Ikulu yamkana aliyemtesa ulimboka

Medical Dictionary

JF-Expert Member
Mar 12, 2012
1,057
309
WAKATI sakata la kutekwa, kuteswa na kisha kutupwa katika msitu wa Mwabwepande nje kidogo ya Jiji la Dar ss Salaam kwa Mwenyekiti wa Jumuiya ya Madaktari Nchini, Dk Steven Ulimboka, likiwa limefikia miezi mitatu, Ikulu imeibuka na kumkana mtumishi wake Ramadhan Ighondu anayetajwa kuhusika katika unyama huo.

Mwanzoni mwa wiki Dk. Ulimboka alitoa tamko akisema kwamba Ighondu ndiye aliyehusika na sakata la kumteka na kumtesa vibaya katika jaribio la kutaka kumuua.

Akizungumza na Tanzania Daima Jumamosi, Ikulu jana, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue, alisema kuwa hamfahamu mtumishi huyo aliyetajwa na Ulimboka. Alisisitiza kuwa Ikulu haipo kwa ajili ya kuteka na kutesa watu, hivyo wale wanaodai kuwa mtumishi wa ofisi hiyo anahusika na tukio hilo wanaongea tu.

"Wala simfahamu…Ikulu haipo kwa ajili ya kutesa watu na hao wanaomtaja mtumishi huyo kuwa yupo Ikulu hao wanazungumza tu," alisema.

Wakati Balozi Sefue akitoa kauli hiyo, juzi Mkurugenzi wa Mawasiliano Ikulu, Salva Rweyemamu, alisisitiza kuwa Ikulu haihusiki na
kwamba Rais Jakaya Kikwete alishalijibu suala hilo.

Katika tamko lake la kiapo lililotolewa kwa waandishi wa habari, Dk. Ulimboka, kupitia kwa wakili wa kujitegemea, Nyaronyo Kicheere, alisema anamfahamu mtesaji wake, na kwamba hata akikamatwa leo hii, atakwenda kufanya utambuzi.

Alisema anashangaa kwamba polisi wameshindwa kumtia mbaroni mtuhumiwa huyo, licha ya kwamba alishatajwa na gazeti la MwanaHALISI na katika mtandao wa YouTube.

Alisema: "Nathibitisha kwamba Ramadhan Ighondu alitambulishwa kwetu kwa jina la Abeid. Binafsi ninamfahamu sana bwana huyu kwa sababu alikuwa akitumwa mara kwa mara kuja kukutana na mimi na tumekutana mara kadhaa kabla ya tukio lile.

"Nathibitisha kwamba mfanyakazi huyu wa Ikulu, ndiye aliyenipigia simu na kuniita kwenye kikao ambacho muda mfupi baadaye nilitekwa. Katika mawasiliano hayo, Abeid alikuwa anatumia simu namba 0713 760473."

Dk. Ulimboka aliongeza kuwa, anakumbuka kuwa Abeid alitambulishwa kwake na kigogo mmoja, akiwa na wawakilishi wengine wa madaktari, kuwa ndiye angehusika katika kuchukua madai na hoja za madaktari katika mgogoro kati yao na serikali.

Kauli ya jana ya Balozi Sefue ni ya tatu kutolewa na Ikulu kuhusu Dk. Ulimboka. Mara ya kwanza, ilitolewa na Rais Jakaya Kikwete
alipokutana na baadhi ya wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari ambapo alisema, "Dk. Ulimboka ana nini mpaka Ikulu imteke? Tumteke ili iweje?"

Kikwete alikwenda mbali zaidi na kusema hata Dk. Ulimboka mwenyewe alipokwenda Ikulu akiwa na viongozi wenzake, alinyamaza kimya tu na kwamba waliokuwa wakizungumza ni wengine.

Hata hivyo, kwa kuwa Ikulu imesema haihusiki, na Dk. Ulimboka mwenyewe ametamka kwamba anamjua aliyemtesa, na kwamba anafanya kazi Ikulu, ni juu ya umma kuamua nani anasema ukweli.

Juni 26, mwaka huu, Dk. Ulimboka alitekwa, akapigwa, akang'olewa kucha kabla ya kuokotwa msitu wa Mabwepande na kupelekwa katika Taasisi ya Mifupa ya Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (Moi) kwa matibabu. Hata hivyo, baadaye alipelekwa Afrika Kusini kwa matibabu zaidi na alirejea nchini Agosti 12, mwaka huu.

Source: Tanzania Daima
 
Dr. Ulimboka amejichanganya katika hayo maelezo yake, Rama ni mfanyakazi wa TISS, na siyo Ikulu, ila haijaondoa ukweli kuwa Serikali dhalimu ya CCM ndiyo iliyopanga kumuua Dr. Ulimboka baada ya kushindwa kujibu hoja zake.
 
Huyo Ighondu ni askari au Usalama wa taifa? na yule mkenya waliyempakazia kesi vp yuko wapi?
 
Dr. Ulimboka amejichanganya katika hayo maelezo yake, Rama ni mfanyakazi wa TISS, na siyo Ikulu, ila haijaondoa ukweli kuwa Serikali dhalimu ya CCM ndiyo iliyopanga kumuua Dr. Ulimboka baada ya kushindwa kujibu hoja zake.

Si unajua hawa staff wa TISS wanapokuwa uraiani hujitambulisha kama wafanyakazi wa ofisi ya rais na ukienda wilayani hujitambulisha kama afisa tawala na ndio maana Dr. nadhani akajichanganya na kusema mfanyakazi wa Ikulu
 
Dr. Ulimboka amejichanganya katika hayo maelezo yake, Rama ni mfanyakazi wa TISS, na siyo Ikulu, ila haijaondoa ukweli kuwa Serikali dhalimu ya CCM ndiyo iliyopanga kumuua Dr. Ulimboka baada ya kushindwa kujibu hoja zake.

Mkuu FF,

Yeye Uli anasema alivyotambulishwa. Sasa ninyi wenye kujua vizuri anwani yake mhalifu ndio mumsaidie na kuisadia jamii kufahamu kilichotendeka ili mwisho wa siku ukweli na haki vichukue mkondo wake.

Nafurahi kuwa umeliweka vizuri kwamba mtuhumiwa mkuu ni Serikali ya JK.
 
Dr. Ulimboka amejichanganya katika hayo maelezo yake, Rama ni mfanyakazi wa TISS, na siyo Ikulu, ila haijaondoa ukweli kuwa Serikali dhalimu ya CCM ndiyo iliyopanga kumuua Dr. Ulimboka baada ya kushindwa kujibu hoja zake.

TISS si taasisi nje ya Ikulu(Presidence); kiuhalisi ni taasisi ndani ya Taasisi ya umma inayoitwa Ikulu. Ni jambo la ajabu kukana hilo, lakini inatuaminisha wengine jinsi serikali hii na viongozi wote walivyodhaifu.
 
Awe mtumishi wa TISS au Polisi wote ni watenda kazi wa Serikali inayoongozwa na JK chini ya chama cha mapinduzi {ccm}, hivyo hawawezi kukwepa kuhusika kwa serikali. Ingekuwa Dr. Ulimboka kamtaja prof. Lipumba au Mh. Freeman Mbowe kuwa alihusika na jaribio hilo la kumwua, je serikali ingebabaika kumkamata na kumhoji mtuhumiwa?
 
Dr. Ulimboka amejichanganya katika hayo maelezo yake, Rama ni mfanyakazi wa TISS, na siyo Ikulu, ila haijaondoa ukweli kuwa Serikali dhalimu ya CCM ndiyo iliyopanga kumuua Dr. Ulimboka baada ya kushindwa kujibu hoja zake.

Mkuu, kwani TISS wanawajibika wapi?
 
Back
Top Bottom