Inakuwaje Rais ajisifu nchi kusaidiwa.

olele

JF-Expert Member
Dec 2, 2010
1,303
1,559
Wakuu habari zenu
Jana nimesikiliza hotuba ya Mhe. Rais Kikwete, katika mambo mengi aliyozungumzia
Amesisitiza sana jinsi gani nchi inavyopatiwa misaada na nchi wahisani, amejisifu sana kuhusu wa-canada wanavyosifia shule za sekondari na wameonyesha nia ya kuongeza misaada. Sasa mi najiuliza inakuwaje rais ajisifu jinsi gani taifa linavyotegemea misaada?
Au watanzania tunapenda sana kuomba omba
Nawasilisha kwenu mi naona hainingii akilini
 
Labda ipo top kwenye manifesto ya chama chake! Mbona hazungumzii matokeo ya hizo shule?
 
Miaka ya hivi karibuni serikali ya Kanada imekuwa msitari wa mbele sana kumpongeza Kikwete kutokana na shinikizo la Barrick Corporation. Wametumia lobbyist mkali sana kuhakikisha kuwa serikali ya canada inampromote Kikwete tangu Sinclair alipokubaliana kumkatika kidogo Kikwete kusudi asivuruge mikataba ya dhahabu. Ndiyo maana ni Kanada pekee katika nchi za west iliyotuma salamu za kumpongeza Kikwete binasi kwa "ushindi," wengine wote walituma message generic za kidiplomasia bila kumtaja Kikwete explicitly: Kanada walifanya hivyo.
 
Kama wakanada wanachukua dhahabu hapa kuna ubaya gani nao kusaidia jamii ama ulitaka iweje hasa maana sioni mantiki hapa .
Ama ulitaka tz ikipewa hiyo misaada ikajenge shule Otawa
 
Wakuu habari zenu
Jana nimesikiliza hotuba ya Mhe. Rais Kikwete, katika mambo mengi aliyozungumzia
Amesisitiza sana jinsi gani nchi inavyopatiwa misaada na nchi wahisani, amejisifu sana kuhusu wa-canada wanavyosifia shule za sekondari na wameonyesha nia ya kuongeza misaada. Sasa mi najiuliza inakuwaje rais ajisifu jinsi gani taifa linavyotegemea misaada?
Au watanzania tunapenda sana kuomba omba
Nawasilisha kwenu mi naona hainingii akilini

Akili ya mkwere ndiyo imegoti hapo. Ndiyo tabia ya watu wa mwambao!! Hata kama ni rais, tabia ipo damuni,.
 
Wakuu habari zenu
Jana nimesikiliza hotuba ya Mhe. Rais Kikwete, katika mambo mengi aliyozungumzia
Amesisitiza sana jinsi gani nchi inavyopatiwa misaada na nchi wahisani, amejisifu sana kuhusu wa-canada wanavyosifia shule za sekondari na wameonyesha nia ya kuongeza misaada. Sasa mi najiuliza inakuwaje rais ajisifu jinsi gani taifa linavyotegemea misaada?
Au watanzania tunapenda sana kuomba omba
Nawasilisha kwenu mi naona hainingii akilini

Asipoenda kuhemea ulaya tutakufa kwa njaa hapa nchini. Alitumia hiyo kama turufu ya kampeni na akashinda kwa kishindo ikimaanisha kuwa wananchi wapiga kura wengi wanakubaliana na viongozi wao wanapoomba misaada ulaya na kwingineko.
 
Uwezo wake wa kufikiri umeishia hapo, kama alishatamka mchana kweupe kuwa hajui kwanini Tanzania ni masikini licha ya utajiri lukuki wa rasilimali uliopo ulitegemea nini toka kwake? Kwa JK jibu la umasikini wa Tanzania ni kupata msaada.
 
Kama wakanada wanachukua dhahabu hapa kuna ubaya gani nao kusaidia jamii ama ulitaka iweje hasa maana sioni mantiki hapa .
Ama ulitaka tz ikipewa hiyo misaada ikajenge shule Otawa

Mwandishi analalamika kuwa Mheshimiwa Rais anajisifia nchi kupewa misaada na nchi nyingine. kitu ambacho hata wewe kwako huwezi kujisifia jirani akiwa anakupa msaada kila siku itakuwa ni ujinga.
 
Mimi naona ni bora tuombe nchi yetu iwe koloni la Canada badala ya kuwa nchi huru. Kama tutakuwa koloni na hawa jamaa wataleta maendeleo ni kipi bora? Kama watu wanajisifu kwa kusaidiwa kwa nini tusiwape nchi hao jamaa tu?
 
Tujitahidi kuelimisha jamii kuhusu ubaya wa kuombaomba na kutegemea misaada kwa kuwa Rais anatokana na jamii yenyewe, kila mtu akichukia mawazo ya kuombaomba basi hata Raisi atachukia kuombaomba kujisifu kwa kusaidiwa!
Kuomba msaada mara nyingi ni jambo la kufedhehesha na hivyo siyo la kujivunia!
 
Mimi binafsi kwa binafsi yangu,sikumchagua huyu jamaa ingawa analazimisha kunitawala na wala hawezi kuniongoza kwani najua atanipeleka shimoni,ana akili iliyolala huyu jamaa na sijui nani sasa wa kuiamusha kwan wote wanao mzunguka ni ma-bongolala kama yeye,...anaona kusaidiwa ni haki yake ya kimsingi,....aaaaaah!...ndugu rahisi bwana.
 
Wakuu habari zenu
Jana nimesikiliza hotuba ya Mhe. Rais Kikwete, katika mambo mengi aliyozungumzia
Amesisitiza sana jinsi gani nchi inavyopatiwa misaada na nchi wahisani, amejisifu sana kuhusu wa-canada wanavyosifia shule za sekondari na wameonyesha nia ya kuongeza misaada. Sasa mi najiuliza inakuwaje rais ajisifu jinsi gani taifa linavyotegemea misaada?
Au watanzania tunapenda sana kuomba omba
Nawasilisha kwenu mi naona hainingii akilini

Aeleze pia na matokea ya hizo shule, hali kadhalika na sababu za ziro zaidi ya 80%.
 
mkwereeeeeeeeeee huyo jamani so msishangae kwa nn anaomba........... keshasema kuwa wa tz ni wa2 wa kuhemea 2......:msela:
 
Hata mabango ya kampeni wakati wa uchguzi alitengenezea hukohuko Canada
 
inabidi tuogope sana pale unapokua na baba anategemea wanaume wenzake ili aweze kuonoza nyumba yake ni jambo la hatari sana na kuogopa. tena anaongea kwa kucheka bila hata ya woga rais wa ajabu kabisa

atatufikisha mahala pabaya sana huyu bwana
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom