Elections 2010 I'm done with Kikwete! - Say NO to Second Term!

Mkjj,

Tuambie hiki kijalida tunakipataje ili tuanze kukisambaza hapa Mwanza, Mara na hapa Shinyanga? Nitatumia gharama zangu Mkuu.

Naomba ufafanuzi Mkuu
 
Ni matatu lakini Unachosema ni kimoja. you are out till he is out (kikwete). Hilo la mtu kufikia 11,000 kwa vile umeweka neno "au" i take it as closely related. To retreat yes! kwa wote tunahitaji from time to time, lakini timing yako ndio inanipa hofu. The 12th of October is very close and i believe that the start to 2010
 
Hakika jk hatufai watanzania na hili limejitanabaisha leo. Mkakati wa mwanakijiji wa kuimarisha kijarida cha cheche za fikra ni hakika na kweli. Right spika 6 angekuwa ndo rais tungepeta kwani hakika hakuridhishwa na hayo maongezi ya masaa ma4 ya rais wake.

Mmkjj nakuunga mkono ila usikae likizo ya moja kwa moja uwe unajitokeza japo kusema hi
 
watu mnasahau kuwa tz haijengwi na jf pekee

kwani tanzania ina watu wangapi ? Wangapi kati yao wana weza kusoma na kuandika wangapi wana access ya mtandao

jf ina wanachamba wangapi waliojisajili na kuchangia mara kwa mara ?

Ukifanya hilo jibu unalo

mimi mailing list yangu ina wanachama karibu 7060 ambao nina badilishana nao mawazo kila siku wengi wako tanzania ni wafanyakazi haswa wa sekta binafsi
 
Poleni wote waliyotegemea JK kusema kitu cha maana. Huyo jamaa ni msanii na ataendelea kuwa hivyo mpaka mwisho wake.
 
...Autopilot or not, ni wajibu wake kutimiza sera za Chama chake, chama cha Mapinduzi. Kama Kikwete hafai, inamaana serikali ya CCM haifai. CCM ndio iliyomchagua Kikwete awe mgombea wake. Watanzania, kwa matarajio ya wengi, CCM pekee ndio inayoonekana ni chama makini kuongoza nchi nzima. Hata akitoka Kikwete atayeteuliwa na CCM ataendelea kupeta tu kwenye uraisi.

...CUF wanakubalika Pemba, CCM wanakubalika Unguja na almost Tanzania nzima, Chadema bara hasa mijini, UDP shinyanga etc etc, huu sio ushindano mahiri, labda Opposition waje na coalition yenye nguvu na umoja wa kitaifa.

...nikiangalia Economic performance ya serikali ya JMK nadhani bado wanajitahidi; ahadi za ARI, NGUVU na KASI MPYA kwa kweli zilikuwa hyped tu,


Tanzania is expected to increase its rate of economic growth this year from last year's 7,3% and to get inflation below the average 2007 level of 7% by mid-2009, the finance minister said on Thursday.

In an economic survey presented to Parliament ahead of his 2008/09 fiscal budget speech, Mustafa Mkulo predicted the rate of growth would rise steadily in each year up to 2011.

"The economy will grow by 7,8% in 2008, 8,1% in 2009, 8,8% in 2010 and 9,2% in 2011," he said in the survey.

Mkulo said the East African country's GDP grew 7,1% in 2007, compared with 6,7% in 2006, led by telecommunications, financial services and construction.

"Inflation will be kept below 7% by the end of June 2009," he said. Average inflation in 2007 was 7%.

Mkulo's forecast comes at a time when high food and oil prices are eating into economies worldwide, and this could be a challenge to growth as it fuels high inflation.

"We expect inflation to stay above 5% largely due to high global oil prices," he said.

The government had targeted average inflation at below 4,5% by the end of the current fiscal year. It will be at 7% in 2008/09, Mkulo said, adding that average inflation stood at 7% in 2007, compared with 7,3% in 2006.

Annual inflation stood at 9,7% in April, up slightly from 9% in March and 6,1% last April, according to figures from the National Bureau of Statistics.


......au kipimo cha jumla cha uraisi ni kuwashikisha adabu wazembe wazembe? sidhani. Tutake tusitake watanzania wengi NDIVYO TULIVYO! tunaoneana haya sana inapokuja suala la uwajibishwaji

...kama nchi ipo kwenye AUTOPILOT na bado kuna amani na usalama, na takwimu hizo hapo juu zinaonyesha stability and growth kwenye economy, naamini wanajitahidi.

anyway, labda leo nimeamka na mtizamo chanya zaidi!
 
Mhhhh! Tusemeje!

Ni mchezo wa kuigiza na usanii ,tupu haswa ukifanyikia kwenye jumba takatifu la bunge.
 
Kitila, kwa kweli baada ya kusikilia hotuba hii umenifanya niwe upande wako; Kawaida yangu siyo kwenye siasa tu lakini hata katika maisha ya kawaida napenda kuamini kuwa wanadamu ukiwapa nafasi ya kufanya wema watafanya wema; Nimejifunza kumpa mtu nafasi ya kukosea na kujisahihisha. Nimejifunza kutokuwa na hukumu kali sana kwa mwanadamu mwingine.

Lakini katika hilo pia nimejifunza kuwa kuna mipaka isiyovukwa na kuna mambo ambayo mtu hatakiwi kupewa nafasi ya pili. Kwa muda mrefu sasa nimekuwa nikiamini kuwa somehow Kikwete atajikuta anakaa peke yake na kujikuta yuko peke (alone and lonely) na kutambua uzito alionao wa kuliongoza Taifa. Nimekuwa nikitumaini na kuombea kuwa Kikwete atatambua wajibu wake mkubwa na kuamua kufanya kile ambacho viongozi wa kweli hufanya.

Hivyo mara kadhaa (wakati Baraza limevunjika) niliamini kuwa JK atasimama na kuuteka wakati na hivyo kuanza upya; haikutokea hivyo. HIvyo hotuba hii jinsi ilivyopambwa na kutokea kwake wakati na saa kama hii niliamini kuwa labda amejifunza kitu na sasa yuko kweli anataka kufanya kitu; nilikuwa nimekosea.

Kikwete hawezi kuongoza; Kikwete si kiongozi ni mwanasiasa mpiga porojo; Kikwete si kiongozi ambaye Watanzania walitarajia kuwaongoza kutoka kwenye kilindi cha umasikini kuelekea kwenye mafuriko ya mafanikio. Rais Kikwete na niliandika wiki mbili zilizopita ni mtu ambaye amepewa nafasi nyingine kufunga goli ambapo amebakia yeye na golipa na mara zote amekuwa akifika golini anabakia kukaa chini na kusubiri mtu mwingine aje ampasia afunge goli wakati mashabiki wamekaa pembeni wakishangalia na kuombea afunge kwa sababu ni Kapteni wa timu na alinunuliwa kwa bei kubwa.

Unaposhinda uchaguzi kwa zaidi ya asilimia 80 unaweza kabisa kusababisha mabadiliko makubwa ya Kitaifa na kuongoza Taifa. Unapopata support ya watu wa mjini na kijijini, maskini na matajiri unakuwa na mtaji mkubwa wa kisiasa ambapo ni wewe tu unajua ukiuwekeza vizuri utalipa. Lakini kwa kushindwa mikakati, kugwaya, kuogopa kuudhi watu n.k unabakia na mtaji huo ambao pole pole unazidi kumemenyuka.

Kikwete ni kilele cha kukatisha tamaa na mfano dhahiri wa nini kiongozi asiwe. Kikwete anasimama leo hii kama kiongozi ambaye ameshindwa kuongoza na anabakia kuitwa kiongozi. Rais Kikwete amebakia kuwa yule mwenye "simba wa kuchora" ambaye anasimama kuunguruma kwenye picha na watoto wanabakia kucheka.

Leo kwa hakika ilikuwa ni nafasi nzuri kwa Rais Kikwete kuonesha uongozi Tanzania badala ya kupiga zogo. Kama alitaka kuelezea hali ya Muungano wetu na ya Taifa yetu alikuwa na wakati mzuri pale Aprili 26, Mei Mosi, Nane Nane n.k au kila mwanzoni mwa mwaka kama wanavyofanya Wamarekani. Lakini hili la kuiweka roho juu nchi na kwenda na magwaride na uongozi mzima wa serikali kwenye hotuba maalumu ya Rais Bungeni ni kuchezea hisia za wananchi. Ni kutuzuga kulikotukuka ambako kwa hakika kunamfanya astahili kupewa nishani iya Uzugaji uliotukuka daraja la kwanza na la pili!

Rais anapoenda kuzungumza Bungeni iwe kwa kweli jambo muhimu, zito, na ambalo kwa hakika linastahili mahali kama hapo. Kusimamisha shughuli za Bunge ili uje upigiwe makofi na saluti wakati mijadala muhimu ya Taifa inaendelea ni kuwapotezea muda wananchi na wabunge. Hotuba yake jinsi alivyoitoa ingeweza kutolewa na Makamu wa Rais, au Waziri Mkuu au hata Salva Rweyemamu! Haikuwa hotuba inayoendana na Urais kwani kwenye suala muhimu la Muungano alitakiwa kutoa msimamo badala ya "kuwaomba" viongozi wenzake.

Kilichodhihirika ni kuwa kama tunataka kuleta mabadiliko ya kweli, kelele za hapa mtandaoni zinapoteza muda na kwa hakika hazifiki kunakotakiwa. NI kwa sababu hiyo nimeamua kutilia mkazo na nguvu zangu zote kwenye kukiendeleza kijarida cha Cheche ambacho nataka kiwe ni nguvu ya kupambana na ufisadi na hata ikibidi kutoka kila siku bure nitafanya hivyo. Nataka kuhakikisha kuwa mwananchi wa kawaida anapata access ya mawazo na fikra nzito, na hoja zenye nguvu ili ziweze kuteka fikra zake.

Ni kwa sababu hiyo, naamua kuchukua likizo isiyo na muda ya kuachana na JF na kutilia mkazo uwanja mpya wa mapambano ambao ni fikra za wananchi wa kawaida wasio na mtandao. Tumeanza kuwafikia wiki hii iliyopita na tunataka tuwafikie zaidi sasa. Kuendelea kujibishana hapa JF na kulumbana na kubezena na kuwashiwishana ni kupoteza muda kwa sababu naamini hakuna watu ambao wako so informed kuhusu nchi yao kuliko watu wa JF. Nadhani hapa tumebakia kuhubiri kwa wanakwaya wetu na tumeendelea kuimba pambio ndani ya kanisa. Tunachofanya sasa hapa ni kuendelea kufanya maulidi kwenye madrasa! Lazima tutoke humu na kwenda kuwa mwanga na nuru kule nje.

So, I said it, tulifanya makosa tulipomchagua Kikwete na ni wajibu wa kila Mtanzania anayeitakia nchi mema, na ambaye anataka Taifa jipya, la kisasa, la kizalendo na lilo nona kwa mafanikio kuwepo kufanya kila awezalo kuhakikisha kuwa Kikwete na maswahiba wake hawarudi tena Ikulu 2010 na kuvunja huu uigizaji wa uongozi unaofanywa nao. Sidhani kama kuna kitu chochote ambacho Kikwete atakifanya sasa ambacho kitanifanya nimpe nafasi nyingine ya kumuamini.

I'm done with him. Kesho naanza likizo toka JF hadi mtu mwingine atakapofikia post 11,000!!! au unless Kikwete resign!


MwanaKJJ pole sana .Mkuu siamini kama kwamba bado uliamini kwamba JK could have came up with a serious Hotuba .Maana hana record ya ktenda wala kuwa hotuba ya utendaji wake kuanzia akiwa Mjumbe wa nyumba kumi na michezoni na hata ndani ta CCM , Mbunge na waziri na sasa Rais .Matendo ya JK ni reflection ya wana CCM na washabiki wao .
 
Lunyungu... wakati ya Young African (labda na hapa) niliwahi kuandika kitu ambacho nilikiita "Hotuba Kikwete angetoa". Hadi hivi sasa sijaona hotuba ya aina hiyo...
 
Hakuna hata sababu ya kusubiri mpaka 2010. Ajiuzulu sasa hivi maana nchi imemshinda...


Ni rahisi kuvunja muungano kuliko Kikwete kukubali kujiuzulu! Sasa cha kufanya ni kuuvunja Muungano ili kusiwepo na kitu kinachoitwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania!

waZanzibar (Raza, Shamhuna, ..) tusaidieni kutekeleza mpango huu!!
 
Mzee Mwanakijiji,

Asante sana kwa hii article. Wala hii si ku-retreat. Katika mapambano yeyote kuna wakati tunahitaji TACTICAL changes to achieve our Objectives. Tuko pamoja kwenye Cheche. Kuna jamaa zangu wengi tu hawana kazi ambao niko tayari kuwalipa wasambaze hiki kijarida bure. Kwa sasa tunasambaza mikoa ya kati.
 
Ni rahisi kuvunja muungano kuliko Kikwete kukubali kujiuzulu! Sasa cha kufanya ni kuuvunja Muungano ili kusiwepo na kitu kinachoitwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania!

waZanzibar (Raza, Shamhuna, ..) tusaidieni kutekeleza mpango huu!!

Mkuu wa Kijijini leo nimejionea maajabu leo kwa ile hotuba .Nimeshangaa mno
 
...to move forward CCM & Mkwere JK must go,lakini sioni akienda hata kwa ballot box 2010,wananchi wanaompa kazi wana deserve huyu bwana na yote yanayoendelea....na kama kitu kilichonihakikishia JK tunaye mpaka 2015 ni ule uchaguzi wa Kiteto ulioipa CCM landslide huku ufisadi ukiwa katika peak na news zote zilikuwa wazi nini kinaendelea lakini what happened? Lowassa kajiuzuru kwa kashfa kubwa kama ile ambayo imefanya suffering kwa nchi nzima lakini kaishiwa kupewa red carpet,Karamagi ndio na mkataba umeongezwa ingawaje ukiangalia vizuri kuna utapeli ulitokea walipopewa mara ya kwanza,Mkapa ndio huyo tumeambiwa tumwache mzee apumzike na tuna kidomo domo,acha njaa ziwapige wananchi labda watapata akili!
 
Mkuu wa Kijijini leo nimejionea maajabu leo kwa ile hotuba .Nimeshangaa mno
Mkuu si ilikuwa aibu mule ndani.....nahisi ulitafuta sehemu ujifiche baada ya kusikia pumba za Vasco da gama.....
 
Back
Top Bottom