Inakuhusu

MMDAU

Member
Aug 15, 2012
94
19
Nimejaribu kuchunguza katiaka jamii yetu hii ya kitanzania pamoja na huku jamii forum nikagundua kuwa watu wengi walio ktk mahusiano hayadumu (maranyingi ni kuanzia siku moja hadi miaka mitano) na hata ndoa nyingi pia hazidumu hivi tunamkosi gani binadamu wa sikuhizi, mapenzi yamekuwa kama nguo leo hii kesho ile magonjwa yameonekana ni jambo la kawaida nini hasa kimepelekea hivyo kila siku mtu kaachwa, mara mpenzi wangu simwelewi, mara watu wanatumia 065/071. kwanini jamani.

MUNGU atuepushe kwani tunapoelekea ni pabaya itafikia siku tunaowana asubuhi jioni tunaachana. watu wanaapa kuwa wataishi pamoja milele baada ya siku chache wana achana kwanini tunamdanganya MUNGU mbele za watu. kuwa na wapenzi wengi sikuizi ndio fashion. Inaniuma sana moyoni, marafiki wana salitiana bila woga, watu wanamsingizia shetani mpaka najiuliza hata kama shetani akizaliwa sasa hivi kisha akaonekana kwa watu watamuuwa japo hakuanza kutenda zambi. wakati mwingine tunajua kabisa kuwa tufanyalo sio sawa
 
Shetani wa mtu ni mtu mwenyewe,,lakini hayo tunaweza kuyashinda tukiwa na hofu ya Mungu,,.
 
Hizi ni dalili kuwa dunia inaelekea kuisha, mimi nampango wa kuhamia kwenye sayari ya Mars nasikia kuna viumbe wengine kule..
 
Duniani maajabu hayaishi hata mimi huwa najiuliza sijui itakuwaje huko.mbeleni nikiamua kuoa maana bora yaishe tu Yesu aje maana utabidilisha kila mtu lakini wote sawa akili zao
 
Futa kauli ya kumsingizia shetani! It seems uyo shetan n innocent e? Shetan n shetan na yote yanayotokea kapanga yeye na anadirect yeye kwa casts wake wanaokubali kuigiza,hakuna suala,la kumsingizia shetani.
 
Futa kauli ya kumsingizia shetani! It seems uyo shetan n innocent e? Shetan n shetan na yote yanayotokea kapanga yeye na anadirect yeye kwa casts wake wanaokubali kuigiza,hakuna suala,la kumsingizia shetani.

Unajua binadamu hatujitambui na hatujui kuwa hatujui. Hii sasa inaenea sana kuwa eti unamsingizia shetani, hivi nani alisababisha matatizo yote haya kwa binadamu? Soma maandiko matakatifu.
Binadamu atalaumiwa pale anaposhindwa kukwepa au yeye mwenyewe kuamua kumfuata shetani, lakini chanzo cha kila aina ya ubaya na uovu ni shetani, na hasingiziwi.
 
Inategemea na wewe ulivyo kama unamwogopa Mungu huwezi kufanya vitu kama hivyo
 
Kuna mahusiano yakivunjika, unamshukuru Mungu! Kuna watu wana maisha ya ajabu kwa namna ya kipekee aisee!
 
Watu siku hizi wamekuwa ni wepesi kumsingizia shetani kumbe ni tamaa zao wenyewe..
Wengine hudiriki kusema etii Mungu hakupenda.
Mungu turehemu waja wako
 
Back
Top Bottom