Inasemekana Dr. Namala Mkopi kiongozi anahojiwa Central Police muda huu

kuna kitu kimoja sikielewi, iweje Dr Kamala aende kuhojiwa central wakati kesi iko mahakama ya kazi? hii ni sheria ipi kwa mnaujua sheria ya kazi hebu tunaomba mtufafanulie juu ya jambo hili.

Cha pili sikielewi ni kwamba, naamini kikwete alifanya uchunguzi juu ya jambo hili la madaktari na kulitolea hukumu, sasa huko mahakamani hii kesi bado inafanya nini ikiwa kikwete keshaamua kwamba wasiopenda mshahara wa serikali waende kwingine.
Wanazidi kutupa utata tu hawa ccm, hivi wamekuwaje jamani au ni laana za kuingia madarakani kwa uongo na udhalimu wa haki za binadamu? maana sasa imezidi.
 
Mbona hawajamuita ACP Msangi kuhojiwa kwa sababu anatuhumiwa kushiriki kumteka na kumtesa Dr. Ulimboka????

Sasa wakimuita kumhoji huyo jamaa ili hali kuna kila dalili wao ndio walimtuma si itakuwa kama wanajitia kidole cha makalio
 
Kichekesho wanao mhoji wana elimu ndogo kuliko yeye.
 
Jamani, dr Mkopi amefika central polis about 16 hrs, sasa ni about 21 hrs, hebu tupeane update, kama ameshapelekwa mabwepande tujue. This time no need ya kumpeleka majeruhi Boko polis post maana ndio wasimamizi wa kituo cha mauaji. Tutaenda direct sauz ama ughaibuni.
 
jamani , ebu tuwekee picha ya huyu ACP Msangi ili akija hospitali tumpe tiba sahihi.

Nani mwenye picha ya ACP Msangi? Niko tayari kuinunua ili nione sura yake. Au anafanana na Zombe? Kwanini naye hajahojiwa kwa tuhuma zinazomkabili? Kwanini hakuna mtu yeyote aliyekamatwa kwa tukio la kuteswa kwa Dk. Ulimboka? Kwanini Kikwete alikimbilia kusema kuwa Serikali haihusiki wakati hakuna uchunguzi wowote uliofanyika? Kwanini? Kwanini? Kwanini?
 
Labda Kikwete anasubiri Wazee wa Mkoa wa Dar es Salaam waamke usingizini azungumze nao.
Nimeisoma hiyo barua, kwani kuna jambo gani hapa serikali inaogopa? Ukweli uko wazi na Dr. anaendelea vizuri na ana fahamu zake kila kitu kitakuwa hadharani. Kwa hakika waliotenda ile kazi walijua wamemaliza kazi kumbe Mungu amempangia kila binadamu kifo chake?!!!!!!! Cha msingi serikali ikubali kuwa fani ya udaktari na ualim si ya kuchezea na iwe na busara na majibu ya viongozi waandamizi wa serikali. Ni vema busara itumike kuongea na hawa ndugu zetu maana ni wasomi wa miaka 7 na si chekechea hawa!!!!! Huduma ya afya ni nyeti hasa kwa sisi ambao hatuna uwezo wa kwenda private au nje ya nchi kwa matibabu. So sad that the crisis is on and no sustainable solution to it. For now, I believe Tanzania lacks mediation expects!!!!!!! So sad our relatives and friends are dying out there na hakuna anayejigusa kuongea inavyopaswa na hawa madaktari. Yaani hadi sasa ni kimya kabisa!!! Hivi kweli wakiacha kazi Tanzania ina uwezo wa ku-hire nje ya nchi? Watawalipa expetriate remunerations au ni vipi? Kwa hakika the medical workforce shortage is a crisis in Tanzania halafu tena waache kazi? Let us be frank and look for a better way to solve it na tuache ubabe na vitisho.
 
Kuna sehemu fulani(sitaitaja) kulikuwa na tatizo kama hili,walichokifanya madaktari kilikuwa tofauti kidogo na hapa kwetu.Wao walihakikisha kuwa kiongozi yeyote wa serikali anayeenda kwa matibabu pale basi lazima afe.Na akija kutibiwa polisi basi ndio hata masaa mawili hatamaliza atakufa tu.Kilichoishtua serikali ni pale polisi mmoja alipokwenda kupimwa macho baada ya muda mfupi akafa,ikabidi wahusika wawaite madaktari na kuwauliza kulikoni,jamaa wakaeleza yote yaliyomo mioyoni mwao na wakatekelezewa yote.Hivyo ningeshauri tu madaktari waache kuvutana na serikali warudi tu kazini na ni serikali hiyohiyo itakayokuja kuwaita tena na kuwaambia jamaniee tutnawalipa stahilizenu zote mnazotudai.
 
wazee wa intelejensia za kipinzani.ukipinga ccm ndo wanafnya intelejensia zao. i hate you police

Lakini vyombo hivi vyote vya usalama huwa vinakula kiapo kulinda serikali iliyoko madarakani pamoja na wananchi wake, bila shaka hata hao cc wapinzani tukifanikiwa kupata madaraka sidhani kama tutaachia serikali iwe inachezewa chewa lazima kutumia vyombo hivyo hivyo kulinda serikali mpya. Therfore we should be very carefully with dis Politics otherwise tutakuwa tunalalamika kila kukicha kwa sababu si tunaona kila siku wao kwa wao ndani ya vyama wamekuwa na migogoro ya kimaslahi si nyie m, C.D.M, Kiafu, wala N nyie R.
 
Kichekesho wanao mhoji wana elimu ndogo kuliko yeye.
Sio Kichekesho Kwani Kila Kazi ina Elimu au Ujuzi Wake Ficha Upumbavu wako... Huyo Dr. alichosomea ni kumuelekeza Mgonjwa kula Dawa iliyotengenezwa na Mkemia... na Mkemia anatengeneza Dawa Zake kwa kumtegemea Enjinia na Injinia anategemea wengine na n.k Elimu ya Udaktari au vinginevyo havihusiani na na kazi ya Kipolisi... Polisi nao wanasomea kazi zao Japo zinauma kwa Mkosaji
 
Back
Top Bottom