Ikulu yadaiwa kuhusika kutoroshwa kwa twiga

kibugumo

JF-Expert Member
Jun 19, 2011
1,448
386
Kwa mujibu wa gazeti la mwananchi toleo la jana jumapili,inadaiwa kuwa baadhi ya maafisa wa ikulu wanahusika katika
sakata la kutorosha twiga wanne na nyara nyingine za serikali hapo mwishoni mwa mwaka jana.Inasemekana haiwezekani
ndege kubwa tena ya kijeshi iingie nchini kinyemela bila ikulu kufahamu.Pia ilitegemewa idara nyeti za serikali kama usalama
wa Taifa na wizara ya mambo ya nchi za nje ingeweza kutolea ufafanuzi juu ya sakata la ndege ya jeshi la QATAR kuingia nchini na kutorosha mali ya taifa.KWELI TANZANIA NI SHAMBA LA BIBI.sijui wadau mnasemaje kwenye hili.
 
Acha waleee mpaka wavimbiwe!!,wafanye wanavyotaka,wajilimbilikie wawezavyo...mpaka pasibaki kitu hapa...nadhani hapo furaha yao itakuwa kuu
 
Tafua mwananchi la jana jumapili habari za kitaifa then utapata link yote kama ulikuwa
hujafuatilia habari yenyewe toka mwanzo.Kwa kukujuza tu ni kuwa habari yenyewe
ilifichuliwa na gazeti la raia mwemw.
 
hapa kweli ni shamba la bibi tena bibi kizee yaani NEMBO yA TAIFA imeuzwa/imeibwa hii ni aibu kubwa sana kwa nchi na vyombo vyetu vya usalama
lakini mimi naona hapa jambo ninaloshangaa hoo wanyama walitolewa huko kwenye ifadhi askari walikuwa wapi?
 
Unategemea askari atafanya nini ilhali kuna mtu mwenye nguvu?Kwa taarifa yako wakati sakata lenyewe
linatokea kulikuwa na askari mmoja hapo uwanjani KIA wa kituo kidogo cha hapo uwanjani,alipojaribu kuhoji
hata kuona document alikaripiwa kama mtoto mdogo,na alipotoa ripoti kwa bosi wake ndege ilishaondoka.
 
Ikulu yatajwa sakata la kutoroshwa Twiga Send to a friend
Sunday, 19 June 2011 07:56
0diggsdigg

Daniel Mjema,Moshi
WINGU zito bado limezingira tukio la utoroshaji wanyamapori hai wakiwemo Twiga kwenda Doha nchini Qatar huku baadhi ya maofisa wa Ikulu na wale wa mamlaka ya mapato Tanzania (TRA) wakitajwa kufahamu mpango huo.

Kutajwa kwa maofisa wa Ikulu kunatokana na ukweli kuwa ndege iliyotumika kutorosha wanyama hao inadaiwa kuwa ni ya Jeshi la Qatar jambo linaloibua maswali kuwa iliingiaje anga la Tanzania bila Ikulu kufahamu.

"Ndege iliyobeba ni ya Qatar Emir Air Force (ya jeshi) na kwa ufahamu mdogo ni kwamba ili ndege kama hiyo ije nchini ni lazima kuwe na mawasiliano kati ya nchi na nchi,"kilidokeza chanzo kimoja cha kuaminika.

Habari zilizolifikia Mwananchi Jumapili ambazo hazijathibitishwa zinadai kuwa kulikuwa na mawasiliano kati ya Ikulu, ubalozi wa Tanzania nchini Qatar na utawala wa kifalme wa Qatar hadi ndege hiyo kupata kibali cha kutua nchini.

"Ukitazama sakata zima hili bado kuna watu wazito hawajakamatwa ambao walishiriki ama kwa kujua au kwa kutofahamu kwa sababu si jambo la kawaida ndege ya nchi nyingine kutua nchi nyingine bila mawasiliano,"kimedai.

Habati hizo zinadai kuwa ndege hiyo ilipewa kibali cha kutua nchini kwa kile kinachodaiwa kuwa ilikuwa imebeba familia ya kifalme, hali iliyofanya isitiliwe shaka hata ilipokuwa ikipakia Wanyama hao Novemba mwaka jana.

