Inakuwaje hapa....ni kweli tunatengeneza hasara hii?

Masikini_Jeuri

JF-Expert Member
Jan 19, 2010
6,829
1,296
Wana jamvi nimekutana na habari ya msaada wa USAID kwenye sekta ya kilimo katika gazeti la Mwananchi nikafurahi sana lakini furaha yangu hiyo ilizimwa na taarifa ya kusikitisha iliyopo ndani ya habari hiyo na nukuu "..................... Alisema hatua ya Tanzania kutoza kiwango hicho cha Vat, imefanywa wakati USAID ikiwa imetoa Dola 1.3 milioni za Kimarekani kuiwezesha Tanzania kuleta ndege hiyo ili isafirishe maua, matunda na mbogamboga, kupitia Uwanja wa Kimataifa wa Ndege wa Kilimanjaro (KIA).

"Hatua hii imesababisha Tanzania kupoteza zaidi ya Sh bilioni 29 kutokana na kuanguka kwa biashara hiyo, kulikochangiwa na utozaji wa kodi ya VAT ya asilimia 18," alisema Dk Rweikiza.

Mkurugenzi huyo alitaja maeneo mengine ambayo Tanzania imekuwa ikipata hasara kuwa ni pamoja na ya ubebaji wa mizigo katika viwanja vya ndege, eneo ambalo alisema serikali inapoteza zaidi ya Sh 91.7 milioni na kwamba hiyo inatokana na utozaji wa kodi kwa kazi hiyo."
 
Nimebold vipengele vilivyonivuta nikaileta maada kwenu;

Kwamba tumeua biashara kwa vile tu tulianza kutoza kodi na sio biashara tu ni biashara ambayo ilikuwa ikiwafaidia wakulima! Na zaidi ya hasara hiyo huo mchezo wetu wa kutoza toza kodi umepelekea hasara kubwa zaidi kama nilivyonukuu hapo chini

Swali kwa wana jamvi ni kweli nchi imekuwa ikipata hasara hizi na ni kweli tumeanzisha kodi ambayo hatimaye imeua biashara yenyewe iliyotarajiwa kuzalisha pato kwa wananchi?
 
Back
Top Bottom