Impact ya maandamano ya Chadema

Quinine

JF-Expert Member
Jul 26, 2010
21,271
47,271
Kuna baadhi ya wanasiasa na wanaJF walibeza maandamano ya Chadema kuwa hayatakuwa na impact yeyote, wengine wakadiliki kusema Chadema hawatapata watu Mwanza, lakini kadili siku zilivyoendelea yakatikisa anga lote la Tanzania hadi rais pressure ikampanda akaanza kulalamika kuwa kuna mpango wa kupindua nchi. Impact hiyo iliendelea kuwatoa watu ambao hatukutegemea kama kina Sophia Simba, Wasirra, Tendwa. Wengine tuliowasikia ni Fredrick Sumaye, Mzindakaya, Sitta, Lowassa nk. Hadi leo hii hata baada ya maandamano kwisha bado mtikisiko unaendelea kutikisa. Jana Pinda alipokewa na mabango yaliyoongelea maandamano ya Chadema. Hamuoni kuwa lengo la maandamano ya Chadema kisiasa limefikiwa. Nawauliza waliokuwa wanabeza wako wapi mbona hawaonekani tena au na wao wamekumbwa na impact ya maandamano, wanaona aibu.
 
Heshima mbele mkuu
Ni kweli impact ya maandamano na hotuba za CHADEMA inaanza kuonekana. Kuna rafiki yangu mmoja ni mtetezi mkubwa wa CCM. Lakini baada ya maandamano ya CHADEMA amekubaliana na hoja zao na amesema anapenda CDM waendelee na maandamano hayo.
 
Huwezi amini afisa elimu wa wilaya ya bagamoyo mr. Makuburi alitembelea shule moja ya msingi nakuongea na walimu cha ajabu alitumia muda mwingi kuwakoromea walimu kuchapa kazi ili CDM Wisipate la kusema hasa ukizingatia hapa ni kwa JK. kwa sauti ya chini walimu walikuwa wanasema peoples power, peoples power.
 
we hushangai hadi kwenye hotuba ya raisi mandamano yanaongelewa!
Ningekuwa mimi rais au msauri wake nisingeongelea maandamano ya CDM kwa sababu kuyaongelea ni kuyapa nguvu zaidi, badala yake ningesema serikali inafanya nini kupunguza makali ya maisha.
 
huoni mpaka mkuu ana wasiwasi ?nguvu ya umma inatisha hasa ukiwa unajua ukweli kwamba sasa hivi soko la kuuza sura limeisha
 
Serikali ilikuwa imelala sasa imeamka.Sasa kuna kazi ya kuilazimisha ifanye kazi maana bado ina usingizi.
 
Walidhani ni chama cha msimu bila kujua cdm ni chama kinachofanya kazi msimu wote unaoufahamu, iwe wakati wa jua au mvua, kinauelewesha umma wajibu wake kwa serikali na kazi za serikali kwa umma. JMK anatishwa kwani hana anachoweza kufanya kuondoa shida za watz na sasa badala ya kuzunguka angani ili tusilale njaa anashinda hewani kupiga picha na wapinga demokrasia
 
kweli mkuu naona baada ya tenzi za mkwere amani amani basi hao uliowataja wakaendelea na wimbo huo unaopoteaza umaarufu huku ule wa haki ukipata mashiko.Bravooo CHADEMA
 
Walidhani ni chama cha msimu bila kujua cdm ni chama kinachofanya kazi msimu wote unaoufahamu, iwe wakati wa jua au mvua, kinauelewesha umma wajibu wake kwa serikali na kazi za serikali kwa umma. JMK anatishwa kwani hana anachoweza kufanya kuondoa shida za watz na sasa badala ya kuzunguka angani ili tusilale njaa anashinda hewani kupiga picha na wapinga demokrasia
Kuna kitu umekisema kimenigusa kwenye bold, hivi rais badala ya kushughulikia matatizo ya ndani yeye anashinda nje kusuluhisha migogoro ya wengine, kwanini asiwaachie kina Zuma ambao nchi zao hazina matatizo makubwa kama yetu? au yeye kaona sifa kama unavyosema kuonekana amepiga picha nchi za watu. Next utasikia amekwenda kusuluhisha mgogoro wa Libya.
 
CCM wameamua kutumia media badala ya kwenda front... Hata Pinda aliyeenda front kupima upepo kakutana na hali halisi atatoa majibu sahihi kwa CCn kuwa wajiandae kuwa chama cha upinzani.
 
Ningekuwa mimi rais au msauri wake nisingeongelea maandamano ya CDM kwa sababu kuyaongelea ni kuyapa nguvu zaidi, badala yake ningesema serikali inafanya nini kupunguza makali ya maisha.

Sasa naona mambbo ambayo waliyataka CDM wananchi wanaanza kuyaelewa, ila watendaji wa Serikali yetu wana uwezo mdogo mno wa kuelewa mambo matokeo yake wanakurupuka na mambo ya hovyo hovyo yasiyo hata na tija yoyote kwa Jamii yetu.

CHADEMA iongeze nguvu zaidi katika maandamano hasa kwenye kanda ya KUSINI, NYANDA ZA JUU KUSINI, MAGHARIBI NA KANDA YA KATI ambako inaonekana wananchi bado wamejifunika Blanketi zito sana la KIDUMU wakati kumekucha na sisi Watanzania tunataka maisha BORA ambayo hatuyaoni japo tuliahidiwa miaka miiingi iliyopita.
 
Sidhani kama kuna sehemu maandamano ya cdm yameleta effect kubwa kama Mwanza. Mimi nimekuja Mwanza kupumzika yaani kila nikipita makundi ya watu yanadiscus weaknes za serikali, iwe kwenye daladala,mitaani,makazini na maeneo mengine. Mpaka mimi nimeamini cdm inawafungua watu wajue tunaibiwa na saiv Mwanza kuna awareness kubwa kwa watu na cdm waendelee haya maandamano ya fungua watu, ila sema kuna wale ndugu zetu wanaopinga kwa kigezo cha dini ya rais tu, hawa Mungu ndo atawafungua
 
Kuna baadhi ya wanasiasa na wanaJF walibeza maandamano ya Chadema kuwa hayatakuwa na impact yeyote, wengine wakadiliki kusema Chadema hawatapata watu Mwanza, lakini kadili siku zilivyoendelea yakatikisa anga lote la Tanzania hadi rais pressure ikampanda akaanza kulalamika kuwa kuna mpango wa kupindua nchi. Impact hiyo iliendelea kuwatoa watu ambao hatukutegemea kama kina Sophia Simba, Wasirra, Tendwa. Wengine tuliowasikia ni Fredrick Sumaye, Mzindakaya, Sitta, Lowassa nk. Hadi leo hii hata baada ya maandamano kwisha bado mtikisiko unaendelea kutikisa. Jana Pinda alipokewa na mabango yaliyoongelea maandamano ya Chadema. Hamuoni kuwa lengo la maandamano ya Chadema kisiasa limefikiwa. Nawauliza waliokuwa wanabeza wako wapi mbona hawaonekani tena au na wao wamekumbwa na impact ya maandamano, wanaona aibu.

CCM ni kama mgonjwa wa HIV aliye flash damu mara kadhaa baadaye mwili ukikataa dawa ni kifo tu
 
Back
Top Bottom