Afisa mmoja mwandamizi katika uwanja wa Ndege wa kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) amedokeza kuwa yupo afisa mmoja wa TRA aliyesaini hati kuidhinisha kupakiwa kwa Wanyamapori hao lakini, hadi sasa hajakamatwa.

Meneja wa TRA mkoa Kilimanjaro, Patience Minga alikaririwa akisema ofisa anayetajwa katika nyaraka hizo alishastaafu mwaka jana hivyo TRA haizitambui nyaraka hizo na haziwezi kutambuliwa kama za mamlaka hiyo.

Wakati wadau wa mazingira wakiibua utata huo, Mahakama Kuu imeruhusu dhamana kwa washitakiwa wote sita wanaotuhumiwa kuhusiuka na kashafa hiyo lakini ikaweka masharti magumu saba wanayopaswa kuyatekeleza.

Uamuzi huo ulitolewa juzi mjini Moshi na Jaji Moses Mzuna wa Mahakama Kuu kanda ya Moshi ambapo aliamuru kila mshitakiwa katika kesi hiyo akabidhi mahakamani fedha taslimu Sh14.2 Milioni au mali yenye thamani hiyo.

Katika uamuzi wake huo, Jaji Mzuna alisema katika kufikiria ombi la dhamana la washitakiwa hao, Mahakama iliweka katika mizania matakwa ya mshitakiwa mmoja mmoja na matakwa ya Jamii na kufikia uamuzi huo.

"It is a bit strange (ni jambo linaloshangaza) ukisikia tukio hili lakini kwa vile bado upelelezi unaendelea, nisingetaka kusema mengi lakini katika kufikia uamuzi huu nimeweka katika mizania matakwa ya pande zote mbili"alisema.

Alifafanua kuwa sheria ya uhujumu uchumi ikisomwa pamoja na ile ya mwenendo wa maosa ya jinai (CPA) inataka mshitakiwa anayeomba dhamana kuweka mahakamani nusu ya fedha za thamani ya kosa alilolitenda.

Katika kesi hiyo, washitakiwa hao wanatuhumiwa kusafirisha Wanyamapori hai wenye thamani ya Sh170, 572,500. Nusu ya fedha hizo ni Sh85, 286,250 ambazo zikigawanywa kwa washitakiwa sita inakuwa Sh14, 214,375.

Kwa mujibu wa Jaji Mzuna, mbali na kulipa fedha taslimu kortini, aliwataka washitakiwa kuwa na wadhamini wawili ambao ni wakazi wa mkoa wa Kilimanjaro watakaosaini hati ya dhamana ya Sh14,214,375.

Masharti mengine ni pamoja na kuwataka mshitakiwa wa kwanza,Kamran Ahmed ambaye ni raia wa Pakistan na wa nne, Jane Mbogo ambaye ni raia wa Kenya, kukabidhi hati zao za kusafiria kituo kikuu cha polisi mjini Moshi.

Sharti lingine linawazuia washitakiwa kuingilia mashahidi na upelelezi wa kesi huku sharti la tano likiwa ni kutosafiri nje ya mkoa wa Arusha na Kilimanjaro bila kibali cha maandishi kutoka kwa msajili wa Mahakama Kuu Moshi.

Halikadhalika washitakiwa hao wanaotetewa na mawakili Median Mwale anayesaidiana na Andrew Maganga, Patrick Paul na Rebeca Peter wametakiwa kutojishughulisha na biashara ya wanyamapori katika kipindi chote cha kesi.

Sharti hilo la sita la kuwazuia washitakiwa mmoja mmoja au kwa ujumla wao kujihusisha na biashara ya wanyamapori, linakwenda sambamba na kuwazuia washitakiwa wote kutotembelea Hifadhi yeyote ya Taifa nchini.

Washitakiwa wote Kamran Ahmed, Martin Kimati, Jane Mbogo,Veronica Beno na Locken Kimaro walifanikiwa kutumiza masharti hayo na kuachiwa kwa dhamana isipokuwa mshitakiwa wa pili Hawa Mang'unyuka.

Ikulu yatajwa sakata la kutoroshwa Twiga
Send to a friend

Sunday, 19 June 2011 07:56
0diggsdigg

Daniel Mjema,Moshi
WINGU zito bado limezingira tukio la utoroshaji wanyamapori hai wakiwemo Twiga kwenda Doha nchini Qatar huku baadhi ya maofisa wa Ikulu na wale wa mamlaka ya mapato Tanzania (TRA) wakitajwa kufahamu mpango huo.

Kutajwa kwa maofisa wa Ikulu kunatokana na ukweli kuwa ndege iliyotumika kutorosha wanyama hao inadaiwa kuwa ni ya Jeshi la Qatar jambo linaloibua maswali kuwa iliingiaje anga la Tanzania bila Ikulu kufahamu.

“Ndege iliyobeba ni ya Qatar Emir Air Force (ya jeshi) na kwa ufahamu mdogo ni kwamba ili ndege kama hiyo ije nchini ni lazima kuwe na mawasiliano kati ya nchi na nchi,”kilidokeza chanzo kimoja cha kuaminika.

Habari zilizolifikia Mwananchi Jumapili ambazo hazijathibitishwa zinadai kuwa kulikuwa na mawasiliano kati ya Ikulu, ubalozi wa Tanzania nchini Qatar na utawala wa kifalme wa Qatar hadi ndege hiyo kupata kibali cha kutua nchini.

“Ukitazama sakata zima hili bado kuna watu wazito hawajakamatwa ambao walishiriki ama kwa kujua au kwa kutofahamu kwa sababu si jambo la kawaida ndege ya nchi nyingine kutua nchi nyingine bila mawasiliano,”kimedai.

Habati hizo zinadai kuwa ndege hiyo ilipewa kibali cha kutua nchini kwa kile kinachodaiwa kuwa ilikuwa imebeba familia ya kifalme, hali iliyofanya isitiliwe shaka hata ilipokuwa ikipakia Wanyama hao Novemba mwaka jana.

Afisa mmoja mwandamizi katika uwanja wa Ndege wa kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) amedokeza kuwa yupo afisa mmoja wa TRA aliyesaini hati kuidhinisha kupakiwa kwa Wanyamapori hao lakini, hadi sasa hajakamatwa.

Meneja wa TRA mkoa Kilimanjaro, Patience Minga alikaririwa akisema ofisa anayetajwa katika nyaraka hizo alishastaafu mwaka jana hivyo TRA haizitambui nyaraka hizo na haziwezi kutambuliwa kama za mamlaka hiyo.

Wakati wadau wa mazingira wakiibua utata huo, Mahakama Kuu imeruhusu dhamana kwa washitakiwa wote sita wanaotuhumiwa kuhusiuka na kashafa hiyo lakini ikaweka masharti magumu saba wanayopaswa kuyatekeleza.

Uamuzi huo ulitolewa juzi mjini Moshi na Jaji Moses Mzuna wa Mahakama Kuu kanda ya Moshi ambapo aliamuru kila mshitakiwa katika kesi hiyo akabidhi mahakamani fedha taslimu Sh14.2 Milioni au mali yenye thamani hiyo.

Katika uamuzi wake huo, Jaji Mzuna alisema katika kufikiria ombi la dhamana la washitakiwa hao, Mahakama iliweka katika mizania matakwa ya mshitakiwa mmoja mmoja na matakwa ya Jamii na kufikia uamuzi huo.

“It is a bit strange (ni jambo linaloshangaza) ukisikia tukio hili lakini kwa vile bado upelelezi unaendelea, nisingetaka kusema mengi lakini katika kufikia uamuzi huu nimeweka katika mizania matakwa ya pande zote mbili”alisema.

Alifafanua kuwa sheria ya uhujumu uchumi ikisomwa pamoja na ile ya mwenendo wa maosa ya jinai (CPA) inataka mshitakiwa anayeomba dhamana kuweka mahakamani nusu ya fedha za thamani ya kosa alilolitenda.

Katika kesi hiyo, washitakiwa hao wanatuhumiwa kusafirisha Wanyamapori hai wenye thamani ya Sh170, 572,500. Nusu ya fedha hizo ni Sh85, 286,250 ambazo zikigawanywa kwa washitakiwa sita inakuwa Sh14, 214,375.

Kwa mujibu wa Jaji Mzuna, mbali na kulipa fedha taslimu kortini, aliwataka washitakiwa kuwa na wadhamini wawili ambao ni wakazi wa mkoa wa Kilimanjaro watakaosaini hati ya dhamana ya Sh14,214,375.

Masharti mengine ni pamoja na kuwataka mshitakiwa wa kwanza,Kamran Ahmed ambaye ni raia wa Pakistan na wa nne, Jane Mbogo ambaye ni raia wa Kenya, kukabidhi hati zao za kusafiria kituo kikuu cha polisi mjini Moshi.

Sharti lingine linawazuia washitakiwa kuingilia mashahidi na upelelezi wa kesi huku sharti la tano likiwa ni kutosafiri nje ya mkoa wa Arusha na Kilimanjaro bila kibali cha maandishi kutoka kwa msajili wa Mahakama Kuu Moshi.

Halikadhalika washitakiwa hao wanaotetewa na mawakili Median Mwale anayesaidiana na Andrew Maganga, Patrick Paul na Rebeca Peter wametakiwa kutojishughulisha na biashara ya wanyamapori katika kipindi chote cha kesi.

Sharti hilo la sita la kuwazuia washitakiwa mmoja mmoja au kwa ujumla wao kujihusisha na biashara ya wanyamapori, linakwenda sambamba na kuwazuia washitakiwa wote kutotembelea Hifadhi yeyote ya Taifa nchini.

Washitakiwa wote Kamran Ahmed, Martin Kimati, Jane Mbogo,Veronica Beno na Locken Kimaro walifanikiwa kutumiza masharti hayo na kuachiwa kwa dhamana isipokuwa mshitakiwa wa pili Hawa Mang’unyuka.

  • Thanks
Reactions: BAK
kama ni kweli je tutafika? Tafadhali wahusika hasa ikulu tunawataka watoe taarifa maramoja.
 
Kuna mengi yatagundulka kwenye sakata hili.

Mie yangu macho. lakini twiga wameshafika hapa.
 
sometimes back ikaja issue ya Loliondo na ikauzwa, haikuwa na tija yoyote kwa wakazi wa huko pamoja na Watanzania kwa ujumla wao! Hapa 'jembe' la uhakika, Bwana Stanslaus Katabaro (Mungu amlaze mahala pema peponi) akapoteza maisha.
Na hili linaibuka wakati huu wa JK (sijui ni nini atakufa safari hii kwa kufichua uozo huu
)!
Laana za mambo yote haya hazitaenda kwa hawa watawala bali zitaenda kwa Watanzania kwa kushindwa kuwaondoa katika nafasi zinazowawezesha kufanya haya madhambi yote!
 
Waja JF,

Silo tu hilo swala la Twiga peke yake last two week usiku nilkuwa na wacth Sky news TV(UK) zilitajwa nchi 7 za Africa kwa serikali zao zina husika kwa kura rusha kwa ajili ya kuuza aridhi kwa wageni wengi esp toka Europe na Marekani na Tanzania ilikuwa mojawapo na wakatuhuu viongozi wa serikali hizo kufanya hizo hujuma sasa hebu angalieni hii hali ndio yale Mwl. Alikuwa akisema uwekezaji huuu utaufikisha pabaya ndio haya sasa kumbe viongozi wetu ndipo wanapata mianya ya kula kwa kuuza rasilimali zetu kwa wageni kwa maslahi yao kisingizio uwekezaji na mwl. alisema kutakuwa na Matajiri wachache watakao shikilia viwanda vyetu hivi na sekta mbali mbali za umma na kunufaika wao na wananchi kutopata kitu kwa ushauri zaidi tafuteni speech ya May Mosi 1995 iliyofanyika Mbeya kweli mta jua Mwl. Aliona mbali sana na ndio haya yanatokea sasa viongozi wetu wamekuwa wanyonyaji kwa wananchi wao walio wachanguwa ukaburu mkubwa kuliko wote zaidi ya makaburu wa enzi izo
 
hakuna yeyote wa serkali hii ya CCm atakayekuwa tayari kuiokoa nchi hii katika ufisadi maana baba na mama zao ni wamoja
 
Kwa mujibu wa gazeti la mwananchi toleo la jana jumapili,inadaiwa kuwa baadhi ya maafisa wa ikulu wanahusika katika
sakata la kutorosha twiga wanne na nyara nyingine za serikali hapo mwishoni mwa mwaka jana.Inasemekana haiwezekani
ndege kubwa tena ya kijeshi iingie nchini kinyemela bila ikulu kufahamu.Pia ilitegemewa idara nyeti za serikali kama usalama
wa Taifa na wizara ya mambo ya nchi za nje ingeweza kutolea ufafanuzi juu ya sakata la ndege ya jeshi la QATAR kuingia nchini na kutorosha mali ya taifa.KWELI TANZANIA NI SHAMBA LA BIBI.sijui wadau mnasemaje kwenye hili.

Kuna jamaa yangu yupo KIA amenieleza kuwa kuna kambi ya jeshi inajengwa kinyemela pale KIA ili kudhibiti vitendo kama hicho cha ndege ya jeshi ya qatar kutua kia bila kibali. Alinijuza kuwa zamani kambi hiyo ilikuwapo ila waliivunja miaka mingi iliyopita na kupelekea kuwa na mianya mingi ya kivamizi kama ilivyotokea
 
Waja JF,
Silo tu hilo swala la Twiga peke yake last two week usiku nilkuwa na wacth Sky news TV(UK) zilitajwa nchi 7 za Africa kwa serikali zao zina husika kwa kura rusha kwa ajili ya kuuza aridhi kwa wageni wengi esp toka Europe na Marekani na Tanzania ilikuwa mojawapo na wakatuhuu viongozi wa serikali hizo kufanya hizo hujuma sasa hebu angalieni hii hali ndio yale Mwl. Alikuwa akisema uwekezaji huuu utaufikisha pabaya ndio haya sasa kumbe viongozi wetu ndipo wanapata mianya ya kula kwa kuuza rasilimali zetu kwa wageni kwa maslahi yao kisingizio uwekezaji na mwl. alisema kutakuwa na Matajiri wachache watakao shikilia viwanda vyetu hivi na sekta mbali mbali za umma na kunufaika wao na wananchi kutopata kitu kwa ushauri zaidi tafuteni speech ya May Mosi 1995 iliyofanyika Mbeya kweli mta jua Mwl. Aliona mbali sana na ndio haya yanatokea sasa viongozi wetu wamekuwa wanyonyaji kwa wananchi wao walio wachanguwa ukaburu mkubwa kuliko wote zaidi ya makaburu wa enzi izo
 
Kwa mujibu wa gazeti la mwananchi toleo la jana jumapili,inadaiwa kuwa baadhi ya maafisa wa ikulu wanahusika katika
sakata la kutorosha twiga wanne na nyara nyingine za serikali hapo mwishoni mwa mwaka jana.Inasemekana haiwezekani
ndege kubwa tena ya kijeshi iingie nchini kinyemela bila ikulu kufahamu.Pia ilitegemewa idara nyeti za serikali kama usalama
wa Taifa na wizara ya mambo ya nchi za nje ingeweza kutolea ufafanuzi juu ya sakata la ndege ya jeshi la QATAR kuingia nchini na kutorosha mali ya taifa.KWELI TANZANIA NI SHAMBA LA BIBI.sijui wadau mnasemaje kwenye hili.

Check this and the link below

The scale of recent land transactions: Who is involved and in what form?
There is a diversity of international participants involved in these land transactions. However, Middle Eastern
countries, like Saudi Arabia, Qatar, Kuwait and Abu Dhabi are some of the biggest investors. A study by the Wilson
Center states that these nations and East Asia were estimated to be controlling over 7.6 million cultivable hectares
overseas by the end of 2008.

The list of host countries participating in these land transactions is somewhat lengthy; a 2009 study by the
International Food Policy Research Institute (IFPRI) lists Ethiopia, Kenya, Malawi, Mali, Mozambique, Sudan,
Tanzania and Zambia as all being involved in allotting foreign land leases or purchase agreements. In addition, the
report from the UN Special Rapporteur on food security lists the main target countries in Africa as Cameroon,
Ethiopia, the Democratic Republic of Congo, Madagascar, Mali, Somalia, Sudan, Tanzania and Zambia.

http://relooney.info/0_NS4053_815.pdf
 
Haya ndiyo baadhi ya mambo ya kuangalia sana wakati tunandika katiba mpya. Check and control must be instutionalised. Where is transparency and accountability?
 
Back
Top Bottom