Elections 2015 Ilani ya CCM 2015-2020 - Uchaguzi Mkuu 2015

Kwanini waongelee katiba mpya wakati inangoja muda ufike ipelekwe kwa wananchi waipigie kura. Unataka wayarudie yale yale yaliyokwisha-pitishwa na BMK.

CCM ina ilani ya uchaguzi na wagombea wanaongelea mambo yaliyopo kwenye ilani ya uchaguzi.
mahakama ya mafisadi ipo kweny ilani, kasome mithali 26:4-5
 
Na ni kwanini ukawa wanaogopa agenda ya ufisadi kwenye kampeni zao?
Mmmmh, wameoga wapi? Richmond ndio unasema ufisadi, haya ongeza epa, twiga, vitalu, meremeta, deepgreen, escrow, uda, operesheni tokomeza, yote hayo ni ukawa mkubwa, kitaeleweka tu, simba trust unaijua, utaijua tu
 
Magufuli na Lowassa hakuna atakae kua tayari kujipunguzia madaraka kwa kupitisha Katiba ya Warioba.!
 
Kwanini waongelee katiba mpya wakati inangoja muda ufike ipelekwe kwa wananchi waipigie kura. Unataka wayarudie yale yale yaliyokwisha-pitishwa na BMK.

CCM ina ilani ya uchaguzi na wagombea wanaongelea mambo yaliyopo kwenye ilani ya uchaguzi.

Naona Warioba na akina Polepole wameshaufyata kwenye hii inshu ya katiba.Ama kweli pesa sabuni ya roho, Mbowe kazeni buti kuyaongoza haya mashambulizi makali ya msituni ili hatimaye october, 25 tumng'oe huyu mkoloni mweusi.
 
Wewe husikilizi au unatumia nini kusikiliza. Nini kirefu cha ukawa, na wanasema sana katiba ya wananchi ndio itatengenezwa

Lini katika kampeni zake Lowasa kasema hayo ya kutengeneza katiba ya wananchi iliyounda ukawa?
 
faizaFox Samia Suluhu alikuwa Makamu M/Kiti wa BMK chini ya Sita, alitumika kusigina katiba ya wananchi/Warioba!!
Hivyo anajua madhambi yake na kura za kihuni toka Zanzibari, sijui kama Watanzania ni mbumbu kiasi hicho, lazima Oct 25 watatoa adhabu!!
Huo ndio ukweli!!
 
Last edited by a moderator:
Habarini za jioni wakubwa, kuna hili jambo linanitaiza, nilitegemea magufuli na samia suluhu kwenye kampeni wangenadi katiba mpya iliyopitishwa na bunge maalum la katiba kuwa serikali yao itahakikisha wanaipitisha na kuwa katiba ya Tanzania.

Wapo kimya kwenye hili, kumbe ile katiba ni rasimu ni chafu sana na ilipitishwa katika mazingira ya giza hadi wao wanaonea aibu. Nakumbuka bunge maalum alikuwamo Samia na Magufuli lakini wanaona aibu kuiongelea, CHADEMA,NCCR Mageuzi, CUF, NLD wanaongelea katiba mpya hawa kimya kulikonii

Walichakachua rasimu?
Wanaona haya haoooooooooooooooooooooo?

Na badoooooooo. CCM kujeni hapa mjibu hili

Kama ukawa wanavyoona aibu kukemea mafisadi sasa.
 
Habarini za jioni wakubwa, kuna hili jambo linanitaiza, nilitegemea magufuli na samia suluhu kwenye kampeni wangenadi katiba mpya iliyopitishwa na bunge maalum la katiba kuwa serikali yao itahakikisha wanaipitisha na kuwa katiba ya Tanzania.

Wapo kimya kwenye hili, kumbe ile katiba ni rasimu ni chafu sana na ilipitishwa katika mazingira ya giza hadi wao wanaonea aibu. Nakumbuka bunge maalum alikuwamo Samia na Magufuli lakini wanaona aibu kuiongelea, CHADEMA,NCCR Mageuzi, CUF, NLD wanaongelea katiba mpya hawa kimya kulikonii

Walichakachua rasimu?
Wanaona haya haoooooooooooooooooooooo?

Na badoooooooo. CCM kujeni hapa mjibu hili

Title ya uzi wako ingekuwa KWA NINI WAPIGA KURA WANAOWASIKILIZA HAWAWAULIZI KATIBA YA WANANCHI IKO WAPI? Hebu nikuulize ukitaka kuku achinjwe ili upate kitoweo wa kumuuliza ni kuku au mchinjaji?
 
mahakama ya mafisadi ipo kweny ilani, kasome mithali 26:4-5

CCM huwa hatupigi porojo za kusadikika, kumbe hata ilani ya CCM hauijuwi?, jisomee:


  1. Katika kipindi cha miaka mitano ijayo, CCM itazielekeza Serikali zake kuendeleza mapambano dhidi ya adui rushwa kwa nguvu zake zote na kuendelea kuziba mianya ya rushwa katika taasisi za umma; kuchukua hatua kali na za haraka kwa wale wote watakaobainika kuendeleza rushwa Serikalini na katika sekta binafsi; na kuimarisha vyombo na taasisi zinazohusika na kuzuia na kupambana na rushwa; ikiwa ni pamoja na kuanzisha Mahakama Maalumu kwa ajili ya makosa ya rushwa na uhujumu uchumi.
 
CCM huwa hatupigi porojo za kusadikika, kumbe hata ilani ya CCM haiujuwi?, jisomee:


  1. Katika kipindi cha miaka mitano ijayo, CCM itazielekeza Serikali zake kuendeleza mapambano dhidi ya adui rushwa kwa nguvu zake zote na kuendelea kuziba mianya ya rushwa katika taasisi za umma; kuchukua hatua kali na za haraka kwa wale wote watakaobainika kuendeleza rushwa Serikalini na katika sekta binafsi; na kuimarisha vyombo na taasisi zinazohusika na kuzuia na kupambana na rushwa; ikiwa ni pamoja na kuanzisha Mahakama Maalumu kwa ajili ya makosa ya rushwa na uhujumu uchumi.

A joker!! hivi unaifahamu vizuri TZ au unajitoa ufahamu?? siku zote mlikuwa wapi kupambana na rushwa? rushwa imekuwa ni kama tabia ktk hili taifa mlikuwa wapi?
 
A joker!! hivi unaifahamu vizuri TZ au unajitoa ufahamu?? siku zote mlikuwa wapi kupambana na rushwa? rushwa imekuwa ni kama tabia ktk hili taifa mlikuwa wapi?

Nnaona huelewi kuwa mwaka 2005 wakati Kikwete anachukuwa nchi kulikuwa kuna kesi chini ya mia za rushwa, leo kuna kwa maelfu.

Pia ni wakati wa Kikwete tumeona mpaka waziri mkuu akiangushwa kwa ufisadi, usifikiri hiyo ilikuja kibahati mbaya tu.

Pia tumeona mawaziri wako jela.

Hiyo yote kama si mapambano na rushwa unafikiri ni nini? mchezo wa kuigiza?

Kufunguwa mahakama ya rushwa ni moja katika mapambano mazuri sana na rushwa, kumbuka na hilo pia.
 
katiba mpya ndio fimbo mpya itakayowapiga watanzania iwapo ccm watashinda,watakuja kusema wamechaguliwa na katiba yao,kwa ufupi hakutakuwa na tafauti yeyote baina ya awamu zilopita na zijazo zote za ccm na katiba hii
 
Iwapo watanzania wataichagua CCM tena mwaka huu ndo tutazidi kuwa masikini kwa kila hali.
 
