Ili tuendelee

sawabho

JF-Expert Member
Feb 25, 2011
5,286
3,107
wakati Tanzania inapata uhuru kulikuwa na msemo uliokuwa ukitumiwa na viongozi wa wakati huo kwamba "Ili tuendelee, tunahitaji Ardhi, Watu, Siasa Safi na Uongozi Bora". Kwa wakati ule walikuwa sawa maana walikuwa na ardhi, siasa safi na uongozi bora lakini idadi ya watu walikuwa wachache na wasiokuwa na utalaam na weledi uliotakiwa kwa maendeleo ya nchi. Leo hii baada ya miaka 50 ya uhuru vitu vyote vinne vipo- Ardhi nzuri yenye rutuba na kila madini na maliasiili; Watu zadi ya milioni 40 ambayo ni nguvu kazi tosha; Siasa safi kwa maana ya vyama vingi vinavyoikosoa Serikalia na Uongozi Bora kwa maana ya chama chenye uzoefu katika utawala na uongozi wa nchi kwa miaka 50.

Lakini mbona maendeleo ya kusua sua? Tatizo liko wapi. Je, huo usemi haukuwa na maana?
 
Ardhi ipo, Watu wapo... Je tunao Uongozi Bora?

Hatuna!

So lets keep daring and daring till we get Uongozi bora....
 
Back
Top Bottom