Inasikitisha

Ngoromiko

JF-Expert Member
Sep 15, 2011
554
175
MKAZI kijiji cha Gehandu,Wilayani ya Mbulu Mkoani Manyara, Gainame Mori (61) amefariki dunia baada ya kukabwa na vinyango ya nyama wakati akila chakula kwenye mazishi ya jirani yaliyofanyika kata ya Magara wilayani Babati.Hali hiyo ilisababisha watu waliofika msibani hapo kushikwa na mshtuko akiwemo Mamo Magi (30) kupoteza fahamu na kusababisha baadhi ya waombolezaji kukimbia mbali na eneo hilo kwa kuogopa kufanywa mashahidi.

Tukio hilo lilitokea juzi saa 10 jioni katika kijiji cha Mayoka A wilayani Babati ambapo mzee huyo alifariki dunia papo hapo kwa kile kinachodaiwa kukosa hewa baada ya kunyongwa na finyango ya nyama wakati akila pilau.
Wakizungumza na Mwananchi baada ya kutokea kwa tukio hilo, baadhi ya mashuhuda walidai kuwa mzee huyo alifika kwenye msiba huo kwenye kijiji cha Mayoka A, kata ya Magara akiwa mzima wa afya.

Walisema mzee huyo akiwa ni miongoni mwa watu waliokuwa kwenye shughuli hiyo na akawa anapata chakula katika sinia pamoja na wazee wenzake huku wakisubiri taratibu za mazishi hayo.

"Ghafla wakati anaendelea kula chakula mzee huyo akawa anatoa macho na machozi na watu waliokuwa jirani yake wakadhani mzee Mori anamsikitikia na kumlilia marehemu huyo," alisema mmoja kati ya shuhuda wa tukio hilo.

Walisema baadhi ya watu walitambua mzee huyo amekwamwa na nyama wakawa wanampiga ngumi mgongoni lakini nyama hiyo haikutoka ndipo mmoja kati yao akaitoa kwa kuingiza mkono wake kwenye kinywa cha mzee huyo.

Hata hivyo,walisema mzee huyo alifariki dunia papo hapo kwa kile kinachodaiwa kukosa hewa baada ya kunyongwa na nyama hiyo,ndipo wakatoa taarifa kwenye ofisi ya kijiji hicho pamoja na polisi.

Mwili wa marehemu huyo umehifadhiwa kwenye hospitali ya wilaya ya Mbulu kwa uchunguzi zaidi na Magi amelazwa kituo cha afya cha Magara ambapo hali yake inasemekana inaendelea vizuri baada ya kupatiwa matibabu.

Source: Gazeti Mwananchi
 
Back
Top Bottom