Katika kipindi cha miaka mitano iliyopita, Serikali imeendeleza juhudi katika
kuhakikisha Sekta ya Madini inachangia kikamilifu katika kukuza uchumi na ajira.
Kutokana na juhudi hizo, mchango wa madini katika Pato la Taifa umeongezeka
kutoka asilimia 3.3 mwaka 2010 hadi asilimia 3.5 mwaka 2014. Kuimarika kwa sekta
hii kumetokana na kufanyika mambo yafuatayo:-
(a) Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) limewezeshwa kumiliki hisa kwenye
migodi ya STAMIGOLD (100%), Buchreef (45%), Buhemba (100%), Kiwira
(100%), Tanzaniteone (50%), Tulawaka (100%), NDC–Liganga (20%),
Mchuchuma (20%), Ngaka Coal Projects (30%) na Mgodi wa Almasi wa
Mwadui (25%);
(b) STAMICO imeanzisha Kampuni iitwayo Kyerwa Tin Company Limited (KTCL) ili
kununua madini ya bati kutoka kwa wachimbaji wadogo wa madini hayo huko
Kyerwa. Hadi kufikia Machi, 2015 jumla ya tani 71.3 zimenunuliwa kwa
gharama ya Shilingi 1,106,326,000. Aidha, tani 30 zimeuzwa kwa Dola za
Marekani 201,000;
(c) STAMICO imefanikiwa kupata kandarasi nne (4) za uchorongaji na utafiti wa madini yenye thamani ya Shilingi bilioni 1.35 ambapo jumla ya ajira mpya 78 zimepatikana kutokana na upatikanaji wa mashine za kisasaza uch
(d) Ofisi mbili za madini za Kanda zimeanzishwa; moja katika Kanda ya Ziwa
Nyasa inayohudumia Mikoa ya Njombe na Ruvuma; na nyingine kanda ya Ziwa
ambayo inahudumia Mikoa ya Mara na Simiyu ili kusimamia na kudhibiti
biashara ya madini. Kuanzishwa kwa ofisi hizo mpya kumeongeza idadi ya ofisi
za Kanda kufikia kumi (10) na hivyo kuongeza ufanisi kwa wadau wa sekta hii;
na
(e) Wakala wa Jiolojia Tanzania (GST) umeendelea kuwezeshwa kwa kupatiwa
fedha na vitendea kazi ili kuimarisha utendaji kazi wake. Katika kipindi hicho
Wakala wa Jiolojia amepata mafanikio yafuatayo:-
(i) Mfumo wa utunzaji, uchakataji, na usambazaji/uuzaji wa takwimu na
taarifa za upatikanaji madini ili kuvutia uwekezaji umeboreshwa;
(ii) GST imejiunga na COSOTA ili kusajili machapisho yake na kupewa haki
miliki (Copyright);
(iii) GST imejenga maabara ya kisasa ya kuchunguza miamba na madini
baada ya kununua vifaa muhimu na vya kisasa; na
(iv) GST imefanikiwa kufanya ugani na uchoraji wa ramani za upatikanaji wa
madini (geological and mineral occurrence mapping) kwa asilimia 92 ya
ardhi kavu ya Tanzania Bara.
(f) Idadi ya leseni za madini imeongezeka hadi kufikia 37,261 mwaka 2015
ambapo leseni za uchimbaji mkubwa ni 15; uchimbaji wa kati ni 380; uchimbaji
mdogo ni 33,131; na leseni za utafutaji madini ni 3,735. Watanzania
wanamiliki asilimia 70 ya leseni hizo, wageni asilimia 25 na asilimia 5 ya leseni
hizo zinamilikiwa kwa ubia kati ya Watanzania na Wageni;
(g) Wachimbaji wadogo wametengewa maeneo 25 yenye ukubwa wa kilometa za
mraba 2,407 na jumla ya leseni 8,800 zimetolewa kwenye maeneo hayo;
(h) Wachimbaji wadogo 10,000 wamepatiwa mafunzo ya huduma za ugani
(extension services) katika nyanja za kutambua umbile na tabia ya mashapo,
masuala ya utunzaji wa mazingira, utambuzi wa madini na uboreshaji wa
uchenjuaji madini;
(i) Jumla ya Shilingi milioni 909.5 zimetolewa kwa wachimbaji wadogo kama ruzuku
(j) Mpango wa utunzaji mazingira katika maeneo ya uchimbaji wa madini (Modern
Environmental Protection Plan) umeanzishwa na umewahamasisha wachimbaji
wadogo kutunza mazingira na kuepuka kuchafua vyanzo vya maji;
(k) Mikataba ya madini imepitiwa kwa lengo la kulinda maslahi ya nchi ambapo
