Imetokea loliondo

Wengi wamepona ati..........
DANCING.jpg
 
Si ajabu hata YESU alibatizwa na YOHANA MBATIZAJI ingawaje hakuhitaji huo ubatizo
 
hahahahaha inawezekana alishawahi kumtabiri sasa anaenda kumuangalia kama ndiye yy au la!
 
does this qualify to be a breaking news!... ?!! washirikina wameenda kukutana labda wameibiana majini.. hamna lolote! lete issue za maana hakuna dawa ya ukimwi! dawa ni kuacha ngono zembe NUKTA
 
NDOA moja iliyodumu kwa muda wa miaka mitatu imeingia matatani baada ya mke kudai talaka baada ya kugundua mumewe amekwenda Loriondo kwa siri bila kujua.
Ndoa hiyo inayoishi maeneo ya Chang’ombe imeingia utata mkubwa baada ya kuhisi mumewe ameambukizwa ukimwi na kumtoroka kwenda kwa babu kupata kikombe cha dawa ya Mchungaji Ambilikile.

Imedaiwa kuwa mke huyo amechachamaa kutaka talaka hiyo mara baada ya kwenda kituo cha afya na kupima afyaa yake na kujikuta hajapata maambukizi ya VVU.

Imedaiwa kuwa mke huyo alichukua uamuzi wa kwenda kuchukua vipimo hivyo baada ya kupata taarifa kuwa mumewe alikwenda Loriondo kunywa dawa hiyo na bila kujua maradhi anayosumbuliwa mumewe.

Imedaiwa kuwa mke huyo aliagwa na mumewe huyo kuwa anasafiri kwa muda wa wiki mbili kikazi mkoani Arusha na alishtushwa na mmoja wa rafiki zake alipofika nyumbani kwake kumuulizia mumuwe kama alikuwa amerudi kwa kuwa aliwaaga kuwa anakwenda kunywa dawa hiyo.

Imedaiwa mwanamke huyo alihamaki na kuanza kumuuliza maswali ya ya kiundani rafiki yake huyo ili aweze kumbainishia ukweli na aligundua kuwa walikwenda Loriondo na marafiki zake wawili, dada yake mmoja na shemeji yake na kumbainishia kuwa yeye alishindwa kwenda kwa kuwa hakuwa na nauli ya kutosha.

Imedaiwa kuwa mumewe aliporudi alianza kumuuliza kuwa alikuwa ameenda Arusha kikazi au alikuw a amekwenda Loriondo na mumewe kumjibu alikwenda kikazi ndipo varangati lilianzia hapo na kumbainishia kuwa alikuwa wamekwenda Loriondo na mumewe huyo kumbishia kwa asilimia miamoja

Hata hivyo mwanamke huyo alishikwa na wasiwasi mkubwa huenda mumewe alikuwa ameathirika na kumficha na alimsihi wakapime afya na mume huyo kuonekana hakuwa tayari kupima afya yake ndipo mwanamke huyo alipochachamaa kumt aka mume huyo kumpa talaka yake

Hata hivyo imedaiwa mwanaume huyo alikwenda kutoa taarifa hiyo kwa wazazi wa pande zote mbili ili waweze kumsaidia sakata hilo na kumtuliza mke wake asiendelee kuomba talaka na kumbainishian kuwa hakwenda Loriondo.
 
Hapa Waislamu hawana ujanja!! Wamelazimishwa kumtambua Yesu! Wanatibiwa kwa imani ya kikristo!! Halafu tusikie kesho wakiponda ukristo kuwa ni ukafir!!

Mkuu naomba nipingane na wewe! Toka binadamu wa kwanza kuletwa duniani(Adamu) Mungu ni yule yule! Tofauti za kiimani zilizopo sasa ulimwenguni zimetokana na wale wapokeaji wa ujumbe wa Mungu! Wapo walioamua kuchakachua ujumbe huo wa Mungu kwa personal interests, otherwise tungekua wote katika itikadi na imani moja.

Vilevile wapo wakristo ambao wanampinga Babu! Mmojawapo alisikika akisema toka asikie habari za Babu hakuwahi kumsikia Babu akitaja neno YESU. Babu huwa anamtaja Mungu! Hii imemfanya mama huyu mlokole awe na mashaka na amesema katu hatuthubutu kwenda Liliondo!

Kwa waislamu kuna maajabu mengi yameshaelezwa kuja kutokea wakati ambao inaaminika ni siku za mwisho kabisa wa Dunia. Case ya Babu wa Liliondo inashabihiana kwa karibu na baadhi ya cases zilizotabiriwa. Kwa muumin mzuri wa kiislamu, hii ni miongoni mwa mitihani ya Dunia, subra na kuzidisha ibada ndio njia pekee itakayokuvusha salama katika Dunia hii.
 
does this qualify to be a breaking news!... ?!! washirikina wameenda kukutana labda wameibiana majini.. hamna lolote! lete issue za maana hakuna dawa ya ukimwi! dawa ni kuacha ngono zembe NUKTA

Mkuu nimeipenda hiyo!! umenichekesha sana:lol:
 
Mkuu naomba nipingane na wewe! Toka binadamu wa kwanza kuletwa duniani(Adamu) Mungu ni yule yule! Tofauti za kiimani zilizopo sasa ulimwenguni zimetokana na wale wapokeaji wa ujumbe wa Mungu! Wapo walioamua kuchakachua ujumbe huo wa Mungu kwa personal interests, otherwise tungekua wote katika itikadi na imani moja.

Vilevile wapo wakristo ambao wanampinga Babu! Mmojawapo alisikika akisema toka asikie habari za Babu hakuwahi kumsikia Babu akitaja neno YESU. Babu huwa anamtaja Mungu! Hii imemfanya mama huyu mlokole awe na mashaka na amesema katu hatuthubutu kwenda Liliondo!

Kwa waislamu kuna maajabu mengi yameshaelezwa kuja kutokea wakati ambao inaaminika ni siku za mwisho kabisa wa Dunia. Case ya Babu wa Liliondo inashabihiana kwa karibu na baadhi ya cases zilizotabiriwa. Kwa muumin mzuri wa kiislamu, hii ni miongoni mwa mitihani ya Dunia, subra na kuzidisha ibada ndio njia pekee itakayokuvusha salama katika Dunia hii.

Walioenda Loliondo, hapo kwenye nyekundu - je ni kweli?
 
Loliondo kwa babu kuna mambo. Inasemekana kua mtu akishapata kikombe cha babu bila kutoa ushuhuda kwa ndugu jamaa na marafiki wa karibu uwezi kupona. Unatakiwa ushuhudie ulikua unaumwa nini, ulikua unajisikiaje kabla ya kikombe na je unajisikiaje baada ya kikombe. Mwisho wa siku mtu asiache kufanya hili kwani asipopona asimlaumu babu.
 
Mh hili ni shart la ngapi?
 
Aliyekuwa kichaa je? atasema kabla ya kunywa kikombe alikuwaje? - kwani anakuwa anajijua yukoje!
Kweli hizo ni tetesi tu za kijinga. Babu kila asubuhi anakuwa na briefing na kuruhusu maswali - nendeni mkamuulize.
 
Du! nadhani sasa LOliondo imejulikana East Africa nzima.
Imekuwa maarufu kuliko Bagamoyo.
 
Back
Top Bottom