Inaudhi: JK - sijui kwanini Tanzania haina viwanda kama Japani...

let's stop this madness.....and fast!

Let's not even talk abt what JK said or didnt say. It's the best his 'IQ' (oh yeah?) could cultivate!

Let's not try re-invent the wheel either.

Let's just revisit history...why during Mwl JKN it was possible to create and construct industries (which have now, sadly,been converted into mere godowns by the thiefing so called traders of Asian origin)?

What and where it has gone wrong along the TZ industrialization history path?
 
Akitembelea Wizara ya Viwanda na biashara,JK ameendelea kutoa kauli zake zenye mzaha na kutia hasira aliposema ati hajui kwanini Tanzania yenye maliasili mbalimbali zenye kufaha kutumika kama malighafi kwenye viwanda haina viwanda hivyo,aliendelea kusema Japan na Indonesia hazina malighafi lakini wana viwanda sijui Tanzania kwanini haina viwanda...Kauli hii inanikumbusha kauli zifuatazo ambazo haliwai kuzitoa huko nyuma;

  1. Sijua kwanini watanzania ni maskini...
  2. Siwajui wamiliki wa Dowans...na sitaki kuwafahamu..
Nadhani JK anaendelea na mzaha uleule wa kila siku....Inakera!!!!!

source:Channel Ten News Bulletin


Hayo ndiyo matunda ya kuchagua rais mswahili.
 
Ni kweli inakera! lakini ebu tumsaidie sasa basi maana huwenda yeye kweli anaumiza kichwa lakini hapati majibu......kuna wasomi wengi sana tunahitaji michango yao sababu Tanzania haitajengwa na JK pekee. JK kuwa rais haimaanishi kuwa yeye ndie mwenye akili kuliko wote nchini. Wasomi tuache ubinafsi sasa tusaidie nchi yetu. Wajenga nchi ni wananchi!

Kwanza hata CDM wamwamshe/wamsaidie vipi ama mtu yeyote amsaidie vipi JK hawezi kuelewa kwa kua amelewa madaraka na kushika dola TZ imekua rahisi tu kwa CCM na yeye mwenyewe.

Pili Raisi JK na timu yake (mawaziri, wakuu wa mikoa/wilaya/tarafa/mameya, na viongozi mbalimbali ktk CCM, nk) wakae na waongelee hili jambo (CCM hawajaongelea hili jambo muda wote huu?), sasa kama TIMU nzima hawajui cha kufanya ama cha kumsadia RAISI JK na wote JK included, wamebaki kurandaranda tu na maVX huku wakiunguza pesa yetu bila huruma tunaomba wajiuzulu uongozi. CHAMA kingine na RAISI mwingine anaweza kua na uwezo wa kujua cha kufanya. Kikwete na CCM yao ilibidi wajue cha kufanya hata kabla hawajaamua kukwapua ama kuomba kushika dola. Kama ni kweli JK kaongea hivyo mimi naona ni dharau zake kwa wananchi, alipewa? nchi kwa ahadi zake leo anatuambia hajui cha kufanya AU LABDA NI LUGHA YETU YA KISWAHILI AMA MILA ZETU NI NGUMU KUZIELEWA KIASI KWAMBA HATUMWELEWI ANAMAANISHA NINI.

Tatu JK kama anapenda viwanda kweli, inabidi achague kati ya maVX, maEPA/DOWANS na VIWANDA. Huwezi kuchanganya vyote halafu ategemee na viwanda viwepo.
 
Akitembelea Wizara ya Viwanda na biashara,JK ameendelea kutoa kauli zake zenye mzaha na kutia hasira aliposema ati hajui kwanini Tanzania yenye maliasili mbalimbali zenye kufaha kutumika kama malighafi kwenye viwanda haina viwanda hivyo,aliendelea kusema Japan na Indonesia hazina malighafi lakini wana viwanda sijui Tanzania kwanini haina viwanda...Kauli hii inanikumbusha kauli zifuatazo ambazo haliwai kuzitoa huko nyuma;

  1. Sijua kwanini watanzania ni maskini...
  2. Siwajui wamiliki wa Dowans...na sitaki kuwafahamu..
Nadhani JK anaendelea na mzaha uleule wa kila siku....Inakera!!!!!

source:Channel Ten News Bulletin
3. mkuu usisahau wanafunzi kupata Mimba nikiherehere chao!
 
