Inasikitisha..Je waujua Ukweli juu ya Adhabu ya Kifo… “Abolish Capital Punishment”

LAT

JF-Expert Member
Nov 20, 2010
4,401
1,312
Nchi yetu ya Tanzania bado ina adhabu ya kifo ..


Je nchi yetu na wananchi tunajua ukweli wowote juu ya ndugu zetu waliokosa na badala ya kuwarekebisha ili warudi kundini lakini tukatumia sheria zisizofaa na kuwahukumu kwa kuondoa maisha yao hapa hapa duniani...? wangapi wameshanyongwa hapa nchini....? je rais wa nchi kuvunja kalamu kama ishara ya kuondoa maisha ya mtu ni sahihi...? je kati ya jaji.., raisi au myongaji ..., ni nani atakayewajibika katika hukumu ya mwisho mbele ya mungu kama mtenda dhambi wa adhabu ya kifo......


ndugu ninaomba uangalie jinsi aina za kifo zinazotumika kutekeleza adhabu hii duniani..,


1. Sindano ya Sumu (Lethal Injection)
Mtu hupigwa sindano Tatu…ya kwanza hukufanya ulale usingizi.., ya pili hufanya misuli yote iwe haifanyi kazi…ya tatu sindano ya sumu (lethal injection) ya kuupasua na kuuzimisha moyo


2. Kiti cha Umeme (Electrocution)
Miguu,mikono, kifua na magoti hufungwa na mikanda kwenye kiti.. Kofia ya chuma yenye nyaya za umeme zenye hasi na chanya huvalishwa kichwani , maji kidogo humwagwa kwenye mwili wa mtu kwa kutumia sponge na switch ya umeme kuwashwa


3. Chumba cha Gesi ( Gas Chamber)
Mtu huingizwa kwenye chumba akiwa amefungwa kwenye kiti… gesi ya sumu huingizwa ndani ya chumba kisichotoa hewa na kuvuta hewa yenye sumu



4.Kupigwa risasi (Firing Sguad)
Mtu hufungwa macho kwa kitambaa cheusi..akiwa amekaa kwenye kiti kafungwa na mikanda..huwekwa mbele ya ukuta wa boxi gumu…boxi huwekwa mbele ya kiwiliwili chake na sehemu ya moyo ulipo kuonyeshwa..kama alama ya kulengea.. wafyatua risasi watano hujipanga futi 20 na bunduki zenye risasi 30 kila mmoja…mmoja hulenga alama ya kwenye moyo katika mtu huyu


5. Kunyongwa kwa kitanzi (Hanging)
Mtu hupimwa uzito wake ..kamba yenye nguvu na uwezo wa kustahimili uzito huu hutengenewa.. miguu ., mikono hufungwa..macho hufungwa kwa kitambaa cheusi..kamba yenye kitanzi iliyopakwa mafuta ya kulainisha huvishwa kwenye kitanzi.. na mtu kuachiwa ashuke chini na kitanzi

Kabla ya siku ya kifo… mfungwa aliye kwenye death row ..hupewa haki ya kuchagua chakula akipendacho kula…. Hupewa nafasi ya kuacha wosia… mwisho hupewa nafasi na muda wa kuonana na kiongozi wa dini yake kutubu , kuomba na kusali..,


This type of justice is immoral, rude, blatant and militant

I argue and propose that .... the prospective new draft constitution of the United Republic of Tanzania to abolish capital punishment a.k.a death penalty .... it is against the well-being of the human rights


tuipinge sheria hii mbaya nchini kwetu
 
Back
Top Bottom