Inatia Huruma kwa Marehemu na Muuaji Pia

Mfumwa

JF-Expert Member
Aug 29, 2008
1,456
42
Ndugu wauana kwa Ugomvi wa kuangalia Luninga


12/26/2008 5:07:48 AM
MFANYAKAZI wa bustani, Innocent Elihuruma [19] wa Mikocheni B, Dar es Salaam amefikishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kinondoni kwa kosa la kumuua ndugu yake Nuru Isack katika ugomvi wa kuangalia luninga.
Inspekta wa polisi Nassoro Sisiwaya aliiambia Mahakama kuwa kosa hilo lilitendeka Desema 19,mwaka huu, nyumbani alipokuwa anafanyia kazi mtuhumiwa eneo la Mikocheni B, majira ya saa mbili usiku.

Alisema wakiwa na ndugu yake ambaye ni marehemu wakiangalia luninga ulizuka ugomvi uliotokana na aina ya kipindi cha kuangalia ambapo kila mmoja alikuwa anataka kuangalia kipindi alichokuwa anakihitaji, ambao ulisababisha kifo hicho.

Alisema mtuhumiwa alimpiga marehemu teke la shingo lililomwangusha chini na kumwongezea teke linguine katika sehemu za siri lililomuua kabisa.
Hata hivyo ilielezwa kuwa mara baada ya mtuhumiwa kuona amekwisha ua alimchukua marehemu na kumficha katika chumba kimojawapo walipokuwa wanaishi.

Ilielezwa kuwa aliporudi mama mwenye nyumba mtuhumiwa aliendelea kuuficha mwili wa marehemu pasipo kumueleza mtu yoyote kwa muda wa siku mbili.

Kutokana na hali hiyo iliweza kumshinda mtuhumiwa aliamua kutoroka, na tajiri yake alikuwa ameeenda kazini na kutoweka sehemu isiyojulikana, ndipo wakati yupo barabarani ghafla alikamatwa na polisi na kupelekwa kituo cha Oysterbay.

Na kutokana na kosa alilolifanya la mauaji hakutakiwa kujibu lolote kuhusu shtaka hilo wakati akisomewa shtaka hilo mahakamani na hadi hapo atakapofikishwa katika Mahakama Kuu kujibu shtaka hilo na kesi imeahirishwa hadi hapo January 7, mwakani.

Na Chondoma Shabani, Dar es Salaam
Souce: Nifamishe.com
 
Back
Top Bottom