NURFUS:
Wewe unaonekana umeguswa sana na nchi hii. Sasa, nini mchango au maoni yako katika hili kama mtanzania? Mchango hata wa sentensi mbili tu? Kulalamika peke yake hakutoshi. If you dont like something change it, if you cant change it, stop complaining. So give us your two cents on this?? Please?
Achangie kwanani!?? hawawatu hawasikilizi hata mala moja, Kunamwalimu anaproposal yake ya jinsi ya kupunguza foleni kaipeleka kwenye tasisi zoote husika hakuna mtu aliyemsikiliza zaidi ya kumwambia NI NZURI, na kwasasa anatembea nayo kwenye vyombo vya habari tuuu wanasiasa hawapendi professionals hata kidogo. wao wanajua kilakitu. ndo matokeo yake hayo!
 
Swali hilo kweli kwa mfumo huu wa kitanzania hata mimi ningeuliza kama ningekua age mate wake,lakini kama mzee ruksa alivyopata kusema kila dhama na vitabu vyake, kwa dhama zangu jibu lake ni jepesi sana, na utekelezaji wake ni simple just uamuzi.Ili kutoka huko asikukopenda yeye inabidi Mheshimiwa akubali kuchukua uamuzi mmoja kati ya njia mbili alizonazo.Kukubali lawama ya muda mfupi nikimaanisha miaka 15-20 au kuacha legacy ya generation to generation.

Maamuzi yake ya kuchukua upande wa kuacha LEGACY ni very painfull kwa wale wote waliokaribu na yeye WASIOJIULIZA swali hilo ANALOJIULIZA YEYE,na kwa watanzania wote wasiopenda maendeleo ya Taifa hili na haswa wasiopenda maendeleo ya Jirani zao, rafiki zao, ndugu zao, classmate zao, workmate zao wanaotafuta maendeleo yao kwa njia halali.
Moja ya tone dogo sana ya gharama za kuchagua uamuzi wa kuacha LEGACY kwa watanzania na kizazi chake ni maamuzi ya Kutumia Wasaidizi kama Mh Magufuri, Sita nk. I believe Nyerere Legacy yake is forever ingawa imemcost as an indivisual person, lakini leo hii hata mtoto aliyezaliwa baada ya kifo chake anamjua as if amemuona. Na kwa Kua aliasisi ujamaa kama mfumo wa kuishi [Social] nchi hii aiwezi kukwepa kwa namna yoyote hile its the spirit, what goes around comes around.

Tuishi Kijamaa [Namaanisha Socially not Econmically] tuendeshe uchumi kwa mfumo wetu wenyewe tunaona tukizinga na kuangalia mazingira yetu, muda, jamii, nyakati, external force ambazo tunaona tunaweza kuadapt kwa faida yetu, sio kwa style ya kucopy na kupaste.Ikibidi kusema No tuseme No kwa yoyote yule kwa kulinda maslahi ya watanzania kwanza.

Msingi wa nyumba ndio uhalisia wa nyumba yenyewe,Baba wa Taifa alishajenga msingi huo pls pls pls pls as nature works, naamini kuna nature, haiwezikana kwenda nje ya uzio huo [Ndio kinachotusumbua japo viongozi wengi nahisi hawakiamini hiki].Alifanya makosa yake as any human being [Cost for Lecacy]. lakini leo maamuzi yake majority wanayatumia kama dira ya kutafuta mwelekeo. Na majority wanaamini leo hii maamuzi yake yamekuwa faida kubwa kwao, and that is the leadership, ikimaaanisha kuonyesha njia kwa kundi kubwa lisilokua na jibu sahihi ya mwelekeo wa kwenda kwenye maendeleo ya kuanzia mtu binafsi, familia, jamii na Taifa kwa Ujumla.

Naikumbuka hotuba yake moja kua vizazi visije vikachapa viboko makaburi vikihoji maamuzi waliyoyafanya huko nyuma,ni kweli vitafanya hivyo kama atoamua sasa kwa gharama yake [Individual Cost]. Ni uamuzi wa kujibu point ya mwisho ya nafsi thats the inner soul decision what pushed him to run for presidency of almost 43 Million peoples. Kukumbatia majority ndio dira na mgawanyo haki wa keki ya taifa ukizingatia watanzania walio wengi ndio kiu kubwa ya generation hii na ijayo.

Nature imezungumza nchi za kiarabu, japo viongozi wetu wengi wanaona kama cinema, kupuuza sauti ya wengi ni kumchukiza Mungu.

Kwa kuanzia ajitoe mhanga ziara nchi nzima tena za kustukiza bila kuwaambia wasaidizi wake , akusanye wazee kila mkoa, wilaya, kijiji hata kata, asiwe muongeaji bali awasikilize wao tena bila kuangalia itikadi, akusanye makundi ya kijamii kama NGO, Vijana, Wanafunzi, Wakulima, Wafanyakazi, Wafanyabishara n.k awasikilize kwa kuwapa uhuru kujieleza. Ajipangie yeye nani wa kuwaona asiache wampangie watamchakachulia mwisho ataishi kupata maoni yasiyo na tija. Hatakayoyasikia huko yatakua majibu ya swali lake.

Kuuzulia mijadala ya kijamii kama leo pale chuo kikuu Mjadala wa Katiba,na kua msikilizaji mzuri pasi kuongea chochote,kwenye kusikiliza majibu mazuri ya utatuzi wa mambo magumu ya kibinadamu upatikana hapo.Kuongeza kasi ya kuonyesha kujishusha chini na kuwaludia wananchi wa kawaida. Mwalimu alicheza bao na watu wa kawaida lakini bao hilo lilitumika pia kupata ukweli wa hali halisi ya maisha ya kawaida ya mtanzania.


Mwisho wadau wake wa karibu wasio upande wa Swali lake analojiuliza watajua amewasaliti, na dhambi ya usaliti ni kubwa na ina gharama yake. hivyo ni kuchagua kusimama kwa wadau wa karibu au kusimama kwa majorirty ambao pia wana uwezo wa kukulinda na kutetea kwa maamuzi uliyofanya kwa faida yao, [Nyerere Vs Kambona]. Judgement ya uamuzi wake leo inaweza isionyeshe faida ya wazi lakini miaka kumi na tano ijayo watu watasimama kushangilia maamuzi hayo na generation inayokuja.

Tupende tusipende hata kama tutakumbatia ustaarabu wa kimagharibi bado tutaitaji kuishi kijamaa kama waafrika kumthamini biandamu na utu wake.Na ndio Dira ya mwalimu aliyokua akiipigania.



Hata wakati mwingine kuongea face to face na mtu na ambae anaonekana kukuchallange wakati wote,
 
Akitembelea Wizara ya Viwanda na biashara,JK ameendelea kutoa kauli zake zenye mzaha na kutia hasira aliposema ati hajui kwanini Tanzania yenye maliasili mbalimbali zenye kufaha kutumika kama malighafi kwenye viwanda haina viwanda hivyo,aliendelea kusema Japan na Indonesia hazina malighafi lakini wana viwanda sijui Tanzania kwanini haina viwanda...Kauli hii inanikumbusha kauli zifuatazo ambazo haliwai kuzitoa huko nyuma;

  1. Sijua kwanini watanzania ni maskini...
  2. Siwajui wamiliki wa Dowans...na sitaki kuwafahamu..
Nadhani JK anaendelea na mzaha uleule wa kila siku....Inakera!!!!!

source:Channel Ten News Bulletin

nimze wakuagiza 2005 alizungukia kalibukirawizara nakutowa maagizokibao hadialiwazungukia maabusu reo tena anaanzakuagiza badara yakuwawajibisha wazembe hizi ziara ni ufujajiwakodi zetu ziarahizihazina tija kwetu tunaka kutenda sikuraramika
 
Kikwete is a big joke. CCM is a big joke. Tanzanians who voted for JK and CCM are also a big joke.
 
Achangie kwanani!?? hawawatu hawasikilizi hata mala moja, Kunamwalimu anaproposal yake ya jinsi ya kupunguza foleni kaipeleka kwenye tasisi zoote husika hakuna mtu aliyemsikiliza zaidi ya kumwambia NI NZURI, na kwasasa anatembea nayo kwenye vyombo vya habari tuuu wanasiasa
hawapendi professionals hata kidogo. wao wanajua kilakitu. ndo matokeo yake hayo!
<br />
<br />
Mi kuna jamaa yangu mtanzania anayeishi uk,alikuja na propasal ya mpango wa kuboresha elimu ndani ya tz..akaenda sehemu zote husika akapewa jibu kama hilo kwamba ni nzuri..jamaa akaipeleka kwa kagame,wakaipokea kwa mikono miwili na malipo juu
 
We simply don't have industrialization strategy, the so called industrialized countries like Japan industrialization passed through various stages but the most important thing is that they invested heavily on Research and Development (R&D). Our institutions entrusted with R&D during Mwalimu's time don't get enough fund due to lack of recognition of their importance by our govt ,as a result we have remained only with deteriorated buildings.

It should be taken into account that R&D should not only be left to govt, various companies and corporations should should assume their role as well. In contrast our companies do not invest in this area with the aim of improving their productivity, as a result they have remained dependent of outside technology which leads to reduced productivity and ultimately remaining stalemate.

I should end up by suggesting that industrialization needs a foresighted leadership and in poor countries the govt has a greater role to play, but technocrat should be given a chance to lead instead of politician whose main focus is to remain in power enjoy privileges at the expense of our future generation.
 
:bored:

Kimsingi ni aibu kubwa sana Rais anapotoa majibu ya "SIJUI" mbele ya wananchi wake


Wale puppetts wake humu JF mumwambie ajifunze kutokutumia neno hilo maana ni aibu kubwa kwake na mpaka sasa tutamkumbuka kwa neno lake la "SIJUI".... bora "RUKSA" kuliko huyu "SIJUI"..........Ari yake, kasi yake na nguvu zake katika "KUTOKUJUA" mambo ya msingi imezidi kuongezeka na sasa inatisha zaidi


Anapaswa ajiulize yeye kama mkuu wa nchi ambae state machinery zote za kuendesha na ku-control uchumi na naynaja nyingine zaiko mikononi mwake "HAJUI" kila kitu ni nani atakaejua?


Aaaah!!! natokwa pove mdomoni kwa kuongea na sikio lisilosikia dawa..........Mwambienio asiendelee "KUJUA" ili atuachie kumbukumbu ya "KUTOKUJUA"....................KILAZAAAAAAAA!!!!!!
 
Jk wakati ndio huu kawachukue wataalamu wajepu kabla hawajakufa kwa Tsunami na kuwapa uraia watz watakusaidia hilo tatizo lako
 
nimze wakuagiza 2005 alizungukia kalibukirawizara nakutowa maagizokibao hadialiwazungukia maabusu reo tena anaanzakuagiza badara yakuwawajibisha wazembe hizi ziara ni ufujajiwakodi zetu ziarahizihazina tija kwetu tunaka kutenda sikuraramika
Great thinker? I don't think so.
 
Are you serious about this post??Kwa hiyo kwa nini aligombea kuwa rais kama hajui matatizo ya Watanzania?Grow up na sio kutoa posts za kipumbavu.You are proving to be thinking like JK.AND THAT IS AN INSULT,AM SERIOUS ABOUT IT!\kwa hiyo unaona anayosema JK ni sahihi na uoga wake kwa mafisadi ni sawa kabisa?Nyie ndio wa kukataliwa kwenye nchi yetu.Na utakuta wewe ni mtu mzima tu mwenye kazi ya kuhitaji kufanya maamuzi magumu....Amazing!
Kousta or whatever your name is, I really do not have time to argue with you. We are absolutely way two different people here. One of us is pretty obnoxious and repugnant.
 
Wakati fulani huko nyuma Kuna kipindi kimoja cha Jenerali Ulimwengu - on Monday walionyesha mahojiano ya kijana mmoja aliye kuwa mbunifu. Huyo kijana aliweza kubuni namna ya kuzima/kuwasha taa nyumbani wakati ukiwa mbali na nyumbani, na alionyesha kwa vitendo hapo studio.

Pia nimewahi kuwasikia watanzania wengi wabunifu wenye mwelekeo hata wa kugundua mitambo mbalimbali na hata kuunda silaha. Matarajio yangu kuwa watu kama hawa wangeendelezwa na tungekuwa na wataalam wa hali ya juu tena wazalendo badala ya kuagiza wataalam au mitambo toka nje. Badala yake tumeelekeza nguvu kwa kuunda vikundi vya uchuuzi - sijui mnaita SACCOS ambavyo siyo endelevu kwa taifa hili ambalo si maskini kama wanasiasa wetu na pengine wengi wetu tunataka kuamini na kupunguza ari na juhudi ya kuzalisha.

Tunataka tufanane na mataifa mengine eti kwa nadharia hilo halitawezekana.... we need to be productive...everybody should be productive.... na hapo hali ya maisha itakuwa njema kwa kila mtanzania.

Nimechunguza sana kwa muda mrefu watanzania walio wengi wanatamani kuchuma kwa kupitia kufisadi kila aina ya pesa inayopitia mikoni mwao, na watu hao nimeona jamii ikiwasifia kuwa eti ni wajanja. sasa ufisadi upo tangu level ya chini kabisa (mtendaji wa kijiji na wengineo) hadi ngazi ya juu kabisa. Wanachotofautiana ni kiasi cha kuchota tuu.... na hii ndiyo sababu kubwa ya nchi hii kuwa maskini na wala haihitaji utafiti wa REPOA kama PM anavyo taka tuamini au anavyojaribu kushangaa kwanini wasomi wengi hawataki kujiajiri kwenye kilimo na mifugo.

Wasomi hawa ambao wengi wao tumewashudia mashuleni wakidhihirisha ubunifu na akili za hali ya juu mashuleni hadi vyuoni wangetafutiwa fursa kwa dhati za kuendelezwa akili zao hizo, VIWANDA VINGEKUWEPO NA MASHA BORA KWA KILA MTANZANIA INGEWEZEKANA KATIKA UHALISIA WAKE na sii katika kutafutia kura za watanzania wakati wa uchaguzi.

Hivyo ndo tunamshauri Raisi wetu na wanzake na kama atataka zaidi kutoka kwangu anijulishe tu nitampa zaidi....

na hii pia ni kwa wale wote wanaotaka tutoe ushauri na siyo kulalalamika......

Ninayo mengi ila kwa sasa na kwa leo chukueni hayo machache....
 
Only83, hivi kama Tanzania JK anakuudhi kwa kuwa Tanzania haina viwanda kama Japan, kwa nini wewe usianze kuunda japo kiji kiwanda kama huwezi Kiwanda? Au option nyingine ni kuhamia Japan.
 
Kwa umeme upi?
Nini Japan, Knya tu wanatushinda.
wakikaa kuzungumzia East Africa mfano wao mkubwa utasikia AZAM. Upuuuuuuuuzzzzzzzzzzziiiiiii MTUPPUUUUUUU!!!!!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom