Inatosha - Lowassa Jiuzulu!

RA ni mfanyabishara kama wafanyabiashara wote duniani yeye kazi yake ni kukusanya mapesa na anapopata mwanya basi anautumia ule mwanya ipasavyo

tatizo ni viongozi wetu wanapotaka kula wanawatafuta hawa watu wenye asili ya ki asia au light skin ppl na kuwapa hizo mianya ya kuiba.

wapi umeona kiongozi wetu weusi akatoa mwanya au kula kwa mweusi mwenzake?..nil..hii ni kasumba yetu weusi tunaposhirikiana na hawa watu(weupe)tunaona ni kama ka status....ndo maana dada zetu wanatumia mkorogo ili kupata hiyo ngozi

Mwanatanu,
Heshima, utukufu na enzi iwe kwake aliye juu,

Nakubaliana nawe kwa sehemu kubwa ya ujumbe wako isipokuwa sehemu ndogo tu, ya mwisho.

Hasa EL hamhusishi Mweusi katika biashara yoyote; iwe halali au halamu. Na Mdanganyika mweusi ukipeleka Clean Business Idea or Opportunity kwa EL umeliwa. Atafanya mwenyewe na Wahindi.

Hebu angalia Leopard Tours. Front desk na management nzima ni wahindi. Kwa macho ya haraka utafikiri kampuni ya Wahindi kumbe kitegauchumi cha EL.

Kuna utani kuwa, jinsi EL anavyowahusudu weupe, siku moja alimsindikiza JK saloon kuweka "yale mambo yetu yale" Walipofika JK akamshawishi naye aweke asionekane umri unapiga kasi. Kwa kuwa EL anahusudu sana weupe akamwambia mie waniwekee ya kuongeza weupe kichwani niwe kama mzungu na kama utaniruhu nita-cream
 
Binafsi naipongeza sana Kamati teule hasa Mwenyekiti Dk. Mwakyembe na naibu wake yule mama kwa ujasiri mkubwa na upeo uliotukuka kwa kuwaambia mafisadi ndani ya CCM yao "enough was enough" Guess what If was me Dr. Mwakyembe would be my new Prime Minister period, because he has showed everybody that he can dare talking openely.
 
BREAKING NEWS!!!

LOWASA KAJIUZULU....Na Spika kaahisiha kikao cha Bunge mpaka saa 11 jioni
 
Haya madukuduku mengine yaje maana mtu mzima kabwaga manyanga kupisha wadau waijadili Hoja..Sasa ni kweli huyo Tyson anaweza kuchukua nafasi ya EL??
 
Can I quote myself...

Mkakati ambao umepangwa hadi hivi sasa na wale mnaoamka nyumbani mtauona kwenye maandishi madogo madogo chini ya vichwa vikubwa vya habari ni ule wa kudai kuwa hawakupewa nafasi ya kujitetea au kusikilizwa.

Mkakati huu utatumiwa na Lowassa (ambaye inadaiwa anajiandaa kujibu mapigo - he won't go down without a fight) na pia ni mkakati ambao Karamagi na Msabaha nao wanataka kuutumia. Kimsingi wanadai wanatuhumiwa bila kupewa nafasi ya kusikilizwa wakati Karamagi anadai ripoti hiyo ni ya "kisiasa".

Hata hivyo tatizo la mkakati huu ni kushindwa kuelewa Kamati licha ya kuwa na nguvu za kimahakama siyo mahakama. Hivyo badala ya kuleta mashahidi wa upande wa mashtaka na upande wa utetezi (kama ilivyo mahakamani)ni Kamati inaamua nani aitwe na nani asiitwe na kwanini.

Mojawapo ya tetesi ambazo zinasikika sana ni kuwa RA aliitwa na akakataa. Sijui hilo lina ukweli kiasi gani. Hata hivyo kama Lowassa, Msabaha, Karamagi na waliotajwa wengine hawakupewa nafasi ya kusikilizwa au kuitwa kutoa maelezo kunaweza kusababisha hisia hiyo ya "uonevu" kwani its against the natural justice.

Hii natural justice (haki ya asili) inaonekana katika maandiko yote ya Kikristu na Kiislamu ambapo licha ya Mungu kujua Adam amekosea lakini bado alimpa nafasi ya kujieleza. Hivyo, kati ya dondoo ambazo zitakuwa muhimu sana kujulikana ni kujua nani aliitwa na nani hakuitwa na kwanini. Kuna kipengele kimoja mwanzoni mwa ripoti kinachoashiria (angalau kwa upande wangu) kuwa wote walioitwa kwa summons (subpoena kwa wenzetu US)walienda.

Lakini hapa kuna mtego ambao Mkakati wa kina Lowassa utakwama. Kama mnakumbuka Mwakyembe alitoa wito kwa "mtu yeyote" mwenye maelezo kuhusu Richmond ajitokeze na kuonana na Kamati. Kwenye ripoti hiyo anasema hakuna mtu aliyejitokeza kwa hiari yake (hapa anawabana kina Karamagi, et al).

HIvyo wakija na "hatukupewa nafasi ya kusikilizwa" Mwakyemba atawaambia.. "tarehe... nilizungumza na vyombo vya habari na kutoa wito kwa "mtu yeyote"... hapo ndipo watakapojua kuwa mtego umetegwa aidha watautegua, ama watanaswa!

Usikose kusikiliza maoni yangu kwenye KLH News kuhusu suala hili.

I'm out.. enough excitement for the day!
 
  1. Kumbe Lowasa alimaliza tembo mzima halafu akatuambia watanzania tugawane kasungura; dah, mshenzi kweli jamaa huyu.
  2. Kama Rais huyu alipinga kujiuzulu kwa Ballali na baadaye akatangaza kumfukuza kazi, ninategemea atafanya vivyo hivyo safari hii kwa Lowassa, Kalamagi na Msabaha.
  3. Ndege ya Lowassa imepata pancha huko angani.
  4. Watu wate waliohusika na upotevu wa mamilioni ya pesa za umma wasiishie kufukuzwa kazi tu na kuachiwa waendelee kudumbua walichoiba, lazima wachukuliwe hatua za kisheria ili siyo tu warudishe walichoiba bali pia waweze kutumikia vifungo vya muda mrefu jela na kufanyishwa kazi za suluba.
  5. Matokeo ya tume ya Mwakyembe yanaonyesha kuwa TAKUKURU haifanyi kazi zake ipasavyo. Ni matumaini yangu kuwa Rais ameliona hilo na atamchukulia hatua kali pia Mkurugenzi wa TAKUKURU kwa kulidanganya taifa kuwa taratibu za utoaji wa tenda hiyo hazikukiuka sheria yoyote na wala hakukuwa na shinikizo la rushwa.
 
Jamaa hana huruma kabisa, pamoja na kujua kuwa kasungura kenyewe kadogo lakini yeye aliamua kutesa kwa kwenda mbele.
 
Unajua alipozungumza alisema lile la "natural justice" nililoandika hapo nyuma nadhani tuna special mis-connection...
 
sasa Lowassa alijua kuhusu Richmond, kwa hiyo naye JK pia aliyajua yote haya. JK jiuzulu. uchaguzi uanze upya. watu wanakufa njaa,barabara mbovu, bunge litaifishwe
 
Mimi mpaka sasa nikilala usiku huwa naweweseka maana siamini ETI WAZIRI MKUU WA NCHI NI MWIZI?!!!!TENA MKUBWA?!!!!
 
Sasa naanza kuamini kuwa kuna watu tena Watanzania ambao walishiriki kikamilifu kumpeleka nyerere kaburini il wapate mwanya wa kuiba yaani ETI HATA RAIS WETU MSTAAFU ALIKUWA MWIZI MKUBWA NA NDIYO MAANA AKINA ZOMBE NA WENGINE, WAO WALIAMUA KUIBA KWA MTUTU WA BUNDUKI KABISA!!! MAANA SASA WANGEMUOGOPA NANI KAMA BABA YAO MKUBWA KABISA NI MWIZI NAMBA MOJA
 
Mimi Niliamini Ya Kuwa Urais Ni Heshima Kumbe Nilikuwa Najidanganya!!!
 
Yaani Raisi Mstaafu Alikuwa Mwizi.!!!yaani Alifanya Ujambazi Wa Kutisha Ikulu?mbona Nilifundishwa Zamani Ya Kuwa Ikulu Ni Mahala Patakatifu Au Nilidanganywa Ina Maana Machozi Yote Aliyoyatoa Alipokufa Nyerere Yalikuwa Ya Kinafiki?!!sasa Mungu Akae Tanzania Akisubiri Nini?
 
Ila Nyerere Alisema Kabla Ya Kufa Ya Kuwa Lowasa Ni Mwizi Mkubwa Ina Maana Hayo Maneno Ya Nyerere Mliyasahau?
 
Mimi Nasema Uwe Kiongozi Serikalini,uwe Mfanyabiashara Uwe Mkulima Uwe Kiongozi Wa Dini,tambua Ya Kwamba Sheria Za Kuishi Kwa Kitu Au Binadamu Yeyote Hapa Duniani Zilikwishawekwa Na Muumba Tena Hata Kabla Ya Akina Madabii Musa, Yesu, Mtume Muhamad. Hivyo Chochote Kitakachofanyika Kinyume Na Ilivyo Kwa Mungu Ni Ubatili Na Haijali Ni Nafasi Gani Uliyonayo Hapa Duniani. Na Kwa Kuthibitisha Hayo Mungu Huwa Anatoaga Mifano Hai Ili Mjue Ya Kuwa Yupo.mfano Mabutu Wa Zaire Yuko Wapi,je Sasa Hivi Unaweza Kuamini Ya Kuwa Thamani Ya Balal Wa Bot Ukilinganisha Na Ya Matonya Omba Omba Matonya Yuko Juu?!!je Unaweza Kuamini Ya Kuwa Thamani Ya Lowasa Kwa Sasa Hivi Ukilinganisha Na Ya Mbwa, Mbwa Yuko Juu? Basi Na Mtambue Ya Kuwa Kwa Mungu Hakuna Mshindi Na Kwake Kila Goti Ni Lazima Litapigwa
 
Mimi mpaka sasa nikilala usiku huwa naweweseka maana siamini ETI WAZIRI MKUU WA NCHI NI MWIZI?!!!!TENA MKUBWA?!!!!

kwanini ulishabikia Wakati Jk akiomba kura,Mie ni Mwana CCM il sikumchagua Muungwana. sababu Mwalimu hakupendezwa naye kwa yeye kushirikiana na Lowassa,ila Nilisherehekea alipoanguka Mara ya Pili sababu siyo chaguo La Mungu.

Sasa naanza kuamini kuwa kuna watu tena Watanzania ambao walishiriki kikamilifu kumpeleka nyerere kaburini il wapate mwanya wa kuiba yaani ETI HATA RAIS WETU MSTAAFU ALIKUWA MWIZI MKUBWA NA NDIYO MAANA AKINA ZOMBE NA WENGINE, WAO WALIAMUA KUIBA KWA MTUTU WA BUNDUKI KABISA!!! MAANA SASA WANGEMUOGOPA NANI KAMA BABA YAO MKUBWA KABISA NI MWIZI NAMBA MOJA

Unayakumbuka Maneno aliyoyatoa Mzee Ndesamburo?Ni bora kuchagua mtu mwenye Pesa,ila Maskini ni mtu mbaya sana.ataanza kujitajirisha wkanza badala ya kuwatumikia wananchi na huyo ndio mzee mmaching ,Aliyeweza kulinda nidhamu ya chama,MR dirty clean.

Mimi Niliamini Ya Kuwa Urais Ni Heshima Kumbe Nilikuwa Najidanganya!!!

Urais Kwa nchi za Afrika,ni heshima ndio sababu watu wanakuheshimu sana na kukuogopa na baadaye wanakuletea dili chafu na unazipitisha.Unapata hata kupiga Mademu unaotaka bila ya kuhojiwa.

Yaani Raisi Mstaafu Alikuwa Mwizi.!!!yaani Alifanya Ujambazi Wa Kutisha Ikulu?mbona Nilifundishwa Zamani Ya Kuwa Ikulu Ni Mahala Patakatifu Au Nilidanganywa Ina Maana Machozi Yote Aliyoyatoa Alipokufa Nyerere Yalikuwa Ya Kinafiki?!!sasa Mungu Akae Tanzania Akisubiri Nini?

Ndio Ikului ni patakatifu.Tatizo watu wanaopata IKULU si watakatifu..ukimuona mtu anakimbilia ikulu jua...th Late Jk Nyerere
 
Back
Top Bottom