ilibaki kidogo tu,niifahamu jinsia ya kongosho!!!!

Deejay nasmile

JF-Expert Member
Nov 8, 2011
5,759
5,289
basi bwana kongosho akaendelea kunitumia sms kuwa yupo mbagala pale mission,hivyo niende kukutana nae,kwa kuwa nilikuwa na shauku ya kujua ni mvurana au msichana nikachukua pikipiki yangu mpaka mbagala kwa kuwa muda huo nilikuwa mitaa ya keko pale.nikafika pale nikampigia simu kwa ile namba aliyonibip lakini kama kawaida hakupokea ili nisiisikie sauti yake ila akani sms,kuwa nimsubili dakika mbili.mzee mzima nikaamua kutulia sehemu nikiwa na shauku kubwa ya kukutana na kongosho alafu miwajuze watu humu jf kuwa kongosho ni jinsia flani,baadae kidogo sms ikaingia katika simu yangu ikasema hivi "nipo hapa karibu na internet cafe,njoo". SASA ile nataka niende tu ndipo kwa mbali nikasikia sauti ya mwenye nyumba ananigongea mlango kwa nguvu.Duh NDOTO yangu ikakata hapo hapo.nikaamka,nikatoka nje kufungua mlango nikakutana na mzee mwenye nyumba akitaka kodi yake.Ndio hivyo tena wakuu sikufanikiwa kukutanana na kongosho....
 
Sasa fanya hivi : tafuta mayai ya Bundi 7 , kisha yaweke uvunguni mwa kitanda unacholalia , mawili weka upande wa kichwani , mawili upande wa miguuni , na ma3 katikati.
Hiyo ndoto lazima itarudia ,
Note : Ukishamuota ukishtuka tu vunja hayo mayai mimina kwenye bakuli ile jelly liquid kisha vua nguo zote ujipake hiyo jelly ,mwili mzima haipiti siku 3 utakutana nae .
Kazi kwako .
 
sasa fanya hivi : Tafuta mayai ya bundi 7 , kisha yaweke uvunguni mwa kitanda unacholalia , mawili weka upande wa kichwani , mawili upande wa miguuni , na ma3 katikati.
Hiyo ndoto lazima itarudia ,
note : Ukishamuota ukishtuka tu vunja hayo mayai mimina kwenye bakuli ile jelly liquid kisha vua nguo zote ujipake hiyo jelly ,mwili mzima haipiti siku 3 utakutana nae .
Kazi kwako .

una undugu NA sheikh yah@@y@!!
 
Dah, nimepaliwa na mate usingizini lol
mbavu zangu mie

Deejay, ukitaka kuninasa kirahisi
am an addict wa fanta orange
kazi kwako na mbinu nshakupa
 
Deejay smile...

Mi nadhani uliwahi kulala,usingizi ukapotea saa kumi alfajiri..

Usingizi uliporudi saa 11 ndiyo mida hiyo kunakuwa na ndoto nyingi sana,ambazo si tu za uongo...,ni za kufikirika..
 
sasa ungejuaje jinsia yake? au mlikuwa mmepanga mmegane?
angalia avator ya huyo jamaa mwenye post namba2 uchukue maujuzi
 
Dah, nimepaliwa na mate usingizini lol
mbavu zangu mie

Deejay, ukitaka kuninasa kirahisi
am an addict wa fanta orange
kazi kwako na mbinu nshakupa

Not fairplay ! Mbona mie ulinipa mbinu ngumu kivile ? Na leo huyu unampa vimbinumbuzi ? Si unakumbuka hadi ilipofikia tunaonana kule Sharif shamba nilipata gharama kibao ?
 
Mimi najua jinsia yake lakini siwambii hata mkiniahidi zawadi. Naogopa akisemea kwa Moderators nitapigwa BAN. Kusingekuwa na sheria ya BAN ningewatajia alipozaliwa, shule ya msingi aliyosoma, shule aliyosomea O-level, shule aliyosomea A-level, chuo alichosomea First degree na chuo alichosomea Masters. Akinipa idhini nitawatajia. Kwa kifupi ana Masters ya TELECOM na anafanya kazi Vodacom. Ombeni idhini kwake nimwage all details zake.
 
Sasa fanya hivi : tafuta mayai ya Bundi 7 , kisha yaweke uvunguni mwa kitanda unacholalia , mawili weka upande wa kichwani , mawili upande wa miguuni , na ma3 katikati.
Hiyo ndoto lazima itarudia ,
Note : Ukishamuota ukishtuka tu vunja hayo mayai mimina kwenye bakuli ile jelly liquid kisha vua nguo zote ujipake hiyo jelly ,mwili mzima haipiti siku 3 utakutana nae .
Kazi kwako .
huu uganga wa kienyej sasa
 
.....Kongoshi ni "ME".... why do u bother.. nina muda mfupi sana hapa... ila nimemsoma ni "ME"
 
huu uganga wa kienyej sasa

Vaislay , umekosea hatuitagi hivo, tunaita "uganga wa Jadi au Tiba asilia"
Nianikie na wewe matatizo yako nikushughulikie fasta, au kama unaona ayubu hapa public wavimbamacho wengi niPM
 
Mimi najua jinsia yake lakini siwambii hata mkiniahidi zawadi. Naogopa akisemea kwa Moderators nitapigwa BAN. Kusingekuwa na sheria ya BAN ningewatajia alipozaliwa, shule ya msingi aliyosoma, shule aliyosomea O-level, shule aliyosomea A-level, chuo alichosomea First degree na chuo alichosomea Masters. Akinipa idhini nitawatajia. Kwa kifupi ana Masters ya TELECOM na anafanya kazi Vodacom. Ombeni idhini kwake nimwage all details zake.

matokeo yake ya olevel pliiz!
 
Kongosho ana div one ya points 7.Yumo katika orodha ya kumi bora kwa huo mwaka aliomaliza. Amepewa zawadi ya kula chakula cha mchana na waziri mkuu mh.Fredrick Sumaye kipindi hicho.

hongera sana kongosho! nani alilipa? Kongosho,sumaye au serikali?
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom