Inatia Uchunguuu Ila ni ukweli mtupu

markdendesi

Member
Sep 7, 2012
45
5
Jamaa mmoja alimfuatilia Mrembo fulani kwa muda mrefu sana na maranyingi akawa anamuomba wafanye mtoko japo mara moja ili waweze kuongea kwa faragha. Kwa bahati mbaya yule mrembo akamwambia Jamaa wawe wanawasiliana kwenye simu na email. Ikawa baada ya muda mrefu wa mawasiliano ya simu na emails, yule mrembo akamwambia jamaa watoke out. Jamaa kwa kufurahia fursa aliyopewa akatafuta kiwanja kizuri sana ambocho kina huduma zote japo ni za gharama kubwa. Siku ikawadia wakakutana na mrembo kwenye eneo la tukio. Wakasalimiana kwa hagi kubwa na tabasamu lenye furaha. Wakanza kupata vinywaji pamoja na chakula. Katika maongezi yule mrembo akamwambia jamaa kwamba amemmisi sana na alikuwa na hamu kubwa ya kukutana na mshikaji huyo. Kwa bahati mbaya jamaa akatafsiri vibaya yale maneno ya yule mrembo. Gafla jamaa akatoka kuelekea toilet na huko huko akaungania kulipia chumba cha kupumzika. Aliporejea kamwambia mrembo nimekuelewa vizuri usipate shida madhali umeshakutana na mimi, nimeshakuandalia chumba kizuri cha kukuenzi. yule mrembo akahamaki manemo ya jamaa, akaanza kumwambia ya kwamba alikuwa anatafuta nafasi ya kumpa jamaa habari njema za ufalme wa Mungu hususani ilivyombaya kufanya ngono (zinaa). Jamaa kwa kuchanganyikiwa na kukosa la kusema akamwambia mrembo, "tukienda chumbani hatutafanya ngono kamwe bali tutafanya mapenzi". Mrembo akamwambia jamaa "shindwa na Ulegee" Jamaa akalegea na kuanguka chini kwa uchungu wa gharama ilizoingia bila mafanikio. Ingekuwa wewe ungefanya nini??????????????????
 
Njooooni tena mje mtiririke

Sent from my BlackBerry 9100 using JamiiForums
 
Bora uamini Mungu yupo uende usimkute kuliko kuamini Mungu hayupo na ukamkuta
 
Shindwa na ulege. Theory bado ipo haha

Sent from my BlackBerry 9860 using JamiiForums
 
Back
Top Bottom