kuwa wako makini na hawawezi kuvujisha siri ,mf hata akimpa mimba haina shida kwan wa kubambikwa kwa bei rahisi yupo tofaut na msichana tu anayekula kwao,
pia walioko kwenye ndoa inaonekana wanaweza vema hilo zoezi ndio maana wanaleseni(hati ya ndoa)
wao huamin kwamba ukitaka samaki nenda kwa mvuvi!!
Acha ujinga wewe!
Padri nani alimpa mimba mke wa nani mwaka gani...Wewe nia yako ni udhalilishaji, na tunaotazama kindani tunakudharau tu!
 
Just a joke, tena nisije kukatiwa fatwa:
Unajua ni mtu gani watu wote humwita "father" isipokuwa mtoto wake ambaye yeye tu humwita "uncle"?.
Jawabu: Padri.
 
Kwamba wanawake wengi ambao wameolewa wanapoamua kutoka nje, hutoka na waume za watu, na sio wanaume ambao hawajaoa.

Haifahamiki sana ni kwa nini wanawake walioolewa hutoka nje na wanaume waliooa, lakini tafiti nyingi hutaja sababu kadhaa ambazo zinaonekana kukubalika zaidi.

Moja ya sababu inayotajwa ni kwamba wanawake huamini kwamba wanaume waliooa hawatawasumbua kwa sababu na wao wana majukumu kwenye familia zao. Wanaamini pia kwamba wanaume waliooa watakuwa waangalifu sana kwenye uhusiano huo wa wizi kwa sababu ya kuogopa kunaswa.

Ingawa hawajui kwamba , sio lazima, lakini wanawake wengi huamini kwamba wanaume waliooa huwa hawarukiruki sana kutafuta wanawake kila kona. Kwa hali hiyo, wanaaamini hawatakereka, lakini pia hawatapata matatizo ya maradhi ya zinaa au misukosukoya kukimbizana na mahawara wengine wa wanaume hao.

sababu kubwa ya msingi ni hiyo ya kwanza yenye rangi nyekundu, na hii ya pili haina ukweli hata kidogo, walio kwenye ndoa wana risk kubwa sana ya kupata kuambukizana ukimwi na magonjwa mengine ya zinaa na wenzi wao.
tabia moja ya uhawara ninayo ijua mimi ni kwamba hiyo ni kama sehemu ya starehe ya mtu, kwa hiyo haitakiwa kuwa misukosuko, hawa vijana wasiooa hawakawii kukubeep usiku umelala na mume eti akikwambia tu kuwa kakumiss, kitu ambacho mume wa mtu hawezi kufanya ! na ukitaka kujua mwenzako ana relatinship na vitoto vidogo angalia atakavyoanza kukoseshwa amani na simu yake, haiweki chini, hata akienda chooni anayo, ikipigwa ajitia network haipatikani ndani hadi aende uani akaongee huko, mara akibipiwa utasikia aah huyu nae anasumbua halafu hata siijui hii namba n.k n.k
 
Kumbe paka ,ungekuwa mtu haya mambo ungeyafaham,
unaposhambulia mawazo ya mtu popote pale na kushindwa kuchangia kwenye mada husika hapo unakuwa na lako jambo, so pleaz badilika na kuwa mstaarabu kwa wenzio popote pale
 
sababu kubwa ya msingi ni hiyo ya kwanza yenye rangi nyekundu, na hii ya pili haina ukweli hata kidogo, walio kwenye ndoa wana risk kubwa sana ya kupata kuambukizana ukimwi na magonjwa mengine ya zinaa na wenzi wao.
tabia moja ya uhawara ninayo ijua mimi ni kwamba hiyo ni kama sehemu ya starehe ya mtu, kwa hiyo haitakiwa kuwa misukosuko, hawa vijana wasiooa hawakawii kukubeep usiku umelala na mume eti akikwambia tu kuwa kakumiss, kitu ambacho mume wa mtu hawezi kufanya ! na ukitaka kujua mwenzako ana relatinship na vitoto vidogo angalia atakavyoanza kukoseshwa amani na simu yake, haiweki chini, hata akienda chooni anayo, ikipigwa ajitia network haipatikani ndani hadi aende uani akaongee huko, mara akibipiwa utasikia aah huyu nae anasumbua halafu hata siijui hii namba n.k n.k

Mkuu unaonyesha una bonge la uzoefu mbona imekaa kiukweli ukweli kwani men hizi ndo zao.
 
Mi naona wanaume waliooa wanaongoza kwa kuruka ruka.
Ndio hao hao wanaoongoza kwa kutoka na vibinti vya shule.
 
Wanawake wanatoka nje kutafuta passion,love and magic we mtu ameolewa Mume full gubu atapataje hivyo nilivyovitaja so it doesn't matter amevipata kutoka kwa aliyeoa au single wanawake ni viumbe wa ajabu sana yaani unaweza kumchota akili yake na kakitu kadoogo!!
 
hii biashara ya kutoka nje ya ndoa sio kabisa, bora kina Jlo wanaotaliki wenzi wao wakiwachoka, ni vema kufuata hisia maisha yenyewe mafupi kama huna hisia na mumeo mkeo ya nini kujing'ang'aniza mtaliki olewa/oa na unaempenda kwanza ikiwa hivyo ndio watu watakuwa na heshima maana ukiharibu unatoswa, wanaume wengine wanaoa watu wa kuangalia nyumba kupika na kufua mapenzi wanatafuta kwingine najiulizaga kwa nini hawakuwaoa hao wanaowafuata nje!! ili watumie mpaka wachoke.
 
Back
Top Bottom