Imethibitishwa na Serikali... Babu wa Loliondo ni Tapeli

Huu ni ujinga. Taarifa hii haina maana., haisadii chochote. Walikuwa wapi muda wote huo?

Watu wameshakunywa, then mnatoa taarifa, ina manufaa gani?

Kwa uvivu wa kufikiri, hakuna suluhisho linatolewa. Je, ukiachana na babu, ambao wamekunywa, wanapewa maelekezo gani sasa? Wanaelezwa nini?
 
Sawa, ni kweli haya yote yameshatokea, watu wamekunywa dawa na hawajapona, wengine wameshadead mda tu. Swali linakuja Nani wakulaumiwa hapa. Kati ya
(i) Babu,
(ii) Serikali,
(iii) Wananchi waliokuwa na imani juu ya tiba itolewayo na Babu.
Tutafakari!!

Hapa wa kulaumiwa ni wananchi wenyewe !!
Mimi nilishangaa sana, watu na akili zao timamu, na usomi wao wote, wanadanyanywa na kuuziwa 'juice' ya mizizi, eti inatibu magonjwa matano !!
Dawa yenyewe ina masharti kuwa lazima unywe huko-huko Loliondo, Yaani ukitoka nayo nje ya eneo la Loliondo, basi, haifanyi kazi !!?? Na kama hiyo haitoshi, unaambiwa eti dawa hiyo ili ifanye kazi lazima uwe na 'imani' !!
Hapo mtu na akili zake timamu anakubali na kuamini !!!
 
alisema"TIBA YAKE INAKWENDA NA IMAN YA MTU"...hapo ndio atakapowapigia bao wanaotaka kumshita.....yes_no imani...hakuna kupona...lo!

Oh yes mkuu! The oldman said it loud and clear!Labda ashtakiwe kwa ubabe tu na kuhukumiwa kwa ubabe.
 
Daaaa babu kwisha habari yako!

Sasa filamu ya babu wa loliondo ndio season 2 imeanza!
 
Muulize William Lukuvi, Dr. Magufuli na Omar Mahita walikwenda kwa babu kufanya nini

Kwani Ndesamburo alikwenda kwa babu kufanya nini...ukweli utabaki kuwa ukweli babu ni Tapeli la kimataifa.
 
Hapa wa kulaumiwa ni wananchi wenyewe !!
Mimi nilishangaa sana, watu na akili zao timamu, na usomi wao wote, wanadanyanywa na kuuziwa 'juice' ya mizizi, eti inatibu magonjwa matano !!
Dawa yenyewe ina masharti kuwa lazima unywe huko-huko Loliondo, Yaani ukitoka nayo nje ya eneo la Loliondo, basi, haifanyi kazi !!?? Na kama hiyo haitoshi, unaambiwa eti dawa hiyo ili ifanye kazi lazima uwe na 'imani' !!
Hapo mtu na akili zake timamu anakubali na kuamini !!!

Hapo kwenye red hapoo, ina maana hata watafiti wa NIMRI na wengine wamepata false results kwa kuwa wameipeleka dawa nje ya eneo husika. Na je, walipoichukua kwa ajili ya utafiti walipata ruhusa ya babu?
 
Du sasa na viongozi wetu waandamizi si walikimbilia huko? Kweli kile kikombe kilitufundisha mambo mengi!! Si na viongozi wetu waandamizi wachache walituambia kuwa ni ruksa kunywa? Sasa wanataka kumkamata wakati matamshi ya viongozi wenyewe yalichochea wingi wa watu kumiminika kule kwa babu Masapila!!??
 
Babu yuko na Toyota land-cruiser Hardtop mpya watamshikia wapi??
 
Huyo mchungaji aliwatahadharisha wananchi kuwa wasiache kutumia madawa yao ya hospitali. Kwa uzembe wa Serikali na wakapuuza ushauri wake wa katazo wakaenda kwa kasi kubwa. Leo wasimulaumu kwa kuwa alitoa tahadhali sisi watu makini hatukwenda, lakini pia bei ya dawa yenyewe ilitia mashaka. Wamuache babu wasimuletee shida, maana hata Prof. Maji Marefu baada ya kutapeli watu sasa hivi ni Mbunge mbona hamjapiga kelele. Serikali DHAIFU.

Unashauri kuwa Babu pia ateuliwe kuwa mbunge?
 
Tapeli huyo wa Loliondo alifikia hatua ya kutoa mahsrti kuwa mtu yoyote atakayeruka foleni, hatapona hata akinywa 'dawa' yake.
Watu wakazidi kukubali kudanganyika !! Wala hawakushtuka kuwa jamaa alikuwa amebuni chanzo cha kukusanya 'mafao' yake ya uzeeni !!
Saa hizi jamaa yuko 'fresh' kabisa, kishakusanya takribani Tzs. billioni tatu....
 
Afadhali imedhihirika hivo,nilikosana na jamaa zangu kwa kuwaambia huu ni utapeli tu.
 
Kweli hapa Serikali Hatuna. Yaani kama ingekuwa ni sumu mpaka leo ndio serikali inastuka, je wangekuwa watu wangapi wamepoteza maisha?

Angetangulia ahera mkuu wa kaya kwani ndo alokuwa wa kwanza kunywa kikombe.
Hivi ktk safari zake za nje zote kakosa ujanja wa kubadirisha damu kama wenzie wanavyofanya?
Kweli kichwa nazi ni nazi tu!!
 
Hapo kwenye red hapoo, ina maana hata watafiti wa NIMRI na wengine wamepata false results kwa kuwa wameipeleka dawa nje ya eneo husika. Na je, walipoichukua kwa ajili ya utafiti walipata ruhusa ya babu?

Hilo sharti la 'kutotoka na dawa nje ya Loliondo' ndio lilikuwa sharti kuu la kuwezesha wagonjwa 'kupona'.
Hapo ndio uongo wake ulipokuwa wazi kabisa.
Watu ilibidi washtuke hapo, maana, haiingii akilini kusema kuwa 'dawa' haifanyi kazi nje ya Loliondo, halafu dawa hiyo-hiyo ichukuliwe ikachunguzwe nje ya Loliondo !!
Hatimaye, NIMR wakatoa tamko kuwa 'dawa' haina madhara !!
 
Binafsi ntajitolea kumtetea babu huyu kwa sababu zifuatazo
1:Serikali imeshindwa kuwatimizia wananchi mahitaji yao mpaka wanahangaika kutafuta tiba mbadala.
2;Uchumi wa samunge umepaa, kwani ikumbukwe hata barabara ilikua hovyo
3:Mawasiliano yameimarishwa ,saa hizi samunge unatwanga kotekote
4:Vijana walijipatia ajira na kutengeneza mitaji
5:Viongozi waliwashawishi wananchi waende kupata kikombe wakati wakijua wao Role models
6:Babu Alisema wazi wenye Imani ndio watapona,Hivyo imedhihirisha wananchiwengi wa TZ hawana Imani:Mf; Nna rafiki yangu yeye ni mgonjwa wa kisukari,aliniambia hajapona sukari,ila maumivu aliyokuwa akiyapata mwanzo,hadi leo hii hayapo tena.Pia kuna watuwengine waliniambia,wakiwa na wake zao Vigongo vyao vimeongeza performance mara dufu.Hivyo inaashiria hawa walinda na Imanio Haba kujaribu.
7:Babu aliwashauri pamoja na dawa yake waendelee kutumia na hizo nyingine hadi unapopita muda,wao wakaacha.Hilo la kuvunja masharti tu,watu waliisha haribu dozi.kwani hata hizi za kitaalam zina masharti pia.huwezi pewa dawa ya siku saba,wewe ukanywa sikumbili au tatu ukaacha utegemee kupona.
8:serikali ilinufaika na biashara ya utalii,na fedha za kigeni kwani wateja wa nje ya nchi pia walikuja samunge.
9:tuliweza kufahamu juu ya ile nchi ya waarabu iliyopo pale Loliondo,kupora rasilimali zetu.
10:watanzania waliweza kufanya Utalii wa ndani ambao,umekuwa ni adimu kwao.
11:CCM walinufaika na kupungua kwa mjadala,wa Dowans na Uchaguzi, hivyo wao wanapaswa kuwa wa kwanza kumtetea na ndio wamenufaika zaidi.lakini kama ilivyo ada kwa CCM wakiisha kutumia hawana haja na wewe,kwani wao huamini kuwa"Mavi ya kale hanuki"
n.k,n.k
My take;Mema aliyofanya babu ni mengi kuliko hata mabaya ,mbayo kwanza naami hayapo,zaidi tu ya ya ile foleni ya kihistoria.
 
Back
Top Bottom