baadhi ya vipengele vimefanyiwa marekebisho ili mrahaba ulipwe kwa kiwango
cha asilimia 4 ya mauzo ghafi ya dhahabu (gross value) badala ya asilimia 3 ya
mauzo halisi ya dhahabu (Net Back Value) iliyokuwa ikilipwa na wawekezaji
hapo awali;
(l) Migodi ya Bulyanhulu, North Mara, Buzwagi na Geita imeanza kulipa ushuru wa
huduma (service levy) kwa Halmashauri husika kwa kiwango cha asilimia 0.3
ya mapato ghafi ya migodi hiyo badala ya Dola za Kimarekani 200,000
zilizokuwa zinalipwa kwa mwaka;
(m) Wakala wa Ukaguzi wa Madini Tanzania (TMAA) imeanzisha madawati ya
ukaguzi kwenye viwanja vya ndege vya Kimataifa ili kudhibiti vitendo vya
utoroshaji wa madini nje ya nchi, hatua iliyowezesha kukamatwa madini yenye
thamani ya Shilingi bilioni 15; na
(n) Kamati Maalumu ya Kitaifa (National Local Content Committee) imeundwa ili
kusimamia mikakati iliyowekwa na wadau kuhakikisha kuwa Makapuni ya
Madini yanaongeza kiwango cha manunuzi ya bidhaa na huduma hapa nchini
kwa lengo la kuongeza ajira na soko la bidhaa za ndani.
35. Katika kipindi cha 2015 hadi 2020, Chama Cha Mapinduzi kitaielekeza
Serikali yake kutekeleza mambo yafuatayo ili kuendelea kukuza Sekta ya
Madini na kuongeza mchango wake kwenye Pato la Taifa:-
(a) Kuweka na kusimamia mfumo thabiti wa kukagua shughuli za migodi,
kukusanya takwimu za madini na kufuatilia maduhuli yatokanayo na madini
kwa malengo mapana ya kuongeza mapato ya Serikali;
(b) Kuweka na kutekeleza mikakati madhubuti ya kuvutia mitaji ya uwekezaji
katika Sekta ya Madini, hususan kwenye madini adimu (Rare Earth
Elements - REE);
(c) Kuhamasisha uzalishaji na masoko ya madini ya viwandani;
29
(d) Kuweka miundombinu muhimu (umeme, simu, maji, barabara) kupitia
ushirikiano wa Serikali na Sekta Binafsi (PPP) kwenye maeneo yenye
uwezekano wa kuanzishwa kwa migodi mikubwa mipya;
(e) Kuboresha mfumo wa utoaji na usimamizi wa leseni za madini, na
upatikanaji wa taarifa muhimu kwa wadau kuhusu Sekta ya Madini;
(f) Kuimarisha udhibiti na usimamizi wa upatikanaji, utunzaji, usafirishaji na
matumizi ya baruti katika shughuli za migodi;
(g) Kuendelea kuliimarisha Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) ili liweze
kushiriki kikamilifu kwenye shughuli za utafutaji, uchimbaji na utoaji
huduma katika Sekta ya Madini kwa niaba ya Serikali na Watanzania wote;
(h) Kuendelea kuujengea uwezo wa kifedha na rasilimali watu Wakala wa
Jiolojia Tanzania ili uweze kufikia kiwango bora zaidi katika ukusanyaji wa
takwimu na taarifa muhimu za kijiolojia na kijiofizikia zitakazosaidia katika
kuchochea kasi ya utafutaji na upatikanaji wa mashapo ya madini hapa
nchini yanayoweza kuchimbwa kwa faida;
(i) Kuendelea kuujengea uwezo Wakala wa Ukaguzi wa Madini Tanzania na
Ofisi za Madini Mikoani ili zijiimarishe katika kukagua na kusimamia shughuli
za uzalishaji na biashara ya madini nchini, na hivyo kuongeza manufaa
yatokanayo na Sekta ya Madini kwenye uchumi;
(j) Kusimamia na kuhamasisha uwekezaji katika shughuli za uongezaji thamani
madini ili kukuza mchango wa sekta hiyo katika Pato la Taifa;
(k) Kubuni na kutekeleza mikakati mahsusi itakayowezesha kupunguza au
kukomesha kabisa vitendo vya utoroshaji wa madini kwenda nje ya nchi na
biashara haramu ya madini nchini;
(l) Kuweka na kutekeleza mikakati maalumu itakayowezesha soko la Tanzanite
hapa nchini kuimarika zaidi na hivyo kuongeza manufaa yatokanayo na
madini hayo yanayopatikana Tanzania pekee;
 
Katika kipindi cha miaka mitano iliyopita, Serikali imeendeleza juhudi katikakuhakikisha Sekta ya Madini inachangia kikamilifu katika kukuza uchumi na ajira.Kutokana na juhudi hizo, mchango wa madini katika Pato la Taifa umeongezekakutoka asilimia 3.3 mwaka 2010 hadi asilimia 3.5 mwaka 2014. Kuimarika kwa sektahii kumetokana na kufanyika mambo yafuatayo:-(a) Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) limewezeshwa kumiliki hisa kwenyemigodi ya STAMIGOLD (100%), Buchreef (45%), Buhemba (100%), Kiwira(100%), Tanzaniteone (50%), Tulawaka (100%), NDC–Liganga (20%),Mchuchuma (20%), Ngaka Coal Projects (30%) na Mgodi wa Almasi waMwadui (25%);(b) STAMICO imeanzisha Kampuni iitwayo Kyerwa Tin Company Limited (KTCL) ilikununua madini ya bati kutoka kwa wachimbaji wadogo wa madini hayo hukoKyerwa. Hadi kufikia Machi, 2015 jumla ya tani 71.3 zimenunuliwa kwagharama ya Shilingi 1,106,326,000. Aidha, tani 30 zimeuzwa kwa Dola zaMarekani 201,000;(c) STAMICO imefanikiwa kupata kandarasi nne (4) za uchorongaji na utafiti wamadini yenye thamani ya Shilingi bilioni 1.35 ambapo jumla ya ajira mpya 78zimepatikana kutokana na upatikanaji wa mashine za kisasa za uchorongaji;27(d) Ofisi mbili za madini za Kanda zimeanzishwa; moja katika Kanda ya ZiwaNyasa inayohudumia Mikoa ya Njombe na Ruvuma; na nyingine kanda ya Ziwaambayo inahudumia Mikoa ya Mara na Simiyu ili kusimamia na kudhibitibiashara ya madini. Kuanzishwa kwa ofisi hizo mpya kumeongeza idadi ya ofisiza Kanda kufikia kumi (10) na hivyo kuongeza ufanisi kwa wadau wa sekta hii;na(e) Wakala wa Jiolojia Tanzania (GST) umeendelea kuwezeshwa kwa kupatiwafedha na vitendea kazi ili kuimarisha utendaji kazi wake. Katika kipindi hichoWakala wa Jiolojia amepata mafanikio yafuatayo:-(i) Mfumo wa utunzaji, uchakataji, na usambazaji/uuzaji wa takwimu nataarifa za upatikanaji madini ili kuvutia uwekezaji umeboreshwa;(ii) GST imejiunga na COSOTA ili kusajili machapisho yake na kupewa hakimiliki (Copyright);(iii) GST imejenga maabara ya kisasa ya kuchunguza miamba na madinibaada ya kununua vifaa muhimu na vya kisasa; na(iv) GST imefanikiwa kufanya ugani na uchoraji wa ramani za upatikanaji wamadini (geological and mineral occurrence mapping) kwa asilimia 92 yaardhi kavu ya Tanzania Bara.(f) Idadi ya leseni za madini imeongezeka hadi kufikia 37,261 mwaka 2015ambapo leseni za uchimbaji mkubwa ni 15; uchimbaji wa kati ni 380; uchimbajimdogo ni 33,131; na leseni za utafutaji madini ni 3,735. Watanzaniawanamiliki asilimia 70 ya leseni hizo, wageni asilimia 25 na asilimia 5 ya lesenihizo zinamilikiwa kwa ubia kati ya Watanzania na Wageni;(g) Wachimbaji wadogo wametengewa maeneo 25 yenye ukubwa wa kilometa zamraba 2,407 na jumla ya leseni 8,800 zimetolewa kwenye maeneo hayo;(h) Wachimbaji wadogo 10,000 wamepatiwa mafunzo ya huduma za ugani(extension services) katika nyanja za kutambua umbile na tabia ya mashapo,masuala ya utunzaji wa mazingira, utambuzi wa madini na uboreshaji wauchenjuaji madini;(i) Jumla ya Shilingi milioni 909.5 zimetolewa kwa wachimbaji wadogo kamaruzuku;28(j) Mpango wa utunzaji mazingira katika maeneo ya uchimbaji wa madini (ModernEnvironmental Protection Plan) umeanzishwa na umewahamasisha wachimbajiwadogo kutunza mazingira na kuepuka kuchafua vyanzo vya maji;(k) Mikataba ya madini imepitiwa kwa lengo la kulinda maslahi ya nchi ambapobaadhi ya vipengele vimefanyiwa marekebisho ili mrahaba ulipwe kwa kiwangocha asilimia 4 ya mauzo ghafi ya dhahabu (gross value) badala ya asilimia 3 yamauzo halisi ya dhahabu (Net Back Value) iliyokuwa ikilipwa na wawekezajihapo awali;(l) Migodi ya Bulyanhulu, North Mara, Buzwagi na Geita imeanza kulipa ushuru wahuduma (service levy) kwa Halmashauri husika kwa kiwango cha asilimia 0.3ya mapato ghafi ya migodi hiyo badala ya Dola za Kimarekani 200,000zilizokuwa zinalipwa kwa mwaka;(m) Wakala wa Ukaguzi wa Madini Tanzania (TMAA) imeanzisha madawati yaukaguzi kwenye viwanja vya ndege vya Kimataifa ili kudhibiti vitendo vyautoroshaji wa madini nje ya nchi, hatua iliyowezesha kukamatwa madini yenyethamani ya Shilingi bilioni 15; na(n) Kamati Maalumu ya Kitaifa (National Local Content Committee) imeundwa ilikusimamia mikakati iliyowekwa na wadau kuhakikisha kuwa Makapuni yaMadini yanaongeza kiwango cha manunuzi ya bidhaa na huduma hapa nchinikwa lengo la kuongeza ajira na soko la bidhaa za ndani.35. Katika kipindi cha 2015 hadi 2020, Chama Cha Mapinduzi kitaielekezaSerikali yake kutekeleza mambo yafuatayo ili kuendelea kukuza Sekta yaMadini na kuongeza mchango wake kwenye Pato la Taifa:-(a) Kuweka na kusimamia mfumo thabiti wa kukagua shughuli za migodi,kukusanya takwimu za madini na kufuatilia maduhuli yatokanayo na madinikwa malengo mapana ya kuongeza mapato ya Serikali;(b) Kuweka na kutekeleza mikakati madhubuti ya kuvutia mitaji ya uwekezajikatika Sekta ya Madini, hususan kwenye madini adimu (Rare EarthElements - REE);(c) Kuhamasisha uzalishaji na masoko ya madini ya viwandani;29(d) Kuweka miundombinu muhimu (umeme, simu, maji, barabara) kupitiaushirikiano wa Serikali na Sekta Binafsi (PPP) kwenye maeneo yenyeuwezekano wa kuanzishwa kwa migodi mikubwa mipya;(e) Kuboresha mfumo wa utoaji na usimamizi wa leseni za madini, naupatikanaji wa taarifa muhimu kwa wadau kuhusu Sekta ya Madini;(f) Kuimarisha udhibiti na usimamizi wa upatikanaji, utunzaji, usafirishaji namatumizi ya baruti katika shughuli za migodi;(g) Kuendelea kuliimarisha Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) ili liwezekushiriki kikamilifu kwenye shughuli za utafutaji, uchimbaji na utoajihuduma katika Sekta ya Madini kwa niaba ya Serikali na Watanzania wote;(h) Kuendelea kuujengea uwezo wa kifedha na rasilimali watu Wakala waJiolojia Tanzania ili uweze kufikia kiwango bora zaidi katika ukusanyaji watakwimu na taarifa muhimu za kijiolojia na kijiofizikia zitakazosaidia katikakuchochea kasi ya utafutaji na upatikanaji wa mashapo ya madini hapanchini yanayoweza kuchimbwa kwa faida;(i) Kuendelea kuujengea uwezo Wakala wa Ukaguzi wa Madini Tanzania naOfisi za Madini Mikoani ili zijiimarishe katika kukagua na kusimamia shughuliza uzalishaji na biashara ya madini nchini, na hivyo kuongeza manufaayatokanayo na Sekta ya Madini kwenye uchumi;(j) Kusimamia na kuhamasisha uwekezaji katika shughuli za uongezaji thamanimadini ili kukuza mchango wa sekta hiyo katika Pato la Taifa;(k) Kubuni na kutekeleza mikakati mahsusi itakayowezesha kupunguza aukukomesha kabisa vitendo vya utoroshaji wa madini kwenda nje ya nchi nabiashara haramu ya madini nchini;(l) Kuweka na kutekeleza mikakati maalumu itakayowezesha soko la Tanzanitehapa nchini kuimarika zaidi na hivyo kuongeza manufaa yatokanayo namadini hayo yanayopatikana Tanzania pekee;(m) Kuwawezesha wachimbaji wadogo kujiajiri kupitia sekta hii kwa kufanyayafuatayo:-30(i) Kuwatambua, kuwarasimisha na kuwapatia maeneo ya uchimbajimadini;(ii) Kuwapatia ruzuku, mafunzo, teknolojia na maarifa ya kisasa kwa ajiliya kuendeleza shughuli za uchimbaji;(iii) Serikali kupitia STAMICO kwa kushirikiana na wachimbaji wakubwakuwawezesha kupata mikopo na masoko; na(iv) Kuendelea kuongeza na kuwekeza mtaji wa Benki ya Rasilimali (TIB)ili iweze kutoa mikopo kwa wajasiriamali wadogo.(n) Kuendelea kuimarisha ukaguzi wa migodi katika masuala ya usalama,utunzaji wa mazingira na afya migodini; na(o) Kuhakikisha migodi yote mikubwa nchini inaendelea inanunua huduma nabidhaa kutoka hapa nchini kwa kiwango cha kuridhisha kwa kadri yaupatikanaji wake.
 
Swali la kujiuluza sekta ya madini imechangia pato la taifa inavyotakiwa.? Je mwananchi wakawaida ameona effect yake.? Tutolee mfano tu maaeneo yanayozunguka maeneo ya uchimbaji kama mwadui na geita wamenufaika hata KIDOGO.!? Otherwise mnaleta hadithi za abunuasi na kudhani watanzania ni wajinga.! CCM ya kuifuta tanzania kabisa tuanze na watu wanaofikiria kawaida.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom