Madela nimekusikia!! Ila ujumbe unaopenyezwa toka kwenye mkutano (bado unaendelea) ni kuwa EL amewagomea kujiuzulu kwani "hana sababu ya kujiuzulu" na kama nilivyosema jana, jiandaeni kwa hotuba ya kuomba radhi na defiance!
Hata hivyo, tetesi ambazo zinaingia taratibu kama mnyoo ardhini zinaonesha kuwa Mawaziri wawili tayari wameandika barua za kujiuzulu... na mida yoyote kuanzia sasa tutajua who is out first..
Kujiuzulu kwa Karamagi na Msabaha (ndicho ninachotegemea kusikia) ni long overdue. Watu tumelalamika hapa siku kibao posts zimejaza mamia ya kurasa! Dr Msabaha kwa kweli namsikitikia, lakini najiuliza nini kilimkosesha uzalendo wa kutamka ule ukweli wa lile neno lake la kizaramo (nikumbusheni!) ili Lowassa ahojiwe na Kamati? Kweli ni mbuzi wa kafara, lakini kafara haramu! Yaani anaona bora atemeshwe mzigo kuliko kumtaja mwizi? Hii tabia wanayo vibaka wazoefu, ukiwaona vibaka watatu wanaiba ukafanikiwa kukamata wawili, kamwe hawamtaji mwenzao hata wakiambiwa wanachinjwa! Sasa huu si ushujaa, ni ukibaka tu! Nitamsifu Msabaha kama atamwaga ukweli wote kwenye hiyo barua yake ya kujiuzulu, better late than never!
Hajiuzulu wala hauzuliwi mtu hapa,CCM ni yetu wenyewe,tutaekana sawa na kuonyana mtu asirudie tena na iwe kosa lake la mwisho,ee mwenye kamaa ajinyonge ,ila sasa ndio wanaingia na kile kilichosemwa ari mpya ,wengine mkae chonjo maana Lowasa akitoka huko ni kama simba aliejeruhiwa wakati bado anautaka mnofu ,lakini kuna kitu kimoja watu wa Mkapa na yeye mwenyewe mbona bado wanapeta ,na yote haya yanayomfika Lowasa na Kikwete ni kumkumbatia Mkapa na kumhifadhi,naamini kabisa Mh.Kikwete ameyarisi haya madudu kutoka kwa Kaka Nkapa ambae ubabaishaji wake wa Ikulu upo wazi alikuwa mkali wa kukemea rushwa kumbe anasanya ,na saikolojia inatwambia mtu akiwa mkali sana basi ujue anaficha jambo !!! Na kweli Mh.Mkapa alikuwa anaficha mambo,baada ya kung'olewa pembe sasa mambo yote yanaonekana wazi kabisa ,kumbe ukali ule ulikuwa unamaana katika elimu ya saikolojia. !!!
These are the moments I wish mchambuzi yuko hapa!!!
These are the moments I wish mchambuzi yuko hapa!!!