Inasikitisha askari polisi kuendesha pikipiki bila helmet au kumpakia abiria bila kuvaa helmet

Magobe T

JF-Expert Member
Mar 19, 2008
4,621
2,567
Hakuna kitu kinachokera kama kuona askari polisi wanaosimamia utekelezaji wa sheria wao wenywe ndio wa kwanza kuzivunja. Mara kadhaa nimekuwa nikiona askari polisi wakiendesha pikipiki bila helmet au askari polisi amempakia mtu asiye na helmet. Nchi nyingine ambako sheria zinasimamiwa vizuri kitu kama hiki kukioni. Lakini hapa kwetu kila siku kinaonekana na wakati huohuo askari wanasimama barabarani kuwakamata waendesha pikipiki bila helmet au kama wamempakia mtu asiye na helmet isipokuwa kama anayekamata ni askari mwenyewe - maana wao kwa wao wanasameheana. Kwa maneo mengine, wao wanaridhia kuvunja sheria kama askari!

Nikiona hivi huwa najiuliza: Hivi hawa askari wanatufundisha nini sisi wananchi! kwamba wao wako juu ya sheria? Kwamba hawajali sheria? Kwamba wana mamlaka ya kufanya watakavyo? Hali hii ni ulimbukeni!
 
wao ndio law breakers namba moja,hawavai helmet,wanatanua na kupaki hovyo.pia traffic wanasimamisha watu hata kwenye keepleft
 
Mbona Dr. wanafundisha watu wasifanye mapeni bila condom lakini wenyewe ni namba moja kwa kutovaa, kunyweni maziwa wao hawanywi, pombe ina madhara wao ndiyo wanalala baa! Kwa mimi naona mtu akiendesha gari, pikipiki bila kufuata sheria za usalama baraari haijalishi ni askari polisi namuona ni mjinga anahatarisha usalama wake.
 
madoctor hiyo ni habari nyingine mana kama ni ukimwi kuna ile dawa yao ya kiinywa kabla ya masaa 24 ya maambukizi alafu mambo yoote swafiii, kuhusu kukaa na kulala bar ni kuchezea mshahara na sio kazi, ila la police kuendesha motor bikes without helmets...... they simply not educated anough to understand the conciqueces and keep in mind wengi wao ni wale wa.darasa la saba so uelewa bado, nikupe mfano - kuna mmoja nilimkuta ati kavaa mask ya kuzuia vumbi kwenye mdomo na pua yake lakini hajavaa helmet.. sasa that can tell u alot about ones brains
 
Hili limenigusa kwenye kidonda cha siku nyingi. Tatizo hapa ni sheria kawekewa nani - sisi au wao na sisi. Hiyo haitoshi. Kofia nyingi ambazo zintumika kwa sasa hazimlindi mwensha pikipiki. Ni nyepesi mno kiasi kwamba ikidondoka inapasuka - kichwa je? Mamlaka husika ya viwango inasubiri mtu mashuhuri apasuke kichwa kwa sababu ya hizo kofia ndio wanze kuja conflicting statements na wenzao wa usalama. Yapo mambo mengine unashindwa kuelewa utawala haswa unakuwa wapi mambo yanaenda mrama.
 
Don't tell me. Hawa jamaa bora wangekuwa wanakukamata na kukutoza faini halali. Wao ni rushwa wazi wazi. Ukienda takukuru ndo walishatangulia. Utajikuta kwenye kesi eti we mzushi. Nchi hii!
 
Back
Top Bottom