In DEFENCE of LOWASSA (Warioba & Butiku on it)

Gin imetolewa kwenye chupa haiwezi kurudi, ukurasa mpya umefunguliwa maana hata JK mwenyewe wabunge wanaweza kumcharukia kabla ya 2010.

Nimependezwa na hili bunge kwa kipindi hiki kifupi kwa kuweza kusema ukweli na kutetea walalahoi.
 
Warioba anachemka na kachemsha kisawasawa!..

Ukisikiliza hotuba ya Mzee six ambayo nimeiweka ktk mada nyingineyo utaona kuwa mwenyewe alishikwa na bumbuazi baada ya Lowassa kujiuzuru yaani hakutegemea na kuna habari kuwa alishindwa kuendelea akitaka ushauri iwe vipi swala hili. Uhakika habari nilizozipata kulitakiwa kuhojiwa mawaziri wahusika kina Lowassa na kamati ya uchunguzi kuhusiana na uchunguzi huo..

Nitanukuu tena maneno ya Mzee six hapa:-
"Sasa baada ya kuwa mheshimiwa Waziri Mkuu amemuandikia Rais barua kwamba anajiuzulu na jioni hiyo hiyo ombi lake kukubaliwa na kwa mujibu wa Katiba kwa kutumia kifungu hicho cha 57(2)E ni dhahiri kwamba Bunge hili sasa hatuna serikali.
Sasa waheshimiwa wabunge kwa kuwa serikali imebaki na Rais na Makamu wake ambao nao hawamo ndani ya Bunge, ibara ya 63 (2) ya Katiba inatamka kazi zetu kama Bunge ni kuishauri na kuisimamia serikali, ikiwa ni pamoja na kuwahoji maswali Mawaziri lakini sasa hawapo,`` alisema Spika na kupigiwa makofi yaliyoambatana na vicheko.

Sasa ni nani aliyefanya uhuni hapa kama sio yeye mwenyewe Lowassa..kwa nini alijiuzuru kabla hata uchunguzi ulioletwa kutazamwa na kuchujwa ukweli na uongo...Je, kama ingekuwa ni uongo unafikiri Lowassa kweli angejiuzuru bila kuhoji uchunguzi huo.. come on guyz Wadanganyika tusiwe vipofu na hizi sheria zinazowakumbatia watu...Huyu huyu Warioba na Butiku walitaka viongozi wanaojihusisha na Ufisadi wajiuzuru sasa ingwezekana vipi kujiuzuru kwao na kutendewa haki kwa wakati mmoja!
 
Hivi huyu Warioba na Butiku wametoka wapi? Sio hawa waliotuletea huu uvundo kwa kushindwa kwao kazi walipokuwa karibu na usukani? Hivi sasa wanakula pension yao halafu wanataka kukebehi wananchi, hawa ni wezi na hakuna sababu ya kutafuta ushahidi kwa kila jambo.

Kama EL kweli anaona haku kutendewa haki afungue mashitaka kulishitaki Bunge na kamati yake. Hatuwezi kuendelea na lelemama kama hizi, kwanza ni lazima ashitakiwe arudishe ubadhirifu wa kulihujumu taifa. Anaweza kutetewa na mtetezi mkuu wa MAFISADI Mkono wa Mkono.

hawa ni wezi na hakuna sababu ya kutafuta ushahidi kwa kila jambo.

Kwa hiyo kesho na keshokutwa tukikuundia a witchhunt committee itakayoku frame na kukusomea a summary execution report bila kukupa nafasi ya kujitetea itakuwa poa tu.Au siyo?
 
1.[
B] warioba ameongelea sakata la richmond..na kusema ripoti haikuwa mbaya ..[/B]

Quote: Mwakyembe Report:-

" Mheshimiwa Msabaha, alituuuma sikio kamati teule kuwa katika suala hilo yeye atakuwa kondoo wa kafara tu au, kwa maneno yake mwenyewe "Bangusilo" kwa lugha ya kizaramo. Maelezo hayo ya ziada yako nje ya kiapo ya mheshimiwa Waziri yaliyotoa ujumbe kuwa "...si yeye ila mkuuu wake wa kazi..." yalioana na maelezo aliyoyatoa Blozi Kazaura nje ya kiapo na kamati teule, Balozi alitoa maelezo ya ziada kuwa "Richimonduli ulikuwa mradi wa bwana mkubwa na mshiriki wake mkubwa kibiashara" akimaanisha Waziri Mkuu Lowassa, na Mbunge Rostam Aziz."

2. [
B]warioba ameelezwa kusikitishwa kwake na kitendo kwa utaratibu wa haki kukiukwa kwa ripoti kubwa kama hiyo kuonesha udhaifu wa kutomuhoji MTUHUMIWA MKUU.,amesema hilo kiutaratibu si sawa na kisheria imesababisha haki isionekane kutendeka[/B]

Quote: Mwakyembe's Report:-

"Pamoja na woga uliokuwa dhahiri wa watumishi hao, ushahidi wa maandishi, wa mdomo na kimazingira ambao kamati teule iliupata kutoka kwa mashahidi mbali mbali, unamhusisha Waziri Mkuu na mchakato mzima wa maamuzi katika suala hili la Richmonduli"

3.
..alimlaumu mbunge lucas dseleli na mwakyembe kwa hilo..HATA hivyo seleli alijitetea kuwa wao walikuwa wakijiuliza kama wamuite wakaona anaweza kukataa..wakafikiria kumuuliza rais kama wamuite ..pia wakaacha na mwisho wakaamua bora tu wapeleke ripoti bungeni,

Quote: Mwakyembe's Report:-

(a). Mashahidi wawili, Ndugu Daniel Yona na Mheshimiwa Rostam Aziz, walipelekewa hati ya kuwaita mbele ya kamati teule, lakini hawakufika kwa maelezo kwamba walikuwa nje ya nchi.

(b). Ni dhahiri kuwa, kwa watumishi hao "Waaminifu" wa serikali, isingelikuwa rahisi kumtaja Waziri Mkuu chini ya kiapo. Hatua hiyo inahitaji ujasiri mkubwa na uzalendo wa hali ya juu.

4.
..hata hivyo warioba aliwaambia kwa kuwa walikuwa hawakumuita..jambo la busara lingeweza kuwa kupeleka ripoti bungeni NA KUTOPENDEKEZA LOLOTE KWA WAZIRI MKUU KWA KUWA YEYE HAKUHOJIWA ..HIVYO BUNGE LINGEFANYA KAZI YA MWISHO YA KUSIKILIZA UTETEZI WAKE ..NA KUAMUA PENDEKEZO AU AZIMIO LA KUTOA KWA RAIS KUHUSU WAZIRI MKUU..ALIMALIZIA KWA KUSEMA KWA KUWA KOSA LA KISHERIA LIMESHAFANYIKA ..IWE FUNZO KWA TUME NYINGINE ZITAKAZOFUATA...KUTOMUHUKUMU MTU BILA KUMSIKILIZA!

Quote: Mwakyembe's Report:-

Ibara ya 52 ya katiba ya jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 inatamka wazi kuwa Waziri mkuu ndiye mwenye madaraka ya juu ya uthibiti, usimamiaji, utekelazaji wa siku hadi siku wa kazi na shughuli za serikali ya Jamhuri ya Muungano. Na ndye Kiongozi wa shuguli za serikali Bungeni.

Kamati teule haikufurahishwa na taarifa zinazomgusa moja kwa moja Mheshimiwa Waziri Mkuu, katika kuipendelea kampuni ya Richimonduli.

Hata hivyo kamati teule imetimiza wajibu wake kwa uwazi na ukweli kama ilivyoagizwa na Bunge letu tukufu. Kwa kuzingatia umuhimu wa nafasi aliyonayo Mheshimiwa Waziri Mkuu katika uendeshaji wa shuguuli za serikali na uongozi wa nchi nzima kwa ujumla, ni wajibu wake yeye mwenyewe kupima uzito wa matokeo ya uchunguzi huuu na wajibu wake kikatiba ndani na nje ya bunge. Vile vile ni wajibu wa Bunge ambalo linathibitisha uteuzi wake kwa mujibu wa Ibara ya 51 inayothibitisha uteuzi wake. Kuangalia ikiwa matokeo ya uchunguzi huu hayajaathiri hadhi na uzito wake ndani ya bunge.
 
The past is an illusion.

Kama kuna kifungu au hakuna kifungu kinachomtaka ajiuzulu is not material to the issue.The issue ni kwamba the report is one sided and did not get Lowassas input and did not afford him a chance to clarify things from his viewpoint.

Hoja ilikuwa iwe 4 sided.
Richmonduli, Tanesco, Wizara ya fedha na Ofisi ya PM

Mwakyembe ameifanya 3 sided kwa kumwengua Lowassa na PM ofisi yake.

Tamati yake ni:

Lowassa alipindisha utaratibu ili kujineemesha Dr Mwakyembe naye kam bypass ili kumzukia kama mwenye na kumbana.

Mwosha huoshwa.
 
Gin imetolewa kwenye chupa haiwezi kurudi, ukurasa mpya umefunguliwa maana hata JK mwenyewe wabunge wanaweza kumcharukia kabla ya 2010.

Nimependezwa na hili bunge kwa kipindi hiki kifupi kwa kuweza kusema ukweli na kutetea walalahoi.

Bunge lina wabunge waachache sana (ukitoa wa upinzani) walio objective na proactive.Wengine waoga wanasoma mood, mpaka Slaa na Zitto apige weee, waue, Lowassa maiti ndiyo unawasikia.
 
Pundit, Kipande hiki kimefunga mjadala..

Hata hivyo kamati teule imetimiza wajibu wake kwa uwazi na ukweli kama ilivyoagizwa na Bunge letu tukufu. Kwa kuzingatia umuhimu wa nafasi aliyonayo Mheshimiwa Waziri Mkuu katika uendeshaji wa shuguuli za serikali na uongozi wa nchi nzima kwa ujumla, ni wajibu wake yeye mwenyewe kupima uzito wa matokeo ya uchunguzi huuu na wajibu wake kikatiba ndani na nje ya bunge. Vile vile ni wajibu wa Bunge ambalo linathibitisha uteuzi wake kwa mujibu wa Ibara ya 51 inayothibitisha uteuzi wake. Kuangalia ikiwa matokeo ya uchunguzi huu hayajaathiri hadhi na uzito wake ndani ya bunge.

That was the next step!

Hii ndiyo sheria ya Bunge na hatuwezi kubeba sheria za mtaani na kuzifungia kirago zikubalike!
 
Kuna mada nyingine wala hazikupaswa kuwa na urefu huu.The guy was corrupt,he resigned himself (nobody forced him out of the office),he had,and still has,several legal avenues to contest the findings if he felt he was treated unfairly by the bunge committee.Kwanini hii "DEFENCE YA LOWASSA" isiachwe mikononi mwake na kwa wanasheria wake?
 
Mlalahoi

JF Senior Expert Member Join Date: Thu Aug 2006

Kuna mada nyingine wala hazikupaswa kuwa na urefu huu.The guy was corrupt,he resigned himself (nobody forced him out of the office),he had,and still has,several legal avenues to contest the findings if he felt he was treated unfairly by the bunge committee.Kwanini hii "DEFENCE YA LOWASSA" isiachwe mikononi mwake na kwa wanasheria wake?
 
Hoja ilikuwa iwe 4 sided.
Richmonduli, Tanesco, Wizara ya fedha na Ofisi ya PM

Mwakyembe ameifanya 3 sided kwa kumwengua Lowassa na PM ofisi yake.

Tamati yake ni:

Lowassa alipindisha utaratibu ili kujineemesha Dr Mwakyembe naye kam bypass ili kumzukia kama mwenye na kumbana.

Mwosha huoshwa.

MADELA nimekuelewa,

Unakubali kuwa pigo limepigwa kimafia, sasa wanasheria ndiyo kitu wanachosema kuwa OK regardless kama Lowassa ana hatia au hana, pigo limepigwa kimafia na halikufuata misingi ya sheria ya kumpa kila mtuhumiwa nafasi ya kujitetea.
 
Kichuguu,'
Nasikia hata kule Musoma watu walikuwa wanasherehekea kuondolewa kwa Lowassa.
Watu walijua jeuri na ulafi wake.

Party itaanza wakimfilisi pesa aliyochota kwa uharamia wake.

Pundit

Mwanzo wa kutembea ni kutambaa.
 
Mlalahoi

JF Senior Expert Member Join Date: Thu Aug 2006

Kuna mada nyingine wala hazikupaswa kuwa na urefu huu.The guy was corrupt,he resigned himself (nobody forced him out of the office),he had,and still has,several legal avenues to contest the findings if he felt he was treated unfairly by the bunge committee.Kwanini hii "DEFENCE YA LOWASSA" isiachwe mikononi mwake na kwa wanasheria wake?

Mkuu ES,

Kwa sababu watu wanajali principle and this is beyond Lowassa.It is about the principles of rule of law and due process.Sasa tumempa Lowassa msemo kuwa "nimekuwa treated unfairly kwa sababu sijapewa nafasi ya kujitetea" unnecessarily.
 
Pundit

Unakubali kuwa pigo limepigwa kimafia, sasa wanasheria ndiyo kitu wanachosema kuwa OK regardless kama Lowassa ana hatia au hana, pigo limepigwa kimafia na halikufuata misingi ya sheria ya kumpa kila mtuhumiwa nafasi ya kujitetea.

"Hata hivyo kamati teule imetimiza wajibu wake kwa uwazi na ukweli kama ilivyoagizwa na Bunge letu tukufu. Kwa kuzingatia umuhimu wa nafasi aliyonayo Mheshimiwa Waziri Mkuu katika uendeshaji wa shuguuli za serikali na uongozi wa nchi nzima kwa ujumla, ni wajibu wake yeye mwenyewe kupima uzito wa matokeo ya uchunguzi huuu na wajibu wake kikatiba ndani na nje ya bunge. Vile vile ni wajibu wa Bunge ambalo linathibitisha uteuzi wake kwa mujibu wa Ibara ya 51 inayothibitisha uteuzi wake. Kuangalia ikiwa matokeo ya uchunguzi huu hayajaathiri hadhi na uzito wake ndani ya bunge".
 
Nasema mtu yeyote anayejali rule of law na due process ataona kuwa the basic tenets za fairness hazikufuatwa.

Mwananchi wa kawaida wa Tanzania hata hajui rule of law ni nini, sembuse ku care.

Nakubaliana na wewe kimsingi. Kuna vitu vya kuangaliwa hapa. Kwanza mategemeo ya wengi kuhusiana na tume yalikuwa ni kuja na conclusion yenye kuleta mwalifu fulani mwenye high profile. Na isingefanyika hivyo, hakuna ambaye angekubali ukweli wa mambo. Hivyo public opion ilisha-set matokeo ya tume.

Vile vile vitu kama hivi havijawahi kufanyika Tanzania. Pamoja na kuwa Mwakyembe alikuwa ni Prof. wa sheria hajawahi kufanya kazi ya namna hii na hakuwa na reference ya kuanzia. Hivyo kutakuwepo na mafungufu fulani. Lakini kwa tume zitakazokuja zitakuwa na reference. Hivyo Warioba ana ukweli ndani yake.

Tukija kwa upande wa kuitetea tume. Tume ilikuwa na haki ya kumwita mtu au kutomwita mtu. Tume hii sio mwendesha mashitaka ambaye anawajibika kupata ushahidi wa mshtakiwa. Kama walichotakiwa ni kutoa conclusion itakayoonyesha kukiukwa kwa utaratibu basi hicho kimefanyika. Kwani vithibitisho pekee yake vinajenga hoja nzito ya kukiukwa kwa utaratibu. Hivyo maamuzi ya tume ni tofauti na mahakama ambayo inataka mshitakiwa naye apewe nafasi ya kujitetea. Kwa mtu kama mimi mwenye trade nyingine inatosha kabisa kuunganisha dots na kupata conclusion lakini kwa mtu mwenye trade ya sheria kama mzee Warioba kumuhoji mtuhumiwa ni kitu muhimu.
 
Kuna mada nyingine wala hazikupaswa kuwa na urefu huu.The guy was corrupt,he resigned himself (nobody forced him out of the office),he had,and still has,several legal avenues to contest the findings if he felt he was treated unfairly by the bunge committee.Kwanini hii "DEFENCE YA LOWASSA" isiachwe mikononi mwake na kwa wanasheria wake?

Kuna issues za precedent, rule of law, due process na fairness ambazo ziko deeper than incident ya Lowassa.Hizi ni principles.
 
MADELA nimekuelewa,

Unakubali kuwa pigo limepigwa kimafia, sasa wanasheria ndiyo kitu wanachosema kuwa OK regardless kama Lowassa ana hatia au hana, pigo limepigwa kimafia na halikufuata misingi ya sheria ya kumpa kila mtuhumiwa nafasi ya kujitetea.

sasa pundit unatufanya watu wote wazima humu ndani vichaa.

since unangangania sana mambo a sheria, lets go;;;

kamati ni kama prosecutor, wamemcharge lowassa kuwa ni mwizi, then wamepeleka kwa judge hapa ni bunge ili lowassa awe defendant, bunge liwe judge na kamati iwe prosecutor.

sasa lowassa kahamaki hamna haki, ala vipi wewe uko mbele ya judge si ulete defense yako//

kama bunge lingepiga vote of no confidence bila kumsikiliza lowassa, then uonevu ungeweza kulalamikiwa.

uko hapo mkuu
 
Pundit, Kipande hiki kimefunga mjadala..

Hata hivyo kamati teule imetimiza wajibu wake kwa uwazi na ukweli kama ilivyoagizwa na Bunge letu tukufu. Kwa kuzingatia umuhimu wa nafasi aliyonayo Mheshimiwa Waziri Mkuu katika uendeshaji wa shuguuli za serikali na uongozi wa nchi nzima kwa ujumla, ni wajibu wake yeye mwenyewe kupima uzito wa matokeo ya uchunguzi huuu na wajibu wake kikatiba ndani na nje ya bunge. Vile vile ni wajibu wa Bunge ambalo linathibitisha uteuzi wake kwa mujibu wa Ibara ya 51 inayothibitisha uteuzi wake. Kuangalia ikiwa matokeo ya uchunguzi huu hayajaathiri hadhi na uzito wake ndani ya bunge.

That was the next step!

Hii ndiyo sheria ya Bunge na hatuwezi kubeba sheria za mtaani na kuzifungia kirago zikubalike!

Tatizo linakuja, in principle, ukileta ripoti bungeni, ripoti inayomnyooshea kidole Lowassa, na wewe hukuchukua muda wa kumsikiliza Lowassa anasemaje kuhusu allegations hizo, basically unaleta a one sided report.

Je wakuu mmesoma sababu zilizowafanya Mwakyembe na Seleli wasimuhoji Lowassa?
 
Pundit,
hakuna jambazi ama fisadi anayekubali kutendewa haki iwe ktk madai ama hukumu wakijua kwamba kukusudia ni makosa makubwa zaidi. Anachojaribu kufanya Lowassa ni kukosha jina lake na hakuna njia isipokuwa kutafuta sababu. Je, unaweza amni kuwa alikwisha iona report kabla hata haijafikishwa bungeni?.. na kuwa alimwendea JK kumwomba isifike bungeni.... haki gani kama sio nia yake kutowatendea haki wananchi... Huo muda aliotumia kujaribu kuipinga hii report angetumia kujieleza na nina hakika JK kisha hoji ama anafahamu zinga lote ndio maana kakubali kujiuzuru kwake laa sivyo JK asingekubali hasa mtu wake wa karibu EL. That is the fact na rais mara kibao kasema hatapenda kufanya makosa ya kuchukua tetezi na kuzitolea hukumu....

Na mbona Balali mmefikia kuondoa visa yake na kumwondoa madarakani hali hakuna mtu kwenda kumhoji..Yule mhandisi aliyefukuzwa kazi on the spot baada ya kuona tu jengo limeanguka Lowassa alihitaji maelezo ya huyo bwana?... acheni ndugu zangu hakuna mtu aliye juu ya sheria...Alifikiria hivyo lakini Mungu kamwonyesha yeye mwenyewe kwa uvivu wake wa kufikiri...Hakuhitaji kujiuzuru hata kidogo kama angeitaka haki.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom