Ilikuwa Sawa CUF Kukosa Urais!

X-PASTER

JF-Expert Member
Feb 12, 2007
11,610
1,809
Kwa haya ya Hamad Rashid, Maalim Seif:
Ilikuwa sawa CUF kukosa Urais

YAPO madai kutoka Chama Cha Wananchi, CUF, na kwa wananchama wake kwamba chama chao kimekuwa kikishinda nafasi ya urais miaka yote toka ulipoanza mfumo wa vyama vyingi nchini.

Na kwa hakika yapo madai pia kuwa hata katika uchaguzi mkuu wa mwaka jana uliotupa serikali ya umoja wa kitaifa baada ya maridhiano ya CCM na CUF, wapo baadhi ya wana-CUF wana amini kwamba nafasi ya Maalim ilikuwa iwe ya Mheshimi wa Shein kwa maana kuwa aliyeshinda alikuwa Maalim Seif ila tu baada ya kuona kumefanyika uchakachuaji, akakubali yaishe akiweka mbele masilahi ya Zanzibar.

Lakini kama tulivyosoma, hayo ni madai. Hatujui hakika yake. Lakini hebu fikiria hali ingekuwaje kama ukijaaliya kwamba hivi sasa CUF ndiyo ingekuwa imeshika ‘dola ya Zanzibar’. Hebu jaaliya kwamba hivi sasa Maalim Seif Sharif Hamad angekuwa ndiye kakalia kiti pale Ikulu akiongoza SMZ, lakini wanao mzunguka ni akina Hamad Rashid wakilumbana “wewe msaliti”, “huyu kala fedha za chama”, “huyu dikiteta anauwa chama” na maneno mengine kama hayo ambayo hivi sasa Hamad Rashid wanarushiana na viongozi wa ngazi za juu CUF!

Ambalo la kufikiria hapa ni kuwa kama chama kinafikia mahali kuwa na viongozi waandamizi na wanachama wanaofikia kuingia katika Bunge, lakini hakuna nidhamu wala kuheshimu taratibu na kanuni za kukosoana na kusawazisha mambo ndani kwa ndani wakitoka nje ni wamoja wakiongoza wanachama wao na wananchi kwa ujumla; hivi wakishika Ikulu, hiyo nidhamu ya kuongoza serikali wataitoa wapi?

Je, haitakuwa mtindo huu huu wa kulumbana mawaziri, Rais na Makamo wake au Waziri Kiongozi kama inavyotokea hivi sasa kwa Hamad Rashid na Maalim Seif?

Bila kujali madai yanayotolewa na pande zote mbili na bila kujali uwongo na ukweli wa madongo yanayorushwa na kila upande, Hamad Rashid na Maalim Seif; lakini hii imeonesha udhaifu mkubwa sana katika uongozi wa chama hicho.

Kwa hakik a yanayo tokea na kufanyiwa karamu katika magazeti, hayatoi taswira na hadhi ya CUF ambayo imejikusanyia umaarufu na kujenga imani kwa Watanzania wengi.

Kama yale madai kuwa CUF ilikuwa ikishinda kiti cha urais Zanzibar (na Tanzania?), lakini matokeo yaki chakachuliwa; huenda waliokuwa wakichakachua walikuwa wakiijua vyema CUF kuliko wananchiwalioipigia kura.

Tunachotaka kusema hapa ni kuwa kwa hakika itakuwa ni hatari kukipa dhamana na amana ya uongozi, chama ambacho kila kukicha akitoka Mapalala na Nyaruba huyu anakuja mwingine.

Sio siri kwamba katika uchaguzi mkuu wa kwanza wa vyama vingi nchini mwaka 1995 aliyekuwa mgombea ubunge jimbo la Bukoba Mjini, Wilfred Rwakatare, ilikuwa akipanda jukwaani anaomba kura awe mbunge kupitia CUF, lakini badala ya kumpigia kampeni mgombea urais kupitia CUF, Profesa Ibrahim Lipumba, alikuwa akimpigia kampeni mgombea wa NCCR-Mageuzi, Augustino Lyatonga Mrema. Sasa huyo pamoja na ubunge kupitia CUF, lakini pia alikuwa ndiye Naibu Katibu Mkuu wa CUF. Unatarajia nini katika chama kama hicho?

Ukirejea yale ya akina Salum Msabaha, na sasa haya ya Hamad Rashid Vs Maalim Seif, yanaibuka maswali mengi kuliko majibu.

Viongozi wa CUF, ni viongozi wa chama kweli cha upinzani au wanacheza ‘gemu? Je, wanafanya usanii? Kama ni viongozi kweli wa chama cha upinzani, wana umakini gani katika kupata wanachama na viongozi katika ngazi mbalimbali kuepuka kukusanya mamluki ambao muda wowote wanaweza kutumika kukivuruga chama?

Wanachama wa CUF Pemba na Unguja, Visiwani na Bara, wamefanya kazi kubwa sana, na wamejitoa muhanga kwa kiasi kikubwa sana kuifikisha CUF hapo ilipo wakitaraji kupata Haki Sawa kwa Wote. Sasa huu ni wakati wa Hamad Rashid na Maalim Seif Sharif Hamad kuwaonesha wanachama hao kuwa hawakuwa wamepotea maboya wakadandia chama ambacho ni bogi na kichaka cha mapandikizi.

Wasidhani kuwa wanachama wao wanapenda na kufurahia umahiri wao wa kurushiana madongo katika magazeti.

Wajue tu kuwa kuendeleza malumbano hayo kutawafanya wanachama wao kuwaweka katika kapu moja na wale mapandikizi wanaogombea Udiwani kupitia CUF, lakini kura ya Urais wanampa Slaa au mgombea wa CCM.

Huu ni usaliti kwa wanachama wao.https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/208088-mwaka-mpya-na-miungu-ya-kisiasa.html


[h=1]soma: Mwaka Mpya Na Miungu Ya Kisiasa[/h]
 
Kura chini ya milioni moja si rahisi kuzichakachua....
Ila naamini Maalim alimshinda Idris Abdulwakil na alimshinda Salmin..... siyo Karume wala Shein.
Wasimamizi kila kituo wapo wa CUF na CCM na waliridhia mahesabu kabla ya kupeleka kwenye tume.
 
Back
Top Bottom