Inauma sana

Wanaume wenye ndoa changa mnahitaji shule kuhusu "Women Psychology". Mke anapokuwa mjamzito kuna mabadiliko hutokea ambayo zaidi ni sababu za kisaikolojia na mabadiliko ya homoni katika mwili. Sababu hizi hazifanani na hutofautiana kutoka mwananamke mmoja na mwingine. Moja ya mabadiliko ni pamoja na kutopendelea aina fulani ya vyakula ambavyo kabla ya ujauzito haukuwa tatizo, baadhi kuwachukiwa waume zao, kukosa hamu ya tendo n.k. na mengine mengi. Kiukweli kuna ambao huwachukia sana waume zao, lakini pia kuna ambao huwapenda sana waume zao kiasi cha kutaka awe naye wakati wote (hii nayo inweza kuwa kero kwa baadhi ya wanaume), kuna wengine wanakuwa neutral zaidi na kukubaliana na hali halisi ya ujauzito.

Haijalishi mimba ni muda gani kwa sababu mabadiliko huja kutokana na hali halisi ya wakati huo. Hapo ni ujauzito, baada ya kujifungua pia kuna mabadiliko, kwa kuwa wakati huu mke huweka attention yake yote kwa mtoto, so mume unakuwa second priority. Hii ni akina mama wote, exceptions chache zipo. So, mwanaume unatakiwa uishi na mke kwa akili. Jifunze yale ambayo ukuyafahamu kabla ya ndoa.

Mabadiliko ambayo hayatokani na ujauzito hicho ni kitu kingine. So, mwambie avumilie na afahamu kuwa hiyo ni hali ya kawaida na anatakiwa kuwa more supportive than before.
hapo nimejikuta napata sababu ya mapungufu kiasi niliyoyanotes kwangu, wakuu mpo juu sana. naamini wengi tuna nufaika na haya hata kama sio leo basi kesho yatusaidie jamani.
 
hapo nimejikuta napata sababu ya mapungufu kiasi niliyoyanotes kwangu, wakuu mpo juu sana. naamini wengi tuna nufaika na haya hata kama sio leo basi kesho yatusaidie jamani.

Mkuu ni ngumu kutabiri tabia za mwanamke mjamzito....
Muhimu ni kuwa tayari kwa lolote....
Kuna wengine hawataki kukuona....ila pia hawataki utoke nyumbani....yaani uwe karibu ila asikuone....
 
Mkuu ni ngumu kutabiri tabia za mwanamke mjamzito....
Muhimu ni kuwa tayari kwa lolote....
Kuna wengine hawataki kukuona....ila pia hawataki utoke nyumbani....yaani uwe karibu ila asikuone....

dah sio mchezo. inahitaji uelewa wa hali ya juu, sasa mimi najiuliza hivi kule kwetu kwenye mfumo dume mbona wanawake wanakuwa hawana haya au nini haswa. sijawahi sikia mama wa kisukuma anamtuma mmewe kupika au kumjibu dry kisa mjamzito au kunakiasi cha kujifanyisha.
somo nimelielewa ila km binadamu nabaki na maswali kichwani, au ndo beijing hii(gender mainstreaming).
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom