Elections 2010 In Statistic CUF Imeshinda ZNZ

John10

JF-Expert Member
Aug 13, 2009
357
11
CCM imeiba uchaguzi Zanzibar. Kwa nini Seif anakubali matokeo wakati kihesabu CUF ndiyo walioshinda? Angalia kura za watu waliojindikisha kupiga kura na waliopiga kura utaona kuna wizi uliotokea.

Again, kwa nini Seif anakubali matokeo wakati CUF ndiyo walioshinda. Seif ni kibaraka wa CCM.
 
CUF wanaweza kuukataa uamuzi wa Seif, na baadaye kumtoa Seif madarakani ndani ya CUF. Seif atabakia madarakani ndani ya serikali ya mseto kama CCM, na siyo CUF.
 
CCM imeiba uchaguzi Zanzibar. Kwa nini Seif anakubali matokeo wakati kihesabu CUF ndiyo walioshinda? Angalia kura za watu waliojindikisha kupiga kura na waliopiga kura utaona kuna wizi uliotokea.

Again, kwa nini Seif anakubali matokeo wakati CUF ndiyo walioshinda. Seif ni kibaraka wa CCM.
huyu sio seif ninayemjua mimi
 
namshangaa seif kukubali matokeo, jamaa nadhani yeye anataka madaraka tu.
 
kachoka maalim, tumsamehe bure. Yeye anataka madaraka madaraka tu sio utawala bora
 
CCM Kali Wamemchakachua mpaka Seif, haelewi kama ameshinda, badala yake kakubali kushindwa,
..he he he eh he..., sisimi ni kiboko. Ila mwaka huu ukweli wataujua, kugawana majimbo siyo mchezo..
 
Ila maalimu kaamua jambola ujasiri, kila siku anashinda na hawampi hata akigoma atagoma mpaka lini na umri ndo huo.Watoto waliozaliwa wakati anagomea uchaguzi wa kwanza sasa ivi wapo sekondari. Aendeleee kugoma mpaka aje achuane nao kwenye urais?
 
Kauli mbiu ya CCM Zanzibar ni; "mapinduzi daima" na serikali ya Zanzibar inajulikana kama serikali ya mapinduzi! Na rais wake pia ni Mwenyekiti wa Baraza la mapinduzi. Katika hali hiyo utakubaliana nami ya kuwa serikali iliyowekwa na wananchi kwa kura, haiwezi kuitwa serikali ya mapinduzi. Ikumbukwe, marehemu Karume aliwahi kusema ya kuwa, madaraka yaliyopatikana kwa mtutu wa bunduki, huwezi kuyapoteza kwa makaratasi; akiwa na maana ya kura. Kwa kujua hilo, inaelekea maalimu Seif aliona vema akampisha mwana haramu apite.
 
Ikiwa hali ndizo hizi,chaguzi za nini?.
Unajua haya mambo ya uchaguzi yana gharama mno,kuanzia mali mpaka muda na afya.
Ikiwa kila siku tunaingia gharama hizo mwishowe matokeo huamuliwa mezani.Ni afadhali tutafute utaratibu mwengine wa kupata viongozi.
 
Utaratibu ninaopendelea mimi ni kuwepo tume maalum inayopokea maoni ya raia na kuyaweka kwenye mtandao kila siku.Watu watasema mtu anayefaa kuongoza baada ya miaka mitano ni fulani na sifa zake ni hizi......
Ikiwa watu wataendelea kuridhika naye hata miaka 70 sawa.Hii itakuwa kati na kati baina ya ufalme na demokrasia.Gharama itakuwa chini sana.Fedha zitatumika kwenye mambo ya mendeleo.

Mbaya wako kula naye sahani moja umjue vizuri,kufanya kitu ambacho majibu yake yanajirudia kila siku ni wehu.Hivyo ametumia busara kubadili mbinu,tuwe na imani salam zake za kwanza kayasema mapungufu ya tume hivyo ni wazi ataishughulikia tume ipasavyo ili iweze kufanya kazi objectively.
 
Utaratibu ninaopendelea mimi ni kuwepo tume maalum inayopokea maoni ya raia na kuyaweka kwenye mtandao kila siku.Watu watasema mtu anayefaa kuongoza baada ya miaka mitano ni fulani na sifa zake ni hizi......
Ikiwa watu wataendelea kuridhika naye hata miaka 70 sawa.Hii itakuwa kati na kati baina ya ufalme na demokrasia.Gharama itakuwa chini sana.Fedha zitatumika kwenye mambo ya mendeleo.

Mkuu Ami inakatisha tamaa. Ningependa baadaye mambo ya Waislam na Wakristo yaishe, tumuondoe madarakani shetani CCM. Maalim Seif kakubali baada ya kuombwa sana. Ila CCM watalipia uhuni wao siku moja.
 
Mkuu Ami inakatisha tamaa. Ningependa baadaye mambo ya Waislam na Wakristo yaishe, tumuondoe madarakani shetani CCM. Maalim Seif kakubali baada ya kuombwa sana. Ila CCM watalipia uhuni wao siku moja.

Hiyo siku inakuja ........... na tunaisubiri kwa hamu
 
Seif inaonekana kashinda zenj ila kafanya uungwana tu. Maneno yake kuwa wananchi ndio washindi pamoja na kusema heshima itawale yana uzito wa mustakabali wa zenj
 
Seif ni mvumilivu na mkomavu kisiasa. Unafikiri angegomea matokeo, sasa hivi zanzibar kungekuwa na misiba mingapi? Je inapendeza kuona waliokupigia kura wanakufa ili wewe uwe rais?

Mpambanaji wa dhati si yule anayetaka aone mabadiliko kabla ya kifo chake. Anc ilianzishwa mwaka 1912, miaka saba kabla ya mandela kuzaliwa; na walichokitaka waasisi wake kimetokea miaka 82 baadaye.

Nampongeza seif kwa kuwa muungwana.
 
Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom