Imethibitishwa na Serikali... Babu wa Loliondo ni Tapeli

kumbe hatuna serikali!!!. Kama MAWAZIRI ( W. LUKUVI NA WENGINEO), WAKUU WA MIKOA (KANDORO NA WENGINEO), WABUNGE (LOWASSA, MREMA NA WENGINEO) na wananchi wengine walipata kikombe na wengine kutamba majukwani kuwa wapo 'fiti' na wakati huohuo WIZARA YA AFYA KUPITIA NAIBU WAZIRI DR. LUCY NKYA (wakati huo) ikatangaza kuwa imethibitisha kuwa DAWA ya BABU inatibu na haina madhara yoyote, iweje leo wamgeuke. HAKYA MUNGU, BINAFSI NITAUNGANA NA MAWAKILI WENGINE KUMTETEA BABU.
 
Tatizo ni kuwa wakati babu alikuwa anatibu kiimani, wao wamefanya utafiti wa kisayansi... hivi ni vitu viwili tofautii
 
Mkuu mbona ueleweki kwa hiyo Babu wa Loliondo ni Chadema...unapinga kuwa sio tapeli?

Umeanzakuharibu thread eeee!!Kunasehemu mtoa mada ametaja Chama?Kazi zakutumwa shida sana!
 
Michungaji miongo imejaa sana waanze mfano kwa kumnyonga huyu halafu afuate askofu wake laizer kwa kutoa ushuhuda wa uwongo
 
Mbona sijasikia wakiwafuatilia wachungaji wengine waliowahi kusema wakiwaombea watu magonjwa yao watapona?

Au shida ni yeye kuambatanisha mambo yake na kikombe?

Wivu tu, wengine wamepona. Mbona shemeji yake mama niniliu alikuwa hoi kwa kisukari lkn tangu apate kikombe mambo byee, anagonga coca kama chekechea
 
Sidhani kama Mchungaji aliwalazimisha kwenda kunywa juice yake. Walienda kwa hiari yao. Tena aliwatahadharisha kuwa ni vema wawe na imani kama yake. Je imani ya wagonjwa imechangia kiasi gani kutoponywa na dawa hiyo?
 
Sheikh Ponda alikemea Waislam wasiende kwenye hii Shirki, Askof Laizer akaponda sana akaipiga Biti serikali isijaribu kumfungia Babu, Jk akasema 'mtoto akililia wembe mpe PANGA amalizie hasira zake',magazeti yalishoboka yakidhani ni ishu ya kidini kumbe Lowezi la Kinyakyusa lililokulia Uchagani!
 
Ule ulinzi, barabara safi kuelekea Samunge na huduma za mawasiliano zilizoboreshwa serikali ilifanya ikijua inasubiria utafiti ama ilikuwa kucheza na akili za watu? Kwa nini hawakumtia huyu babu hatiani?
Oh my God! Nchi hii ina nini jamani? duh madudu kila uchao na simulizi za alufulela ulela
 
SERIKALI ndiyo nini?.BABU alikuzwa na watu wengi hata Viongozi waandamizi walikwenda kwa BABU.Tena ripoti ya watu wawili kutoka Kitengo cha Tiba za Asili Muhimbili na AMREF zilionesha dawa ya babu ingeweza kutibu baadhi ya STIs na Kisukari.Zaidi Serikalihiyo hiyo ilifikia mahali pa kumpa Babu ulinzi maalumu.
Lazima kuna jambo Serikali ilitaka kufanya ikawapotezea mawazo ENYI BANTU BA TZ mkabaki mnashangaa kumbe mmepigwa bao.Kama changa la macho vilee!
Ni juu yetu kuibua kwa nini Serikali ilimshabikia BABU na sasa imemtelekeza?
Katika ulimwengu wa utafiti Gazeti ni chanzo DHAIFU MNO CHA TAARIFA hivyo wana JF tuwe machona magazeti aun tufikiri zaidi ya tuliloambiwa na magazeti!
 
magufuli aliamrisha barabara ichongwe, iweje umchongee barabara tapeli, kuna chunguzi za maana ambazo serikali inapaswa ifanye siyo kumaliza pesa zetu za kodi kwa kufany auchunguzi kama dawa ya babu ni kweli ama vipi, hivi kuna watu walifikiri kabisa ni kweli inaponya ukimwi
 
Utapeli wa Babu ni kidogo sana - aacchwe apumnzike kwenye hicho kinyumba na na kijigari alivyojipatia.

Hao majitapeli wa ukweli na uhakika wenye mabilioni katika akaunti za nje, wanaohujumu rasilimali za taifa kila kukicha na kuishi kama miungu wadogo mbona wako huru? Hawa ndio wanawaua watanzania kwa ufukara uliokithiri.
 
ndio mnashtuka leo,wakati kipindi kile mlikua mnatafuta misifa kwa kila mmoja kumwaga ahadi bwerere...yule aliyesema ataweka lami sijui alishafanya hivyo?
 
kwa mtizamo wangu Serikali ya ccm ndio matapeli kwani ndio waliompigia debe ingawa kuna watu kama Askofu Kakobe alitoa taarifa katika vyombo vya habari kuwa Babu ni tapeli na hana tofauti na DECI wakambeza na kumpuuza. sasa kiko wapi? acha wale matapishi yao ss wajanja hayatuhusu
 
Back
Top Bottom