Imani yetu kwa serikali ya Kikwete

Bado una imani na serikali ya Kikwete?

  • NDIYO (YES)

    Votes: 215 19.4%
  • HAPANA (NO)

    Votes: 834 75.1%
  • Sijui (Undecided!)

    Votes: 64 5.8%

  • Total voters
    1,111
"Kila kitu kimefanywa na wewe. Wee ndiye ulokutana na huyo rafiki yako. Wee ndiye unaotueleza kile alichosema rafiki. Baada ya kutueleza hivyo, ni juu yetu sie kuamini au kutoamini hayo ulotueleza. Huna haja ya kumlazisha mtu aamini kile ulichokisema wee pamoja na huyo rafiki yako. Na pia huna haja ya kumtukana mtu. Umetumia kipimo cha aina gani hata ukagundua kiwango cha akili alonacho malaria sugu????"
Asante kwa Kuchangia baba mtu, tarehe 31 october usisahau kumpigia Kura ya Ndio Dr. Wilbroad Slaa
 
Wakuu juzi nilisikia kati ya ahadi zake kule Mlandizi ni kuwa amefanya mazungumzo na waisraeli kuja kulima nyanya kwenye bonde la mto RUVU.
1. Je hii inawezekana au ni ghiliba tu za mkulu ili apate kura?
2. Je anafahamu kuwa huo mto ni chanzo cha maji yanayotumika Bagamoyo, Dar na Kibaha na kwamba uwekezaji wowote mkubwa katika secta ya kilimo ungeathiri maisha ya watu wengi wanotegemea mto huo?
3. Je anafahamu madhar ya kimazingira yanayoambatana na matumizi ya viatilifu katika kilimo (kemikali)?
4. Je at what point of the river hicho kilimo kitafanyika?
5. Je kwa nini NAFCO walishindwa kuendesha mashamba yale ya zamani?
6. Je Kikwete anatumia ujinga wa ndugu zake kuwadanganya ili apate kura wakati akijua fika kuwa anawadanganya?
7. Je kwa style hii ya ngonjera za ahadi za kikwete tutafika?

Mungu ibariki Tanzania

Duh Jk Kiboko, hadi kwenye nyanya anaita wawekezaji? imebaki kuwahalalisha wachina wanaouza Maua Kariakoo!
 
Nafikiri hili siyo jambo geni!asilimia kubwa ya watanzania wanalifahami hili,hata wenzetu walio CCM wanalifahamu hili!Wakati umefika tufanye mabadiliko!
 
Nafikiri hili siyo jambo geni!asilimia kubwa ya watanzania wanalifahami hili,hata wenzetu walio CCM wanalifahamu hili!Wakati umefika tufanye mabadiliko!

ni kweli mkuu, nasikia mikutano ya ccm licha ya kuwabeba watu kwenye malaori .....mahudhurio yamekuwa na kwamba watu huwa wanafuata muziki wa wasanii waliochoka kimaisha na si kusikiliza sera!
 
kuna washauli wake wanamhalibia jamani mi naona kama siyo akili yake vile! na usisahau Reli toka tegeta mpaka posta, barabara za juu ameludia tena. WATAKAO MCHAGUA VILAZA SANA HAO BORA YA YEYE!
Muda mwingi aliutumia kwa safari za nje zisizo na tija na kusahau kazi yake ya msingi.Ulimwengu wa sasa wa mawasiliano ya kisasa kama video conference nakadhalika yangemrahisishia kazi na kupunguza gharama,bado ana mabalozi,na waziri wa mambo ya nje.Sijui kama Raisi wetu amejifunza kitu toka kwa wananchi anaongoza,Wananchi hawadanganywi kama mtoto mdogo na peremende,wanataka Raisi afanye kazi ya Uraisi sio kazi ya vipeperushi.Ni bahati mbaya atakumbukwa kama Raisi aliyetoa ahadi nyingi nakushindwa kuzitekeleza kifasaha.
 
Juzi nilikuwa na rafiki yangu mmoja ambaye anafanya kazi usalama wa taifa! tulikuwa tunabadilishana mawazo kuhusiana na uchaguzi wa mwaka huu, dakika za mwisho kabla ya kuachana nilifurahi nilipoona jamaa kakiri mbele yangu kwamba " Anatambua ya kuwa watu wengi wamepoteza matumaini na serikali iliyoko madarakani" na huo ndo ukweli!

Blanket statement, na ni personal opinion of which he is entitled to. Halafu, kwa nini mtu asitetee nafsi yake...........???
 
Jambo la dowans,iptl,sh kushuka thamani,rada,mabilioni ya jk,mfumuko wa bei,umeme kupanda bei,mikataba mibovu ya madini,safari za nje
 
Bunge limejaa wachumia matumbo. Hawajali mwelekeo wa nchi. Wanachojali ni 12 million per month. A few (48) MPs would stand up for that. Mnyika peleka hoja utaona yatakayotokea
 
Tusubiri bunge jingine lakini siyo hili la sasa lenye kuweka maslahi ya Chama mbele kuliko maslahi ya nchi
 
jamaani hiyo kura ipigwe na nani labda 48MPs ndo nawakubali ila wale wengine woote ni vimeo wanasinzia tu kwenye viti kusubiri noti mwisho wa siku. mwisho wao uuupo tu piga ua.
 
Halafu wakishamtoa JK nani aongoze nchi?Mbowe/Slaa,Zitto, Mnyika au Mdee?kwa akili yenu JK ndo kasababisha mfumuko wa bei?ili umsaidie nini?tafuteni suluhisho sahihi la matatizo si kulaumu mtu binafsi kwenye suala kama hili.Imeshakuwa wimbo sasa kila kitu JK?Kumuondoa Jk si suluhisho.
 
Wasipokuwa na IMANI NA MKUU WAWE TAYARI KUACHIA UBUNGE. HIYO NI KWA MUJIBU WA KATIBA YA JMT. RAIS AKITOKA UCHAGUZI UPYA PYAAA KWAO WOTE. HAWAKO TAYARI KUKOSA U MP HASA WALE WALOCHAKACHUA.
 
Halafu wakishamtoa JK nani aongoze nchi?Mbowe/Slaa,Zitto, Mnyika au Mdee?kwa akili yenu JK ndo kasababisha mfumuko wa bei?ili umsaidie nini?tafuteni suluhisho sahihi la matatizo si kulaumu mtu binafsi kwenye suala kama hili.Imeshakuwa wimbo sasa kila kitu JK?Kumuondoa Jk si suluhisho.

Nakubaliana na wewe, kumwondoa JK siyo suluhisho kabisa. Suluhisho sahihi ni kuiondoa CCM katika mamlaka ya kuongoza nchi ngazi zote maana tatizo ni mfumo mbovu ulioasisiwa na unaoendelezwa na CCM. CCM is our no. 1 enemy to our development and prosperity.
 
Isn't Tanesco a business entity? If it's, let us separate it from political decision making and run it as any other business enterprises.
 
Wabunge wenyewe wakishamaliza kupiga kura warudi majimboni / uraiani wakaanze upya maana hawatakuwa Wabunge tena mpaka uchaguzi mpya.
 
Back
Top Bottom