Inatisha sana: Jinsi madini yetu yanavyoibiwa kweupe!!!!

Zak Malang

JF-Expert Member
Dec 30, 2008
5,404
233

Wanajamvi: Stori hii kutoka MwanaHalisi ya leo inatisha. Lakini nadhani ndiyo maana CCM huwa haipendi wabunge wapinzani watoke maeneo ya migodi.
Halafu chama kama Chadema kikielezea kitu hiki majukwaani wanaambiwa wanataka kuleta machafuko!

Machafuko my foot!!!!!! Ukimya au ushiriki wa CCM katika masuala haya ndiyo utaleta machafuko!


Usiri hatari migodini

Na Yusuf Aboud, Bukombe

Usiri umegubika migodi nchini. Katika usiri huu, ukweli hauwezi kupatikana. Ni kwenye mgodi wa dhahabu wa Tancan, ndani ya msitu wa hifadhi ya taifa ya Kigosi, kata ya Igulwa, kilomita 80 kusini magharibi mwa makao makuu ya wilaya ya Bukombe, mkoani Shinyanga.

Shuhudia mieleka kati ya diwani wa Chadema na kaimu meneja mkuu wa Tancan inayochimba dhahabu katika kata ya Igulwa:

Diwani Yusuph: Mimi nimefanya kazi kwenye migodi ya dhahabu kwa miaka saba. Mtambo huu (akiugusa) ndio wa mwisho katika usafishaji dhahabu safi. Sasa huwezi kusema hamjaanza uzalishaji.

Meneja Headlam: Ni kweli, huu ndio mtambo wa mwisho katika kuchuja dhahabu; lakini sio kwamba tumeanza uzalishaji. Huu tunautumia tu katika utafiti wetu.

Hiyo ndiyo hali halisi. Wenye mgodi hawakutegemea kufumaniwa na mjuzi. Hii inaonyesha wanafanya watakalo; waweza kuwa tayari wanachimba madini bila serikali kujua.

Lakini kufika kwenye mgodi huo “ndiyo ngoma.” Wiki mbili zilizopita Prof. Kulikoyela Kahigi, mbunge wa Bukombe (Chadema), alijaribu kwenda Tancan.

Alifuatana na madiwani watatu wa chama chake: Yusuph Fungameza wa Uyovu, Patrick Kalugusi wa Namonge na Sudi Ntanyagala wa Igulwa ambako ndiko kwenye mgodi.

Kwenye msafara huo pia kulikuwa na polisi wawili wenye silaha na mwandishi mmoja wa habari.

Kizingiti cha kwanza: Kilomita 25 hivi kutoka barabara kuu, kuingia msitu wea Kigosi, mti umekatwa; umeanguka barabarani na kuziba njia. Inaonekana wazi mti huo umekatwa muda mfupi uliopita.

Dereva anatafuta njia mbadala. Anarudi barabarani ambako kuna makorongo yaliyojaa maji – madimbwi. Kizingiti cha pili.

Kilomita moja kabla ya kufika geti la mgodi, lori linaonekana mbele. Linakuja kwa kasi. Dereva wa msafara wa mbunge anasimama kupisha lori.

Lakini dereva wa lori naye anasimamama kama mita kumi mbele. Baada ya takriban nusu dakika, dereva huyo anaondoa lori lake kwa kasi na kubamiza gari la mbunge kwa upande wa dereva. Kizingiti cha tatu.

Lori hilo la tani 15, mali ya Tancan, lenye namba ya usajili T 207 BJT limebeba kifusi. Linaendeshwa na Mkwisa Olimbaga Mwakibete.

Polisi: Kwanini unatugonga makusudi?

Mkwisa: Gari langu halina breki.

Polisi: Kwanini unaendesha gari lisilokuwa na breki?

Mkwisa: Huku ni porini bwana; breki za nini?

Polisi: Kwani porini ndio unatakiwa uendeshe gari lisilokuwa na breki?

Mkwisa: Maswali yote ya nini? Kwani ninyi mmefuata nini huku?

Mwandishi: Kwani huku watu hawaji?

Mkwisa: (Kimya).

Polisi: Lete leseni yako.

Mkwisa: Sina leseni hapa; iko Mwanza ofisini kwetu.

Polisi: Kwa nini unaendesha gari bila leseni?

Mkwisa: Leseni porini ya nini?Mara wanaingia waendesha pikipiki watano, kila pikipiki ikiwa imebeba watu wawili – wote pamoja 10. Vitisho. Kizingiti cha nne.

Hawa walivaa sare za walinzi wa mgodi, akiwemo aliyejitambulisha kuwa “mkuu wa ulinzi”, Kejo Yoram.

Ndipo dereva Mkwisa akaachia mdomo: Mnatafuta nini huku? Hamnifanyi chochote ninyi. Kama mmekuja kwa shari semeni.

Akitizama waliokuja kwa pikipiki, aliendelea, “Nenda kawaite wote (walinzi) ili tuwaonyeshe. Wamefuata nini huku?” Hakuna aliyeondoka.

Msafara wa mbunge ulikwenda hadi kwenye geti. Hapa ulikutana na Kaimu Meneja Mikuu, Robert Headlam. Alichosema ni kwamba meneja mkuu hayupo naye hawezi kujibu maswali. Kizingiti cha tano.

Hata hivyo, mmoja wa askari wa wanyamapori alininong’oneza kuna eneo jingine zaidi ya tulipokuwa, na kwamba huko kuna wafanyakazi, mahema, magari na uwanja wa ndege. Msafara haukuruhusiwa kwenda huko.

Akijibu swali la Prof kahigi kama wameanza kuchimba dhahabu, Headlam alisema “bado tunafanya uchunguzi.”

“Lakini haiwezekani utafiti ufanyike miaka minane wakati eneo hili kulikuwa na wachimbaji wadogo wakichokonoa dhahabu kwa vijiti na majembe,” alishangaa Prof kahigi.

Naye diwani Sudi Ntanyagala alitaka kujua Watanzania ambao wanashirikiana na mwekezaji kutoka Canada. Lakini meneja Headlam alogoma kutoa maelezo kwa madai kuwa ataingilia masuala ya ofisi kuu aliyosema ipo Mwanza.

Kwa vitisho na vikwazo hivi vya Tancan, usiri unaongezeka na migodi inakuwa sehemu ya nchi nyingine na siyo Tanzania.

0784 447077
unclejay_jongo@yahoo.com





Chanzo: Mwanahalisi ya leo.
 
You made me finish my day sick

Swali la kwanza akili yangu inapata ni "Nani anawapa hawa watu Jeuri?" Who the hell are these people kwenye hii nchi?

Hii haiwezi kuwa jambo la kawaida tu kutazamwa juu juu, lazima jeuri hii iko grounded somewhere...hata askari wa polisi anatunishiwa na kuulizwa maswali ya kipuuzi na "dereva wa lori"?.....what a heck

Kama JK yuko makini badala ya kupita wizarani kutoa maagiozo yale yale ya 2006, huku ndiko kwa kupita na kutoa maagizo....Au kwa udhaifu wake anaogopa nae ataulizwa na walinzi na madereva wa Lori amefuata nini? Au hana sauti kwa hawa wadudu wanaosumbua vichwa vya watanzania??

You have finished this country you cowards!
 
This is a really b. f. country. Inaudhi sana! halafu wako watu kama Profesa mmoja wa uchumi 'aliobobea' anajikita gizani na kuanza kuwaponda CDM kwa sababu wanaumulika uporaji wa aina hii!

Hongera Prof wa ukweli Kahigi (Bukombe MP) kwa kutufumbua macho. Na kwa CDM -- endelezeni Operation Sangara mara moja wananchi wafahamu na hili pia, potelea mbali CCm na 'mawakala njaa' wao waseme wanavyotaka -- kwani mtakuwa mnafanya kitu sahihi kabisa kwa manufaa ya umma, wala hamleti machafuko. CCM wamekwisha kabisa, kilichobakia ni kuwabembeleza mashehe, wanasiasa waliochakarika ili kuwasemea. Hawatashinda!!!
 
This is a really b. f. country. Inaudhi sana! halafu wako watu kama Profesa mmoja wa uchumi 'aliobobea' anajikita gizani na kuanza kuwaponda CDM kwa sababu wanaumulika uporaji wa aina hii!

Hongera Prof wa ukweli Kahigi (Bukombe MP) kwa kutufumbua macho. Na kwa CDM -- endelezeni Operation Sangara mara moja wananchi wafahamu na hili pia, potelea mbali CCm na 'mawakala njaa' wao waseme wanavyotaka -- kwani mtakuwa mnafanya kitu sahihi kabisa kwa manufaa ya umma, wala hamleti machafuko. CCM wamekwisha kabisa, kilichobakia ni kuwabembeleza mashehe, wanasiasa waliochakarika ili kuwasemea. Hawatashinda!!!


Hapo kwene rangi -- Kweli CCM kaput. Ona jinsi wale vijana wa CCM (UVCCM) wa kileo. Hivi hata mmoja pale kwenye uongozi wa juu wa kikao chao Dodoma unaweza kusema ni watoto wa wakulima? Kama ilivyokuwa Tanu Youth League (TYL) ya enzi za Mwalimu? Wengi wa hawa wa sasa ni mafisadi tu, wengine wanamiliki magorofa ya mabilioni.

Sijasikia katika azimio lao likikemea uporaji wa maliasili zetu, bali ni kupeana vijembe tu katika masuala ya ulaji. Shame on them!!!!
 
Aaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaghhhhhhhhhhhhhhhh! Where are the g**s & ar****y jamani amkeni kumekuchaaaaa
 
Hii inchi bwana kuna mambo ya jabu hasa kwenye madini.
Kwanza hawa walinzi na madereva wa kwenye migodi ni watanzania walionunuliwa kwa kupewa mishahara zaidi ya elimu yao. Wengi ni cheap labourers kwa hiyo vijisenti wanavyopata hawawezi kufikiri kabisa kwanga wanaibiwa. Unapewa kiwembe, unaibiwa bati, wapi na wapi?. Kwa hiyo tunahitaji kuelimisha hawa watu na ndo wanaoweza anza kuchoma hayo mamitambo na magari makubwa yanatumika kuiba mali zetu

Pili, hawa wamigodini wanaajiri watu wengi wenye elimu ya chini kama f4 na mwaka juzi walifanyia interview wanafunzi wanafunzi waliomaliza F4 kabla ya matokeo. Wamewadanga wengine wamefaulu vizuri kwenda kukalia hayo mamitambo yao ili mradi wapate cheap labourer. Sasa tunapoteza vijana wazuri kitaaluma kwa sababu ya ushawishi wa hawa jamaaaaa.

Nchi ilishauzwa zamani sana ndo maana wamarekani wapo kimya, Nchi iliyokuwa bado kunuliwa kwa Afrika ni Libya ambayo wameamua kuvamia.

Nasikitika sana watu wanaposhangilia uvamizi wa hawa wezi, wamerakani kule Libya

Kazi tunayo
 
Kweli inasikitisha 'wajinga' ndiyo waliwao hapa namaanisha serikali ya CCM, maana wananchi wa kawaida na CHADEMA tunaona live wizi/ujambazi/uhujumu uchumi huu wa wawekezaji bado wanafanya 'utafiti','uchambuzi yakinifu' aka research??!!!**

Hivi kamati ya nishati na bunge haiwezi kuzuka huko na kujionea 'madudu' haya? au Spika atasema siyo jambo la'dharula'?*** Mawaziri kazi kutembelea miradi ya mjini au Rais kutembelea mawizara jirani na Ikulu ??

Kweli inauma sana kuona 'mwekezaji' kwanza anatuibia, pili ananyanyasa watanzania ikiwemo Mbunge na madiwani walioteuliwa na wananchi!

Nilipata kusoma riwaya ya Andy McNab - ''RECOIL" juu ya majeshi binafsi ya 'wawekezaji' huko Congo DRC, viwanja vya ndege porini/migodini na ndicho kinachotokea Tanzania sasa.

Nadhani kuna haja ya Kamati ya Bunge kutembelea huko ikiongozana na waandishi wa habari tupate kujua zaidi juu ya nchi kufanya kichwa cha mwendawazimu.

Haya wakisema mgodini ni porini sana basi makao makuu ya TANCAN Tanzania yapo jijini Mwanza mkabala na barabarza za Makongoro Rd/ Uhuru st/Nkrumah st . ambapo serikali / kamati ya Bunge inaweza kuzuka ghafla na kudai miadi(appointment) rasmi ya kukagua nyaraka za utafiti na kupanga ziara ya haraka kufika migodini.
 
Ni habari ya kusikitisha, unatamani iwe ni sinema ya uongo na si habari ya ukweli. Hivi ni watanzania wenzetu hawa wanaofanya haya mambo kwa kushirikiana na hawa wawekezaji?
 
Ni hatari sana, na ndio maana ukisikia UTAWALA unasifiwa ujue hao wanaousifia wana maslahi makubwa na UTAWALA huo.
 
Hii nchi inasikitisha kabisa yaani kweli watu wanaiba
madini mchana kweupe huku wakisaiwa na wananchi
wenyewe?
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom