In case You missed it: Watch Darwin's Nightmare!

Kwa kuwa mimi sio mtalamu wa IT, ningeupoad hapa maana mi ninayo soft copy au ningeweka link hapa ili iwe rahisi.
Lakini hata hivyo unaweza ukaingia kwenye piratebay (Download music, movies, games, software! The Pirate Bay - The world's most resilient BitTorrent site) ikishafunguka enter neno Darwin's Nightmare zitakuja options kadhaa kisha utachagua mojawapo unadownload ni kama 690MB tu. Ila lazima uwe unatumia torrent downloader ambayo nayo ni free unaweza download na ku install kabla ya kuanza ku download hiyo movie.

Good luck.
 
Kipindi kile mama mmoja wa Kiingereza alihojiwa kuhusu hiyo movie akiwa Uk, alisema "kuanzia sasa sitanunuwa tena minofu ya sangara inayoletwa ulaya ili kudhibiti hali inayoendelea ukanda wa ziwa Victoria". Je sisi Watanzania tulichukuwa hatuwa gani? Kuipiga marufuku movie? Kuwa-harass waliompokea director wa ile movie? Still najiuliza. Yaani Muingereza kawa Mzalendo kwa Tanzania kuliko Watanzania wenyewe.

Nakumbuka kipindi kile tulichukua hatua ya kufanya maandamano kupinga kile tulichoambiwa kuwa tumesingiziwa.
Wakati ule maandamano yalikuwa yanaruhusiwa!
 
Nakumbuka kipindi kile tulichukua hatua ya kufanya maandamano kupinga kile tulichoambiwa kuwa tumesingiziwa.
Wakati ule maandamano yalikuwa yanaruhusiwa!

ccm mwanza waliandamana chini ya usimamizi wa wakina jairo eti wanapinga kudhalilishwa kwenye movie kwamba wanakula mapanki.hadi ile movie wakawaonyesha wabunge..kikwete alilani sana. mia
 
Raisi alienda Mza kuwapa pole wanamza,wakati kweli mapaki ndo mboga yao huko buswelu,kahangala,igoma n.k
 
Ndugu wnaJF, filamu ya Darwin's Nightmare by Hubert Sauper ilileta kasheshe mwaka 2006 baada ya Rais Jkaya Kikwete kutembelea Mkoa wa Mwanza. Wanasiasa mbalimbali walionesha kukerwa na ujumbe wa filamu hii na kuwaita wale waliomsaidia mtunzi wake vibaraka. Lakini leo hii ujumbe wa filamu hii wa "kula mapanki wakati monofu ya samaki aina ya Sangara ikisafirshwa nje" una maana zaidi.

Angalia tu wavuvi wakubwa wanawapiga vita wavuvi wadogo. Kule Ziwa Victoria wavuvi wadogo hawaruhusiwi na wavuvi wakubwa kuvua maeneo ambayo samaki wakubwa wanapatikana. Wakati huohuo serikali inawataka wavuvi wadogo wavue samaki wakubwa na si wadogo (yaani, wavue samaki maeneo ambayo wakienda wanafukuzwa kwa kudhaniwa wezi au kutaka tu kulinda samaki wasivuliwe na wavuvi wadogo).

Ardhi inaporwa na wenye fedha, maskini wanabaki kuwa wapangaji na hata kama wangepewa ardhi muda wanaotakiwa kuwa wameiendeleza (ndani ya miaka 3) unaisha na pengine wanaweza kunyang'anywa kwa kuadaiwa kushindwa kuiendeleza na kuwapa watu wenye uwezo wa kuiendeleza (wenye fedha). Lakini kwa kipato watu wa chini walichonacho, je inawezekana mtu anatelipwa mshahara wa laki 2 au 3 na kusomesha watoto aweze kujenga nyumba ndani ya miaka 3? Fedha za umma na mali asili zinaporwa na wenye nacho na wafanyabishara wadogo wadogo wanabaki wakikimbizana na mgambo wa jiji kama panya na paka.

Hali ya maisha ni ngumu, ngumu, ngumu. Elimu hovyo... huduma ya afya na hduma nyingine za jamii hovyo na umaskini unaongezeka kwa watu wa chini wakati matajiri wanazi kuneemeka. Je, huku siyo sawa na "kula mapanki"?
 
Hakuna mapana yasiyo na mwisho. Ila kwa Tz mwisho utakuwa ni mbaya sana kwani watu wamevumilia kwa muda mrefu. Siku wakisema basi mbwai ni mbwai patachimbika. Bora kabla ya 2015 itafutwe namna ya kuwafanya wananchi wale minofu ya samaki na siyo mapanki. Mapanki haya yapo kwenye nyanja njingi sana. Kilimo vocha zinawafaidisha mawakala na wengine wachache. umeme bei juu hata hao wa mapanki hawawezi sasa kuwasha hata taa moja. Petroli nduyo hiyo hata daladala zitapandisha bei watakavyo. Shule nzuri ada juu. Hospitali nzuri malipo juu. Tutakwenda wapi? Jubu likikosekana ndiyo tutakapokuwa tumefika mwisho na kila mla panki atasema liwalo naliwe tumechoka. Mola wape hekima wahusika tusifike huko. Amin.
 
Hakuna mapana yasiyo na mwisho. Ila kwa Tz mwisho utakuwa ni mbaya sana kwani watu wamevumilia kwa muda mrefu. Siku wakisema basi mbwai ni mbwai patachimbika. Bora kabla ya 2015 itafutwe namna ya kuwafanya wananchi wale minofu ya samaki na siyo mapanki. Mapanki haya yapo kwenye nyanja njingi sana. Kilimo vocha zinawafaidisha mawakala na wengine wachache. umeme bei juu hata hao wa mapanki hawawezi sasa kuwasha hata taa moja. Petroli nduyo hiyo hata daladala zitapandisha bei watakavyo. Shule nzuri ada juu. Hospitali nzuri malipo juu. Tutakwenda wapi? Jubu likikosekana ndiyo tutakapokuwa tumefika mwisho na kila mla panki atasema liwalo naliwe tumechoka. Mola wape hekima wahusika tusifike huko. Amin.

Watawala wanajua hili haliwezekani. wamezungukwa na vyomba vya dola.
Ila Sudan, nakumbuka raia walipindua serikali ya kijeshi.
 
Wadau, kuna yeyote mwenye documentary ya Darwin's Nightmare (2004) - Hubert Sauper? Nmeitafta online, nmeikosa.... what was it all about hadi serikali ya Baba Riz ikaipinga ilhal 'mzungu' akijipatia misifa kibao ulimwenguni? Nidadavulieni jamani....
 
hyo documentary imefichua mambo mengi sana kuhusu ujinga ya serikali ya wa Tz nenda wikipedia wametoa maelezo ya kutosha au nikufanyie ku copy hapa au nenda youtube. Uka download
 
The film opens with a Soviet
made Ilyushin Il-76 cargo plane landing on Mwanza airfield in Tanzania, near Lake Victoria. The plane came from Europe to ship back
processed fillets of Nile Perch, a species of fish introduced
into Lake Victoria that has
caused the extinction of
hundreds of endemic species. Through interviews with the
Russian and Ukrainian plane
crew, local factory owners,
guards, prostitutes, fishermen
and other villagers, the film
discusses the effects of the introduction of the Nile perch
to Lake Victoria, how it has
affected the ecosystem and economy of the region. The
film also dwells at length on
the dichotomy between
European aid which is being
funneled into Africa on the one hand, and the unending
flow of munitions and
weapons from European
arms dealers on the other.
Arms and munitions are
often flown in on the same planes which transport the
Nile perch fillets to European
consumers, feeding the very
conflicts which the aid was
sent to remedy. As Dima, the
radio engineer of the plane crew, says later on in the film:
the children of Angola receive
guns for Christmas, the
children of Europe receive
grapes. The appalling living
and working conditions of the indigenous people, in
which basic sanitation is
completely absent and many
children turn to drugs and
prostitution, is covered in
great depth; because the Nile perch is fished and processed
for export, all the prime fillets
are sold to European
supermarkets, leaving the
local people to survive on the
festering carcasses of the gutted fish. At one point in the film a local
preacher, asked whether he
encourages condom use to
prevent AIDS, responds that he does not address using
condoms because having pre-
marital sex is an act of sin and
against God's law. Therefore
he preferred to preach to
people not to have sex before marriage. As to why the local
fish can't be sold to the
domestic market to counter
the impending famine (local
news reports relayed in the
film indicated Northern and Central Tanzania were facing
famine), one fish processing factory manager explains "it is too expensive
 
hiyo documentary inaonyesha ukweli tupu,mi nimekulia mwanza hayo mabaki ya minofi ya sangara(mapanki)yalikuwa yanatupwa maeneo ya igoma,mwanzoni yalikuwa hayana dili,yalikuwa yanaliwa na ndege fulani kwa jina maarufu Mabwana afya,hee wa2 wakagundua dili hilo,wakaanza kuwa wanakwenda kuyabeba kwenye baiskeli,wanayapeleka vijijini wanayabanika na kuuza au kubadilishana na nafaka,.mala biashara ikachanganya wale wa kiwandani badala ya kwenda kuya2pa wakaanza kuwauzia.Nilishangaa kuona eti serikali inasema watanzania tumedharirishwa!eti wa2 waandamane!!
 
hyo documentary imefichua mambo mengi sana kuhusu ujinga ya serikali ya wa Tz nenda wikipedia wametoa maelezo ya kutosha au nikufanyie ku copy hapa au nenda youtube. Uka download

Unawezaje kudownload kitu kwenye you tube? Saidia dugu mkuu
 
Wadau, kuna yeyote mwenye documentary ya Darwin's Nightmare (2004) - Hubert Sauper? Nmeitafta online, nmeikosa.... what was it all about hadi serikali ya Baba Riz ikaipinga ilhal 'mzungu' akijipatia misifa kibao ulimwenguni? Nidadavulieni jamani....

darwinsnightmareah3.jpg


Hii website poa sana mkuu on that movie.... DARWIN'S NIGHTMARE by Hubert Sauper
 
... kuna ukweli kabisa katika hii filamu. kama wanasiasa wa hapa Tanzania wanapinga hebu watuthibitishie jinsi gani nile patch walivyo ukuza Uchumi wa mwanza!
 
Blood diamonds, chocolate and child(slave?) labour aibu tupu kwetu na the west. However west have put into place mechanism to ensure diamond origin and cocoa is child/slave labour free.
 
Back
Top Bottom