Fundi Mchundo
Platinum Member
- Nov 9, 2007
- 8,940
- 6,854
Naomba thread hii iunganishwe na ile ya Sanda Matuta iliyopo kwenye Habari mchanganyiko na ihamishiwe kwenye Jukwaa la Siasa ili ipate a bigger audience. Hii ni kwa sababu hii ni imani inayotugusa jamii nzima na inabidi ikemewe kwa juhudi na nguvu zote. Kama mambo kama haya yanaweza kufanyika Dar es Salaam huko vijijini ni wangapi wameonewa, wamedhulumiwa na wengine hata kupoteza maisha yao kwa imani kama hizi? Wote tunajua ni wengi sana maana kila kukicha tunasikia hadithi za watu ( mara nyingi bibi vizee ambavyo bila shaka vimeanza kupata matatizo ya Alzheimer) wakishikwa ati wanga kwa sababu wamekutwa wakitembea bila kujisitiri usiku na magazeti yetu kushabikia bila mtu kuthubutu kuyapinga. Imani hii imejengeka sana hata kwa wale wanaojiita wasomi. Tabia hii inabidi ikome ili kila mmoja wetu katika jamii aweze kutendewa haki sawasawa na wengine.