inasikitisha sana mtoto huyu jamani!!FATAKI kaharibu

kilimasera

JF-Expert Member
Dec 2, 2009
3,068
268
MLEZI wa mtoto mwenye umri wa miaka minane anayedaiwa kunajisiwa, ameiomba Serikali na taasisi mbalimbali kumsaidia fedha za matibabu ili mtoto huyo akatibiwe.

Akizungumza na gazeti hili jana jijini Dar es Salaam, Marium Omary, shangazi wa mtoto huyo ambaye ni yatima anayesoma darasa la pili katika shule ya Msingi Buguruni, alisema tangu mtoto huyo aingiliwe kimwili na mwanaume wa miaka 25 na kuchanwa katika maumbile yake hajapata tiba ya kutosha.

“Nalazimika kumvalisha vitambaa hasa anapokwenda shule kwa kuwa haja zinatoka mara kwa mara kupitia njia ya uzazi. Naomba msaada mtoto huyo ashonwe ili awe na maisha mazuri kama watoto wengine,”amesema.

Amesema, mtoto huyo (jina limehifadhiwa) alinajisiwa, Agosti mosi mwaka jana saa 3 asubuhi katika eneo la Buguruni.

Mariam amesema, baada ya kufanyiwa kitendo hicho, mtoto huyo alipelekwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili, Dar es Salaam, akalazwa lakini Daktari aliyekuwa akimtibu alisema hawezi kumshona kabla kidonda hakijakauka hivyo alimpa dawa za kutumia.

Amesema, walipokwenda mara ya pili waliambiwa daktari huyo aliyemtaja kwa jina la Mohamed aliondoka na kuhamishiwa katika hospitali nyingine na kumtaka aende huko alipo lakini alishindwa kwa kuwa hana fedha.

Kwa upande wake, mtoto huyo amesema, siku ya tukio kijana alimuita na kumuomba amsindikize kwenye duka la dawa ghafla akamuingiza kwenye nyumba mbovu na kumlisha pipi aliyoipaka dawa yenye rangi nyeupe akamziba mdomo na kumuingilia kimwili.

Omary amesema, mtoto huyo amepata madhara makubwa kwa kuwa njia yake ya haja kubwa na ndogo vimeunganika na kuwa wamefungua kesi namba 864 ya mwaka 2010 katika Mahakama ya Wilaya ya Ilala na mshitakiwa, Mwarami Gumbo (25) yupo mahabusu.

Mwendesha Mashtaka Mkuu wa Mahakama ya Wilaya Ilala, Naima Mwanga amethibitisha kuwa kesi hiyo imefunguliwa mahakamani hapo.
 
kwanza naomba hii pia ipelekwe jukwaa la kisheria labda msaada zaidi wa kisheria unaweza kupatikana.

Pili, nampa pole huyo binti na mlezi na kumlaani huyo kijana.

Tatu, huko mahabusu ufanyike u-mafia huyo jamaa nae afanyiwe the same yaani hadi njia yake ya nnya ipasuke ili a-feel alichomfanyia huyo malaika wa mungu.
 
Kama kuna njia yoyote ya kuweza kuwasiliana na mzazi au mlezi wa huyu binti, naomba mnijuze au mniPM niko tayari kugharamia matibabu ya mtoto huyu.
 
ubarikiwe sana uliyejitolea kumsaidia huyu binti!! Mungu akujaalie, nimesikitika sana kama binadamu anaweza kumpa binadamu mwenzake mateso katika dunia hii
 
OMG! yaani machozi yamenitoka jamanii inauzunisha sana hivi hawa wanaobaka watoto wadogo kwanini wasihasiwe kama Mbizi,ngombe, Mbwa?
jamani wantuharibia watoto na taifa letu.....i wish nae huyo kijana anajisiwe naye asikie maumivu yake sijui watafute tembo ama punda ndio atamfaa
 
nadhani ule muswaada unaotakiwa kupitishwa wa kuhasiwa kwa wanaume wanaobaka na kunajisi Zanzibar upate kasi na Bara ili watu kama hawa tuondoke kabisa kende zao. Huu ni ukatili ulopitiliza
 
Kama kuna njia yoyote ya kuweza kuwasiliana na mzazi au mlezi wa huyu binti, naomba mnijuze au mniPM niko tayari kugharamia matibabu ya mtoto huyu.

Nenda kituo cha polisi Buguruni au Mahakama ilipofunguliwa kesi watakusaidia kumpata huyu mtoto. Ukimpata, mpe pole nyingi saana kutoka JF.

Alaaniwe alietenda hiki kitendo ambacho hata wanyama hawafanyi, hafai kuwachiwa kutembea mitaani hata kidogo.
 
huyo mtu aliyefanya unyama huo inatakiwa anyongwe mbele ya umati pale mnazi mmoja iwe fundisho kwa mafataki.halafa hao watu wa hospital hawana huruma?wangemtibu kwanza madai ya pesa baadae
 
Sometimes I just wish I could be recruited as a sniper

Huyu jamaa angekua ameshazikwa at this time.

Ee Baba Yetu Uliye Mbinguni

Umsaidie huyo mtoto na familia yake.
 
..Utashangaa kuwa uchunguzi wa kesi hii utachukua mwaka mzima na shetani aliyefanya unyama huu atakuwa anpeta tu mitaani. Naungana na mtu anayesema hapo kuwa anatamani awe sniper. Inatia Uchungu Mno na Hasira Mno.
 
system ya bongo ishachoshaga zamani sana watu wengi sana haki zao zinapotea nadhani tukibadilisha mfumo wa utawala haya yote yanaweza kubadilika!
..Utashangaa kuwa uchunguzi wa kesi hii utachukua mwaka mzima na shetani aliyefanya unyama huu atakuwa anpeta tu mitaani. Naungana na mtu anayesema hapo kuwa anatamani awe sniper. Inatia Uchungu Mno na Hasira Mno.
 
Back
Top Bottom