Ilimu ya tanzania haifikii malengo yake.

NGOWILE

JF-Expert Member
Sep 8, 2011
454
258
Lengo kubwa la elimu ni kumuandaa mtu ili aweze kukabiliana na mazingira yanayomzunguka.Si lengo la elimu mtu kuzunguka na vyeti kutafuta kazi za ofisini tu.Katika fikra za MWALIMU alisema elimu ya Tanzania ni lazima imuandae mtanzania ili aweze kujitegemea mwenyewe ikiwa ni pamoja uwezo wa kuwa na fikra sahihi pamoja maamuzi sahihi(mambo sahihi hutokana na fikra sahihi)
-Asilimia kubwa ya walimu wa Tanzania wamekuwa walimu baada kukosa nafasi kwenye taaluma nyingine.
-Wanafunzi wengi wa shule za msingi wanakaa chini na wengine chini ya miti.
-Walimu wachache waliopo hawana maslahi ya kutosha hivyo wamekata tamaa.
-Asilimia kubwa ya walimu ni wale waliofaulu viwango wa chini sana kwenye elimu ya sekondari.
-Idadi kubwa ya wanafunzi darasani kuliko uwezo wa darasa.
-Shule kukosa nyumba za walimu.
-Kutokuwa na bodi ya walimu.
-Mtihani shule za msingi kuwa na maswali ya kuchagua tu(multiple choice) mpake hesabu.
KWA KUZINGATIA NILIYOYATAJA,LENGO LA ELIMU TANZANIA LINAFIKIWA?
 
Back
Top Bottom