Inatosha - Lowassa Jiuzulu!

I dont want to believe kwamba Lowassa naye katika misamiati ya kiswahili neno Wananionea limo kwenye orodha.

Mimi nilidhani yeye ni mtu liye zaliwa kuonea wengine.

Nilisema mwaka jana kwamba kabla ya uchaguzi wa 2010 tutaona na kusikia mengi.

Kweli Mwosha Huoshwa.

Mtu anaambiwa naye achuchumaye kwenye bafu yetu ya kiswahili aogeshwe anang'aka.
 
MA MODS nao wajiuzulu Hawajui kazi. Wawajibishwe, Hawafai. Wajiuzulu. Kitaeleweka tu

He! We vipi! tayari usha jisahau unadhani JF ni shirika la Umma.

Hiki ni kijiwe binafsi Bro!

Hapendwi mtu sura yake mvi zake wala nini. Inapendwa hoja ya haja tu hapa.

Tena sisi wenye majina yasiyo na Vilemba kama mimi na wewe inabidi tunyamaze kusema sema upuuzi kama huo ulo usema, kwani tunaona ichuzi yetu mali kuliko jamvi tulitumialo kutolea sauti zetu.

Nakuomba bro Usnooze na kupotelea kwenye wembamba wa hoja yako.
 
Ndio maana kila siku mimi nasema Waafrika Ndivyo Tulivyo!! Huyu Lowassa sasa ni zaidi ya muongo mmoja amekuwa akituhumiwa/ kuhusishwa na ufisadi lakini cha kushangaza bado anapewa madaraka serikalini tena ktk nafasi nyeti. Hivi hili kundi la mafisadi waliokubuhu Tanzania lina wangapi? Nina imani kabisa hata elfu mbili hawafiki kwa sababu miaka nenda rudi ni majina hayohayo tunayoyasikia. Kwa kweli inashangaza kuona taifa lenye watu karibu milioni 40 likiwa "pimped" na kikundi cha wafisadi wachache!! Chini ya moyo wangu sitaki kabisa kuamini kwamba kweli sisi Waafrika Ndivyo Tulivyo lakini kwa kutumia kichwa changu na macho yangu ninajikuta sina jinsi zaidi ya kufikiri kuwa labda ni kweli Ndivyo Tulivyo.
 
Ndio maana kila siku mimi nasema Waafrika Ndivyo Tulivyo!! Huyu Lowassa sasa ni zaidi ya muongo mmoja amekuwa akituhumiwa/ kuhusishwa na ufisadi lakini cha kushangaza bado anapewa madaraka serikalini tena ktk nafasi nyeti. Hivi hili kundi la mafisadi waliokubuhu Tanzania lina wangapi? Nina imani kabisa hata elfu mbili hawafiki kwa sababu miaka nenda rudi ni majina hayohayo tunayoyasikia. Kwa kweli inashangaza kuona taifa lenye watu karibu milioni 40 likiwa "pimped" na kikundi cha wafisadi wachache!! Chini ya moyo wangu sitaki kabisa kuamini kwamba kweli sisi Waafrika Ndivyo Tulivyo lakini kwa kutumia kichwa changu na macho yangu ninajikuta sina jinsi zaidi ya kufikiri kuwa labda ni kweli Ndivyo Tulivyo.

NDIO ma MODS hao Ndivyo Walivyo
 
Ndio maana kila siku mimi nasema Waafrika Ndivyo Tulivyo!! Huyu Lowassa sasa ni zaidi ya muongo mmoja amekuwa akituhumiwa/ kuhusishwa na ufisadi lakini cha kushangaza bado anapewa madaraka serikalini tena ktk nafasi nyeti. Hivi hili kundi la mafisadi waliokubuhu Tanzania lina wangapi? Nina imani kabisa hata elfu mbili hawafiki kwa sababu miaka nenda rudi ni majina hayohayo tunayoyasikia. Kwa kweli inashangaza kuona taifa lenye watu karibu milioni 40 likiwa "pimped" na kikundi cha wafisadi wachache!! Chini ya moyo wangu sitaki kabisa kuamini kwamba kweli sisi Waafrika Ndivyo Tulivyo lakini kwa kutumia kichwa changu na macho yangu ninajikuta sina jinsi zaidi ya kufikiri kuwa labda ni kweli Ndivyo Tulivyo.

Ni kweli hilo tatizo waafrika tunalo weakness yetu kubwa ni ubinafsi,hatuna sense of patriotism...kula kupo duniani kote lakin wenzentu wanafnya kazi na kuawaacha legacy ya kazi njema lakini sisi Waafrika tunataka tule na tumalize kikapu chote.

Hebu angalia PM,Karamagi,Mramba,na...yaani ni list ndefu..wamejikusanyia mapesa mengi yetu si walala hoi inawatosha kuishi mpaka kufa na vijukuu vyao bila kufanya kazi na bado wanang'ania cheo...na ukiangalia kitu kizuri walichofanya kwa nchi ni zero...inasikitisha ni matapishi matupu..MINGI IBARIKI TZ..hakuna wananchi wapole duniani yaani ni kondooo kama sisi wabongo.
 
Mzee Mwanakijiji

Re: Inatosha - Lowassa Jiuzulu! UCHAMBUZI WA KISIASA

M. M.

RA ameingia Dodoma muda si mrefu uliopita... sijui anatokea wapi...


Mkuu Mwenzangu,

1. the dataz ni kwamba Muungwana, alipelekewa ripoti kwanza nyumbani, akaonywa kuwa kuna watu wake huko ndani ya ripoti, akawaambia waende nayo hataki kuiona isemwe kama ilivyo isiondolewe kitu chochote,

2. Alipowasili Dodoma, Air-Uchumi hakuenda Airport!

stay tuned.....!
 



Mkuu Mwenzangu,

1. the dataz ni kwamba Muungwana, alipelekewa ripoti kwanza nyumbani, akaonywa kuwa kuna watu wake huko ndani ya ripoti, akawaambia waende nayo hataki kuiona isemwe kama ilivyo isiondolewe kitu chochote,


...Damn, EL ataponea wapi sasa na soon hell itamwangukia!
 
Nafikiri unakumbuka kwenye thread yangu nilisema serikali ishinikizwe na ikibidi mawaziri wote watupwe nje!Uozo ni serikali nzima..sio Lowassa peke yake!
 
RA ni mfanyabishara kama wafanyabiashara wote duniani yeye kazi yake ni kukusanya mapesa na anapopata mwanya basi anautumia ule mwanya ipasavyo

tatizo ni viongozi wetu wanapotaka kula wanawatafuta hawa watu wenye asili ya ki asia au light skin ppl na kuwapa hizo mianya ya kuiba.

wapi umeona kiongozi wetu weusi akatoa mwanya au kula kwa mweusi mwenzake?..nil..hii ni kasumba yetu weusi tunaposhirikiana na hawa watu(weupe)tunaona ni kama ka status....ndo maana dada zetu wanatumia mkorogo ili kupata hiyo ngozi
 



Mkuu Mwenzangu,

1. the dataz ni kwamba Muungwana, alipelekewa ripoti kwanza nyumbani, akaonywa kuwa kuna watu wake huko ndani ya ripoti, akawaambia waende nayo hataki kuiona isemwe kama ilivyo isiondolewe kitu chochote,

2. Alipowasili Dodoma, Air-Uchumi hakuenda Airport!

stay tuned.....!


Vipi, walikuwa wanajambiana mashuzi?

Nilisoma sehemu kuwa kuna grupu lilijifungia kwenye chumba fulani cha Bunge kujadiliana namna ya kukabiliana na JK wakati anaingia mjini.
 
Hivi hoja hii inaweza kufikishwa Chamwino kwa Muungwana?

Mzee Dotori, Heshima yako Mkuu!

Ama kweli hizi ni zama mpya za utawala. Kwanza kabisa, binafsi sijawahi kuwa na ndoto kuwa atatokea Mbunge yeyote wa chama chochote kinachotawala nchini Tanzania, kuandika ripoti kama ya Dr. Mwakeyembe ya kuwavua nguo chafu viongozi na kuzianika juani ili zifuliwe. Katiba yetu imewapa watawala wetu madaraka makubwa mno, kiasi kwamba ni jambo la hatari kuanika madhambi yao hadharani. Unahitajika moyo wa kiwendawazimu kutoa ripoti kama hii. Ndio maana kwa dhati ya moyo wangu, nawapongeza wajumbe wote wa kamati teule.

Pili, naunga mkono hoja ya Mzee Mwanakijiji ya kumtaka Waziri Mkuu ajiuzulu. Naungana na Mzee Dotori kuwa hata sisi tunaweza kuonyesha msukumo wetu wa kuiunga mkono kamati teule kwa kupaza sauti zetu kwa matendo. Utaratibu unaotumika mara nyingi kufikisha duku duku za wananchi kwa wahusika ni ule wa kusaini “petition”. Hata hivyo, binafsi nadhani kwamba, kama mianya ya kisheria ndani ya katiba ya Tanzania ingetumiwa ipasavyo, sauti za wananchi zingesikika kwa kishindo kikubwa.

Nadhani hoja ya Mwanakijiji ya kumtaka Waziri Mkuu ajiuzulu ingepewa nguvu mpya na sura mpya katika historia ya nchi yetu. Katiba na sheria za nchi zinaturuhusu sisi wana Jambo Forums, kupitia kwa Mbunge yeyote, kutoa hoja Bungeni ya kumtaka Waziri Mkuu ajiuzulu.

Mfano, kwa mujibu wa ibara ya 21 (1) ya katiba ya Tanzania: “kila raia wa Jamhuri ya Muungano anayo haki ya kushiriki katika shughuli za utawala wa nchi, ama moja kwa moja au kwa kupitia wawakilishi waliochaguliwa na wananchi kwa hiari yao, kwa kuzingatia utaratibu uliowekwa na sheria au kwa mujibu wa sheria”

Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania liliweka kanuni ambazo wananchi ( mfano, Jambo Forums) wanatakiwa kuzifuata ili kutimiza lengo la ibara ya 21 (1) ya katiba ya Tanzania.

Mfano, kanuni mojawapo ni ya 28 fasihi ya (1) ambapo: “Mbunge yeyote aweza kuwasilisha Bungeni maombi yoyote juu ya jambo lolote kwa niaba ya watu wanaotoa ombi hilo, na halitatolewa Bungeni mpaka kwanza taarifa ya ombi hilo iwe imetolewa kwa maandishi na kupokelewa na katibu si chini ya siku mbili za kazi kabla ya Mkutano ambapo ombi hilo linakusudiwa kutolewa”.

Pia, nukuu ya kanuni ya 28 fasihi ya (3): “ Mbunge anayewasilisha ombi atatoa maelezo mafupi ya kutambulisha watu wanaotoa ombi hilo, idadi yao, saini zilizoambatanishwa kwenye ombi hilo, madai ya msingi yaliyomo, na madhumuni ya ombi hilo.”

Tutakuwa tunakosea tukidhani kuwa Waziri Mkuu, atakuwa na busara za kujiwajibisha mwenyewe, au kutarajia kuwa Rais atamwajibisha. Pia tutakuwa tunakosea tukidhani Bunge linaweza kumwajibisha Waziri Mkuu. Lazima tukubali ukweli kuwa wabunge mithiri ya Dr. Mwakyembe ni adimu sana Bungeni. Ndio maana naomba kutoa hoja kwa wana JF ya kuunga mkono hoja ya Mzee Mwanakijiji na wazo la Mzee Dotori.

Lakini tusiishie hapo, bali tutengeneze hoja nzuri na kuziweka katika maandishi. Tujiorodheshe majina yetu na saihi zetu kama kanuni za Bunge zinavyotuagiza. Alafu tumkabidhi Mbunge yeyote ili aisome hiyo hoja Bungeni kwa niaba ya wana JF na kwa mujibu wa katiba ya Tanzania na kanuni za Bunge la Jamhuri ya Muungano.

Lengo la hoja yetu liwe kuliomba Bunge kutumia ibara ya 53 A (1) ya katiba ya Tanzania kupitisha Azimio la kura ya kutokuwa na imani na Waziri Mkuu. Inawezekana azimio lisipitishwe na Bunge, lakini lazima hoja yetu itasomwa ndani ya Bunge kwa sababu tutakuwa tumefuata taratibu zote kwa mujibu wa katiba na kanuni za Bunge ambazo ziko wazi na zinaeleweka.

Tumechoka kulalamikia pembeni au kusemea tumboni. Sio lazima hoja yetu Bungeni ifanikiwe kwa mara ya kwanza, lakini tutakuwa tumetoa ujumbe kwa watawala wetu kuwa hatuna chuki binafsi na kiongozi yeyote, bali tuna chuki na matendo yao yasiyojali maslahi ya taifa letu. Tumeelezwa ndani ya ripoti na kutafakari kuwa chuki za udini, ukabila, na nyinginezo miongoni mwa jamii, zinazopelekea mauaji ya raia wasio na hatia kama ilivyo Kenya, hazipandikizwi na wananchi bali watawala wanaojali maslahi yao binafsi na baadaye zao.

Watawala wa namna hii hawafai kutuongoza kwa sababu wameaminiwa na wananchi lakini wenyewe hawataki kuaminika. Wameheshimiwa na wananchi, lakini wenyewe hawataki kujiheshimu. Tumuunge mkono Mwakyembe kama tulivyomuunga mkono Zitto.

 
Tumuunge mkono Mwakyembe kama tulivyomuunga mkono Zitto.

Kuna kila haja ya wananchi Tanzania nzima kuandaa maandamano, kwanza kuwapongeza wana kamati hiyo ya uchunguzi swala la Richmond na pili kumsisitiza rais achukue hatua zilizopendekezwa!...
 
Kyoma,

Nawe unapotea sana mkuu!. Hoja yako nzuri tumuombe Zitto aratibu shughuli hiyo, sidhani kama kwa sasa utakosa watanzania hata elf kumi kukuunga mkono!

Zitto naomba shughulikia jamaa ajiuzulu!

Asante in advance.
 
Yani ukisoma report unapata some chills,na unajiuliza kama EL na kina Karamagi ni watu ambao walifikiri wako untouchable au labda ni incomptent yao ndio iliwafanya wakatuibia kitoto na kampuni ya briefcase,EL should go ASAP na lazima akajibu mashtaka ya ubadhilifu in the court of law pamoja na kina karamagi,na hao TAKUKURU lazima waende nao maana ni matapeli tuu wanaoshirikiana na mafisadi kutumaliza...report ya BOT najua ndio itakuwa tsunami kama mnabisha subirini na hata wasipoitoa wajanja wataitoa tuu maana watu wamechoka na sasa kila kitu kijulikane kama muungwana alivyosema..toa kama ilivyo na hakuna kubadilisha kitu!
 
Hivi mtu akifukuzwa kazi kama Waziri Mkuu bado anawajibika kupewa heshima na marupurupu ya cheo hiko?
 
Hivi mtu akifukuzwa kazi kama Waziri Mkuu bado anawajibika kupewa heshima na marupurupu ya cheo hiko?

Mchungaji,

Sidhani kama kuna precedent ya hili na ingefaa EL to set the precedent. I think it is (in the words of Dr. Ngasongwa as quoted in the Mwakyembe report) GOOD PRACTISE that is used all over the world to revoke all the aluanses (allowances) and privileges that a former PM is entitled, by law, to receive.
 
Mkakati ambao umepangwa hadi hivi sasa na wale mnaoamka nyumbani mtauona kwenye maandishi madogo madogo chini ya vichwa vikubwa vya habari ni ule wa kudai kuwa hawakupewa nafasi ya kujitetea au kusikilizwa.

Mkakati huu utatumiwa na Lowassa (ambaye inadaiwa anajiandaa kujibu mapigo - he won't go down without a fight) na pia ni mkakati ambao Karamagi na Msabaha nao wanataka kuutumia. Kimsingi wanadai wanatuhumiwa bila kupewa nafasi ya kusikilizwa wakati Karamagi anadai ripoti hiyo ni ya "kisiasa".

Hata hivyo tatizo la mkakati huu ni kushindwa kuelewa Kamati licha ya kuwa na nguvu za kimahakama siyo mahakama. Hivyo badala ya kuleta mashahidi wa upande wa mashtaka na upande wa utetezi (kama ilivyo mahakamani)ni Kamati inaamua nani aitwe na nani asiitwe na kwanini.

Mojawapo ya tetesi ambazo zinasikika sana ni kuwa RA aliitwa na akakataa. Sijui hilo lina ukweli kiasi gani. Hata hivyo kama Lowassa, Msabaha, Karamagi na waliotajwa wengine hawakupewa nafasi ya kusikilizwa au kuitwa kutoa maelezo kunaweza kusababisha hisia hiyo ya "uonevu" kwani its against the natural justice.

Hii natural justice (haki ya asili) inaonekana katika maandiko yote ya Kikristu na Kiislamu ambapo licha ya Mungu kujua Adam amekosea lakini bado alimpa nafasi ya kujieleza. Hivyo, kati ya dondoo ambazo zitakuwa muhimu sana kujulikana ni kujua nani aliitwa na nani hakuitwa na kwanini. Kuna kipengele kimoja mwanzoni mwa ripoti kinachoashiria (angalau kwa upande wangu) kuwa wote walioitwa kwa summons (subpoena kwa wenzetu US)walienda.

Lakini hapa kuna mtego ambao Mkakati wa kina Lowassa utakwama. Kama mnakumbuka Mwakyembe alitoa wito kwa "mtu yeyote" mwenye maelezo kuhusu Richmond ajitokeze na kuonana na Kamati. Kwenye ripoti hiyo anasema hakuna mtu aliyejitokeza kwa hiari yake (hapa anawabana kina Karamagi, et al).

HIvyo wakija na "hatukupewa nafasi ya kusikilizwa" Mwakyemba atawaambia.. "tarehe... nilizungumza na vyombo vya habari na kutoa wito kwa "mtu yeyote"... hapo ndipo watakapojua kuwa mtego umetegwa aidha watautegua, ama watanaswa!

Usikose kusikiliza maoni yangu kwenye KLH News kuhusu suala hili.

I'm out.. enough excitement for the day!
 
Grey Mgonja anakuwa "featuring" kwenye kila ripoti ya ubadhirifu, hivi ni kitu gani kinamfanya asiwajibishwe mpaka sasa? Hivi hili la BOT yeye limempitia kando kweli?
Naomba kueleweshwa, kwa nini ako kazini hadi leo wakati madudu waliyofanya na Balali yanatosha kabisa kumnyang'anya kazi?

Kwenye hili Mgonja alifanya kazi yake... hayo mengine ya BOT etc... Mgonja beba mzigo wako mwenyewe ....

"Kila mtu atauchukuaaaa mzigo wake mwenyewe, na kila mtu atao sababu zake mwenyewe mbele ya UMMA siku hiyo ikifika..."
 
kuna news zinatoka DOM na si za reliable source..inasemekana Msabaha amebeba msalaba na kujiuluzu amekubali full responsibility...na Lowasa majibu yake ni "nilimwamini waziri Msabaha na ametuangusha"....tungojee full report asubuhi....
i hope haitakuwa hivyo MUNGU tusaidie
 
Back
Top Bottom